1. TIF News

Dkt. Mwakyembe asifu uwekezaji, utendaji Imaan Media

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amevitembelea vituo vya matangazo vya Radio na TV Imaan vinavyomilikiwa na taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) na kutoa shukran zake na pongezi kwa utendaji uliotukuka.

Kadhalika, Waziri Mwakyembe amempongeza Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi kwa fikra nzuri ya kuanzisha vituo hivi pamoja na uwekezaji wa hali ya juu katika teknolojia ya habari.

Katika ziara yake hiyo, Waziri Mwakyembe alipata fursa ya kutembelea studio za vituo hivyo na kushangazwa na uwekezaji na weledi wa watendaji wa vituo hivyo.

Alikuwa ni Mwenyekiti Nahdi na viongozi wengine waandamizi wa taasisi hiyo ndio waliompokea mgeni wao na kumpa maelezo ya kina juu ya shughuli mbalimbali za taasisi hiyo.

Naye Waziri alitoa nasaha mbalimbali kwa Imaan Media juu ya namna ya kuboresha shughuli zao za utangazaji, ukizingatia kuwa yeye mwenyewe ni mtaalamu katika fani hii.

Mwenyekiti TIF alitumia ziara hiyo kumkabidhi tuzo Waziri Mwakyembe kutambua mchango wake mkubwa katika kuilea na kuiendeleza tasnia ya habari.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close