1. Habari3. Kimatiafa

Wanafunzi Uingereza waliogomea somo la ushoga, usagaji, wasimamishwa shule

LONDON
Wanafunzi wawili Kaysey na Farrell wa shule ya msingi ya Heavers Farmer jijini London nchini Uingereza walijikuta wakisimamishwa shule baada ya kukataa kushiriki kwenye somo liitwalo ‘Pride Month’ ambalo linaendana na sherehe za kukumbuka ghasia zijulikanazo Stone-
wall za mwaka 1969 zinazowahusu watu wa mapenzi ya jinsia moja.

walijikuta wakisimamishwa shule baada ya kumuomba ruhusa mwalimu wao kutoshiriki somo hilo

Farrell na mwanafunzi mwenzake Kayesy ambae ni binti wa miaka 10 walijikuta wakisimamishwa shule baada ya kumuomba ruhusa mwalimu wao kutoshiriki somo hilo. Ruhusa hiyo ilichukuliwa kuwa ni ubaguzi dhidi ya mashoga na wasagaji na badala yake mwalimu wao alisisitiza kuwa somo hilo ni sehemu ya mtaala wa shule.

Mkuu wa shule hiyo Susan Papas, aliwasimamisha wanafunzi hao kutohudhuria shuleni kwa muda wa siku tano kwa madai kuwa mwanafunzi Farrell alitoa matamshi ya kibaguzi kwamba mashoga na wasagaji ni wanyonya damu na wasiojielewa. Kwa upande wake, Farrell
alikana madai yote hayo na kusisitiza kuwa imani yake ya Kikristo inapingana na vitendo vya ushoga na usagaji.

Kwa upande mwingine, Mwalimu Papas alidai kuwa wanafunzi hao wametishia kuwaua mashoga na wasagaji, madai ambayo yalikanushwa na wanafunzi hao.
“Mnadhubutu vipi kusema mnataka kuwaua mashoga na wasagaji?” Mwalimu Papas aliwauliza vijana hao mbele ya darasa.

Kaysey alijibu: “Sijasema wauawe.” Lakini Mwalimu Papas alisisitiza kuwa Kaysey alisema maneno hayo: “Ni kweli umesema
na wala usidanganye.” Binti Kaysey alisema, watu wanaofanya vitendo hivyo vya ushoga na usagaji wanawaathiri wanafunzi wengine na kwamba watu hao wamepoteza hali ya kujiamini katika matendo yao.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close