1. TIF News

Msikatishwe tamaa, tungesikiliza maneno TIF isingekuwepo – Nahdi

Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation (TIF), Aref Nahdi amewataka Waislamu wasikatishwe tamaa na wale wote wanaolisema vibaya kongamano la Miski ya Roho, na kwamba hata TIF yenye isingekuwepo kama wangesikiliza maneno ya watu.

Nasaha hizo zimetolewa katika Kongamano la Tatu la Kida’awa La Afrika Mashariki lijulikanalo kama ‘Misk ya Roho’ lililofanyika Jumapili Desemba mosi, 2019 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake ya kufunga kongamano, Nahdi alisema alisema kukata tamaa hakutasaidia lolote bali jambo linalohitajiwa kwa Waislamu ni kuungana pamoja na kushikana katika kuihami dini ya Allah kwa kuchangia juhudi za kuendeleza dini, jambo ambalo ndio litaleta mafanikio.

“Tusikatishwe tamaa na wale wanaotukatisha tamaa ili tusiendelee kufanya makongamano kama haya. Kama tungekubali kukatishwa tamaa hata The Islamic Foundation yenyewe isingekuwepo. Tushikamane, tuaminiane na vilevile tuweze kuwa na moyo wa kuchangia katika dini yetu. Mwenyekiti huyo wa TIF alisema, kitendo cha Waislamu kuchangia katika juhudi za dini ni kujitengenezea kesho yao, huko akhera.

Awashukuru wadhamini Aidha,

Nahdi aliwashukuru wadhamini wote waliofanikisha shughuli hiyo wakiwemo wadhamini wapya waliojitokeza mwaka huu, likiwemo Shirika la Ndege la Kimataifa la Emirates, iERA na Camel Flour Mills, hatua inayoonesha kuwa TIF inaaminika na wengi.

Miski ya Roho 2019 iliyofanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo ni kongamano linalohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake, na pia kuvutia watu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na nchi za jirani.

Kongamano hili pia limekuwa likifuatiwa duniani kote kupitia vyombo vya habari kama televisheni, redio, machapisho na mitandao ya kijamii. Kuonesha namna kongamano hilo linavyokualika, watu walipoulizwa kama wangetaka liendelee kwa kuitikia ‘Takbir’ iliyotolewa na Mwenyekiti, ukumbi ulirindima ‘Allahu akbar’, jambo ambalo Nahdi alisema linaonesha watu wangependa liwepo hata mara mbili kwa mwaka.

Watu walionekana kufurahi na kustafidi mada mbalimbali zilizohudhurishwa kwao, walipoulizwa na Mwenyekiti kama kuna umuhimu wa kuendelea na kuliandaa kongamano hilo, wanakongamano walisema wanalitamani liwe hata mara mbili kwa mwaka.

Licha ya mada zenye manufaa zinazohudhurishwa kwa hadhira, Miski ya Roho pia huleta pamoja masheikh mbalimbali katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ambao hubadilishana uzoefu wa kiutendaji katika mbinu za ulinganiaji.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close