1. TIF News

Kaya mia zafaidika na futari za TIF

ZAIDI ya familia mia moja Mjini Morogoro zimenufaika na msaada wa futari pamoja na daku kutoka kwa taasisi ya The Islamic Foundation utakaowezesha kukidhi mahitaji yao katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kaya hizo mia na ziada kidogo zilikabidhiwa sadaka hiyo katika hafla iliyofanyika makao makuu ya TIF. Baadhi ya vyakula vilivyokuwepo katika kifurushi kila kifurushi cha futari ni pamoja na mchele, sukari maharage, tende pamoja na unga wa ugali.

Wakizungumza na Sayari ya Imaan, wanufaika wa msaada huo wameishukuru TIF kwa msaada huo na kueleza kuwa utarahisisha ibada yao ya funga.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Da’awah, Sheikh Ismail Rajab Kundya ametaka wadau wazidi kusaidia wasiokuwa na uwezo.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close