1. Habari3. Kimatiafa

Wasomali Milioni 6 Wakabiliwa na Njaa Kali

Umoja wa mataifa(UN) umesema kuwa watu milioni 6.2 nchini Somalia wanakabiliwa na njaa kali kutokana na ukame ulioikumba nchi hiyo; na tayari mpaka sasa watu zaidi ya 100 wamekwishafariki. Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limeonya kuwa imesalia miezi mwili tu ili kuepeuka hali hiyo iliyowahi kulikumba taifa hilo mara tatu ndani ya miaka 25 iliyopita ambapo njaa ya mwisho ya mwaka 2011 iliuwa watu takribani 260,000. Pia imetajwa kuwa watoto takribani 363,000 wanakabiliwa na utapiamlo mkali na wanahitaji msaada wa haraka wa chakula. Jumanne wiki hii Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres aliwasili kwa dharura nchini Somalia ikiwa ni jitihada za kushawishi dunia itoe msaada kwa taifa hilo. Guterres alisema dunia inapaswa kuchukua hatua za hali hiyo ambayo Serikali ya nchi hiyo imeiita janga la kitaifa

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close