2. Taifa

Al-Azhar yaitaka jamii kuisaidia serikali vita dhidi ya dawa za kulevya

Mwanachama wa Kituo cha Kiislamu cha Kimisri (Azhar Sharif), kilichopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam, Sheikh Abdul-Rahiim Swaleh Sayed, ameitaka jamii kutowaonea haya wafanyabishara na watumiaji wa dawa za kulevya kwa kuwa dawa hizo zina madhara makubwa kwa jamii.

Sheikh Sayed, aliyasema hayo hivi karibuni katika kongamano la maimamu na wahubiri wa dini ya Kiislamu, lililoandaliwa na Azhar Sharif, Tawi la Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam.

Sheikh Sayed alisema matumizi ya mihadarati ni tatizo sugu siyo tu hapa Tanzania bali duniani kote, na ndio maana nchi nyingi zinapambana kufa na kupona kuwadhibiti watu wanaojihusisha na biashara na matumizi ya mihadarati.

Sheikh Sayed aliwaasa maimamu na walinganiaji kuitahadharisha jamii juu ya hatari ya mihadarati kwani wao wana nafasi kubwa katika kuwashawishi Waumini wao kujiepusha na matumizi ya dawa hizo haramu.

“Wako waliojiingiza katika matumzi ya dawa za kulevya kwa sababu tu ya kuiga, wapo pia ambao hufanya hivyo kwa ajili ya tamaa ya kutaka starehe,” alisema Sheikh Sayed.

Alisema tabia ya wazazi wengi kuwanyamazia watoto wao ni miongoni mwa vyanzo vya ukuaji wa matumizi ya mihadarati zikiwamo dawa za kelvya. Mgeni rasmi katika kongamano hilo,Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, alisifu juhudi zinazofanywa na Azhar Sharif katika kueneza fikra za ukati na kati za Uislamu na kufikisha ujumbe wa Uislamu kuhusu amani, usamehevu na kupambana na maovu katika jamii.

Kongamano hilo lililohudhuriwa na watu takriban 50, lilishereheshwa na Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sheikhn Mohamed Hassan Attia, Mkuregenzi wa Kituo cha Kiislamu cha Kimisri (Azhar Sharif) Tawi la Tanzania, Sheikh Haji Saidi, Imamu wa msikiti wa Aziza uliopo wilaya ya Kigamboni na Dkt. Christian Mmbwasi kutoka idara ya kupambana na dawa za kulevya, Ofisi yaWaziri Mkuu.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close