2. Taifa

Sheikh aasa viongozi wa taasisi kuogopa dhima mbele ya Allah

Jamii ya Kiislamu hapa nchini imeaswa kuvitumia vituo ambavyo vimekuwa vikianzishwa kwa lengo la kuisaidia jamii ya Kiislamu, zikiwemo shule za ngazi mbalimbali, vinatekeleza kazi iliyokusudiwa katika uanzishwaji wake.

Jamii pia imetakiwa kuhakikisha vituo hivyo havitumiki kwa maslahi ya dunia kwa kuwa kufanya hivyo ni dhima kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.

Hayo yameelezwa na mlinganiaji wa dini Tukufu ya Kiislamu, Shekhe Ally Jumanne, wakati alipofanya ziara ya katika Kituo cha Kiislamu cha Kondoa, kinachomiliki shule ya msingi na sekondari. Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kujionea namna kituo hicho kinavyoendeshwa.

Akizungumza na viongozi wa kituo hicho, Sheikh Ally Jumanne ambaye ni Msimamizi wa Maadili na Maudhui wa vyombo vya habari vya utangazaji vya Imaan, aliwaasa wamiliki wa kituo hicho na vingine kama hivyo, kuvitumia kuisaidia jamii ya Kiislamu.

Moja ya namna aliyopendekeza ya kuwasaidia vijana ni kuwajenga katika maadili mema. Sheikh Ally Jumanne, ambaye ana ni msomi aliyepata Shahada yake katika Chuo Kikuu cha Madina, alizitaka taasisi hizo kutoa misaada kwa jamii ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikishindwa kumudu gharama za huduma bora za kielimu katika maeneo mengine, na siyo kutumika kwa maslahi ya kidunia Shekhe Ally Jumanne alisema,kumekuwa na wimbi kubwa la uanzishwaji wa vituo ambavyo vimekuwa na nembo ya Uislamu, lakini jamii inayozunguka vituo hivyo haipati msaada wowote au kunufaika. Sheikh Ally alikemea tabia ya kubadili vituo hivyo kuwa ni vya kibiashara jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likiuchafua Uislamu.

Katika hatua nyingine, mlinganiaji huyo ambaye mwaka jana alikuwa ni mmoja kati ya masheikh waliwasilisha mada katika kongamano la Misk ya Roho 2018, ameitaka jamii ya Kiislamu kuhakikisha wanawapeleka watoto kwa wingi katika kujifunza elimu ya dini, lakini bila kusahau elimu ya mazingira ambayo nayo ni muhimu katika dunia ya sasa ya utandawazi.

Nao viongozi wa kituo hicho wakiongozwa wamesema wamekuwa wakitoa msaada kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakishindwa kuendelea na masomo ikiwemo wale wa Tahfidhul Qur’an. Walisema, kiyuo kimekuwa kikiwafadhili na kuwahudumia wanafunzi hao kwa kila kitu kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close