2. Taifa

UAE kutumia Mil. 80 kuchimba visima vya maji Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge amemshukuru balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) hapa nchini, Khalifa Al Marzooqi kwa kukubali kuwachimbia visima vitatu vya maji katika mkoa wa Dodoma vitakavyogharimu zaidi ya shilingi milioni 80 za kitanzania.

Dkt. Mahenge ametoa shukrani hizo wakati akiongea na waandishi wa habari.

“Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Balozi wa UAE Mheshimiwa Khalifa Al Mazrooq kwa kutukimbilia kwani tunakabiliwa na changamoto kubwa ya maji katika baadhi ya wilaya za mkoa wetu wa Dodoma ikiwamo Kondoa na Bahi,” alisema Dkt Mahenge na kusema kuwa balozi huyo wa UAE amekuwa mfano wa kuigwa katika kusaidia huduma za jamii.

Dkt. Mahenge aliongeza: “Kipekee kabisa tunamshukuru Balozi Al Mazrooq kwa maamuzi yake ya upendo kwetu kwa kutusaidia kuchimba visima vitatu.”

Kwa mujibu wa Dkt. Mahenge visima hivyo vitachimbwa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa ili kupunguza adha ya ukosefu wa maji wanayoipata.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi na watendaji wa vyombo vya habari vya Tv na Radio Imaan kwa kazi nzuri wanayofanya katika kuielimisha jamii ya Watanzania.

“Kiukweli nawapongeza sana kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya kuelimisha na kuhabarisha jamii, endeleeni”, alisema na kuongeza:“Naomba vyombo vingine viige mfano huu mzuri wa wenzetu hawa.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close