1. TIF News

Dar Al Ber Society ya UAE na TIF zakabidhi msikiti Unguja

Naomba muutunze vizuri msikiti huu na muutumie kwa kufanya ibada na kuwafundisha watoto Qur’an na elimu nyinginezo ili kuwaandaa waweze kukua kwenye misingi ya imani” (Sheikh Ibrahim Twaha).

Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) yenye makao yake makuu mkoani
Morogoro imekabidhi msikiti uitwao ‘Masjid Dhakarat’ kwa Waislamu wa eneo la Maungani katika mkoa wa mjini Magharibi Unguja.

Ujenzi wa msikiti huo umefadhiliwa na taasisi ya Dar Al Ber Society ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msikiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIF, Sheikh Ibrahim Twaha amewataka Waislamu kuutumia vizuri msikiti huo kwa kufanya ibada na kutoa elimu ya dini ya Kiislamu kwa watoto na watu wazima. “Naomba muutunze vizuri msikiti huu na muutumie kwa kufanya ibada na kuwafundisha watoto Qur’an na elimu nyinginezo ili kuwaandaa waweze kukua kwenye misingi ya imani,” alisema Sheikh Ibrahim na kuongeza kuwa kufunza watoto elimu ya dini ni jambo la wajibu linaloweza kumuingiza mtu peponi.

Wakielezea furaha yao wakati wa hafla ya kukabidhi msikiti huo, Waumini na viongozi wa msikiti huo walisema, sasa wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata msikiti ili kujumuika na wenzao katika ibada ya sala.

“Tunaishukuru taasisi ya Dar Al Ber Society kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kufadhili ujenzi wa msikiti huu kwani utatuwezesha kutekeleza ibada kwa murua na utulivu,’ alisema mmoja wa waumini hao, Makame Haji.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close