1. TIF News

Rais Mwinyi ateta na viongozi wa TIF Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepongeza kazi zinazofanywa na Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za kuimarisha sekta ya huduma za maji safi.

Rais Dkt. Mwinyi aliyasema hayo wakati alipokutana na viongozi wakuu wa taasisi hiyo ikulu ya Rais, jijini Unguja. Msafara wa TIF uliongozwa na Mwenyekiti wake, Aref Nahdi,Ikulu ya Rais Jijini Zanzibar.

Mwinyi aliwaahidi viongozi wa TIF kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana nao. Pia, aliwakaribisha kufungua ofisi kisiwani humo ili kuimarisha huduma zao kwa wananchi.

Naye, Mwenyekiti wa The Islamic Foundation Aref Nahdi alimshukuru Rais Dkt. Mwinyi na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuiongoza Zanzibar na kazi nzuri aliyoifanya hivi mpaka hivi sasa.

Nahdi pia aliahidi TIF itashirikiana na serikali ya Mwinyi kutatua changamoto za wananchi. Pia, alimkabidhi Rais Mwinyi tuzo kutambua mchango wake kuwaunganisha Wazanzibar na kuendeleza visiwa hivyo kupitia uchumi wa bluu.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close