2. Taifa

Wazazi waaswa kusimamia tabia njema za vijana wao

Wazazi wa Kiislamu nchini wametakiwa kuwa na tabia ya kuwasimamia watoto wao mara baada ya kuhitimu masomo shuleni ili waendelee kuwa na tabia njema.

Wito huo umetolewa na mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Nuru Mruma wakati wa mahafali ya nne ya shule ya msingi na chekechea ya Ilala jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Kiislamu (IDF).

“Wazazi, niwaambieni hawa watoto wakati wako shule walikuwa wanasali, wanafunga. Hivyo, dhima inarudi kwenu ya kuhakikisha mnawasimamia watoto hawa mara baada ya kuhitimu masomo hapa shuleni,” alisema Mruma.

Pia Mruma alikemea ugomvi ndani ya misikiti akisema hali hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya misikiti na Uislamu kwa ujumla.

“Misikiti sio sehemu ya kuswalia tu, misikiti ni sehemu ya kupanga maendeleo ya Uislamu…sasa hivi misikiti mingi ina migogoro na ukiangalia chanzo ni maslahi tu,” alisema MRUMA.

Naye Mkurugenzi wa shule hiyo ya Kiislamu ya Ilalal, Mwinyi Kombo Ayub amewataka wazazi wa watu hao kuwaendeleza katika shule za Kiislamu ili waendelee kujengeka katika maadili mema na kuwa nuru kwa jamii.

Jumla ya wanafunzi 149 wamehitimu shuleni hapo na waliyofanya vizuri wamepewa zawadi mbalimbali.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close