1. TIF News

Mwenyekiti CIFCA apigia chapuo mfumo wa fedha wa Kiislamu

Dkt. Mwinyi mgeni rasimi

kufanyika Hyatt Kilimanjaro Hotel

KUELEKEA Kongamano kubwa la Afrika la mfumo wa kifedha wa Kiislamu linalotarajiwa kufanyika wiki ijayo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kituo cha Masuala ya Huduma za Kifedha za Kiislamu na Ushauri Tanzania (CIFCA), Aref Nahdi ameahidi kuendelea kupigia chapuo mfumo wa fedha wa Kiislamu nchini.

Mwenyekiti Nahdi alisema kuna mambo mawili yanayohitaji msu-kumo mpya katika kuendeleza sekta hiyo nchini Tanzania.

Nahdi alisema kuwa jambo la kwanza na la muhimu zaidi ni kushirikiana na serikali kuhakikisha kunakuwa na sheria na kanuni zote za huduma za kifedha za Kiislamu ili kurahisisha udhibiti wake.

Jambo la pili ambalo Mwenyekiti Nahdi alisema linalohitaji msuku-mo mpya ni CIFCA kuwa na mpan-go endelevu wa kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo mbalimbali ili kuongeza uelewa wa wadau juu ya mfumo wa fedha wa Kiislamu.

Miongoni mwa programu kubwa za CIFCA za kufikisha elimu kwa umma ni vipindi kupitia TV Imaan na Radio Imaan vinavyoendeshwa na mtaalamu Sheikh Khalfan Abdallah.

Vipindi hivyo ni pamoja na ‘Uchumi wa Kiislamu na Ujasiria-mali’ ambacho kinaruka kila Iju-maa jioni saa moja hadi moja na nusu na kurudiwa Jumatatu saa 04:30 – 05:00 asubuhi na Jumanne saa 03:30 – saa 04:00 usiku. Kipindi kingine ni Trials of Wealth amba-cho kinaruka kila Jumatano saa 02:20 – 02:50 usiku na kurudiwa siku ya Alhamisi usiku saa 03:30 – 04:00.

Ukiacha vipindi hivyo, taarifa za mfumo wa fedha wa Kiislamu na CIFCA zimekuwa zikitolewa kati-ka vipindi vya habari na vingine maalumu. Kadhalika, Gazeti Imaan, tovuti na mitandao ya kijamii ya Imaan pia imekuwa ikishiriki kutoa elimu hiyo.

“Bila watu kuwa na uelewa hata tukiwa na sera, she-ria na kanuni zote bado hatuta-fanikiwa. Kwa hiyo, mambo haya mawili yanahitajika yafanyike kwa pamoja. Unahitaji taratibu nzuri za kisheria na kanuni ili watu washiriki kwenye mfumo huu kwa maslahi yao ya kidunia na akhera,” alisema.

Kuhusu mkutano huo unao-fanyika kila mwaka ikiwa hii ni mara ya 7, Nahdi alihimiza wadau kujisajili kushiriki ili kujifunza kwa undani masuala ya mfumo wa kifedha wa Kiislamu.

Mingoni mwa watakaowasilisha mada katika mkutano huo utakaofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency ni pamoja na aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali nchini Tanzania (CAG).

Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na taasisi ya AlHuda CIBE ya Umoja wa Falme za Kiarabu ikishirikiana na taasisi nyingine kadhaa ikiwemo CIFCA. Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF)ambayo Nahdi ni mwenyekiti wake, kupitia vyombo vyake vya habari pia ni sehemu ya washirika katika kuu-tangaza mkutano huo

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close