2. Taifa

Walimu wa madrasa washauriwa kubadili mfumo wa ufundishaji

Walimu wa madrasa hapa nchini wameshauriwa kubadili mfumo wa utoaji elimu ya madrasa kwa kuwafundisha wanafunzi wao tafsiri ya kitabu kitukufu cha Qur’ an badala ya kuwasomesha na kuwahifadhisha pekee.

Wito huo umetolewa katika semina iliyowakutanisha walimu wa madrasa kutoka kata ya Chanika Minazi Saba, katika wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika semina hiyo iliyofanyika katika msikiti wa Tawfiq Chanika, Katibu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu wilaya ya Ilala, Sheikh Abdurahman Ali Salehe alisema, tija ya Qur’an itapatikana ikiwa vijana watafundishwa tafsiri ya kitabu hicho kitukufu na siyo kukisoma kwa mtindo wa kukariri tu.

Alisema, kuhifadhi Qur’an kwa kuzingatia maudhui na tafsiri yake kutawafanya wanafunzi kuwa na mwamko mkubwa na utambuzi wa kutosha.

Sheikh Salehe alidokeza kuwa, Qur’an ni kitabu kinachodhamini maisha ya Muislamu hapa duniani na kesho akhera, hivyo ni muhimu kwa wazazi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na walimu wa madrasa katika kuwasomesha na kuwahifadhisha watoto Qur’ an

Sanjari na hilo, Sheikh Salehe aliwataka walimu wa madrasa kutokatishwa tamaa na wazazi wanaoponda elimu ya dini na badala yake waongeze mbinu za ufundishaji ili kupandisha kiwango cha taaluma..

Show More

Related Articles

Back to top button
Close