1. TIF News

TIF, Sharjah Charity zatoa msaada wa chakula Morogoro

JUMUIYA ya Sharjah Charity International kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kushirikiana na taasisi ya The Islamic Foundation (TIF), zimetoa msaada wa chakula kwa wakazi wa Kata ya Chamwino Mkoa wa Morogoro.

Chakula kitatochotosheleza mahitaji ya kipindi cha mwezi mmoja kwa kila kaya.

Akizungumza katika zoezi la ugawaji wa chakula, Mkurugenzi wa Idara ya Da’awa wa TIF, Sheikh Ismail Rajab Kundya amesema kaya zaidi ya 60 za Chamwino zimenufaika na msaada huo msaada huo wa chakula uliojumuisha unga wa ugali kilo 20, mchele kilo 20, maharage kilo 10, sukari kilo 5 na mafuta ya kupikia lita tatu kwa kila kaya.

Aidha, Sheikh Kundya aliongeza kuwa, huo ni utaratibu kwa TIF kupokea misaada kutoka kwa wahisani mbalimbali kutoka UAE na kwingineko duniani na kisha kuwafikishia walengwa wanaohitaji msaada huo.

Kwa upande wao, walionufaika na msaada huo walieleza furaha yao kwa msaada huo na kuwaombea dua viongozi na watendaji wa taasisi ya The Islamic Foundation kwa wema wao. Pia, waliitaka TIF isiishie hapo, bali waendelee kuwasaidia wao kwa mahitaji mengine na wenzao wengine wenye uhitaji popote Tanzania, na hata nchi za jirani.

Msaada huo ni muendelezo wa TIF wa kufanya kazi kama daraja, walipokea msaada kutoka kwa wahisani na kuwafikishia walengwa kwa weledi, ufanisi, uaminifu na uadilifu mkubwa.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close