1. Habari3. Kimatiafa

Ushauri: Shambulio la kigaidi msikitini

Imetafsiriwa na Mariam Mzingi

Niliamka asubuhi na huzuni baada ya kusikia habari za kusikitisha juu ya tukio lililowakumba ndugu zetu katika imani, vijana na wazee katika misikiti miwili huko Christchurch New Zealand. Walikuwa viumbe wenye amani wakitegemea Ijumaa hii iwe kama Ijumaa nyingine.

Waliianza siku yao wakitegemea kufanya kazi zao, kwenda shule, kuwahudumia watoto wao, kulipa bili zao, kula chakula chao wanachokipenda, kuswali swala zao, kusoma suratul Kahf na kufanya shughuli za Ijumaa.

Mara! Subhanallah! bila taarifa, muda ambao hawakuwa wakitegemea hata kidogo kwamba kitu kama hicho kingeweza kufanyika, kila kitu kilifikia tamati kwenye mikono ya magaidi na wale wanaowadhamini. Ili kutudhalilisha zaidi, mmoja wao alirekodi tukio zima bila aibu.

Hakika Allah anatutosha.

Wengi wakikumbwa na hali kama hii wanasema:” Simamisha dunia, nataka kushuka”

Naapa kwamba nilishangazwa sana na habari hii ya kusikitisha, na sikuweza kuyazuia mataminio yangu ya kutaka tukio hili liwe ndoto mbaya tu ili niweze kuamka na kumuomba Allah atuepushie (kutokea kwake).

Katika kipindi hiki kigumu, niruhusu kutoa muongozo huu muhimu

MOSI

Kila nafsi itaufikia umauti katika wakati wake ulopangwa kwa idhni ya Allah, sio sekunde kabla, wala baada ya muda huo. Ndugu zetu katika imani wamerudi kwa muumba wao katika muda muafaka waliokuwa wamepangiwa.

Allah (swt) anasema katika Surah Al- Imran:
وَما كانَ لِنَفسٍ أَن تَموتَ إِلّا بِإِذنِ اللَّهِ كِتابًا مُؤَجَّلًا ۗ وَمَن يُرِد ثَوابَ الدُّنيا نُؤتِهِ مِنها وَمَن يُرِد ثَوابَ الآخِرَةِ نُؤتِهِ مِنها ۚ وَسَنَجزِي الشّاكِرينَ

Na haiwezi nafsi kuwa ife ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyo andikwa ajali yake. Na mwenye kutaka malipo ya duniani tutampa; na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa. Na tutawalipa wenye kushukuru. (Qur’an 3:145)

Hivyo basi, tukumbuke kwamba siku zote tunatakiwa tuwe tayari kukutana na Mola wetu na tuswali kila swala kama vile ndio swala yetu ya mwisho.

PILI

Wanazuoni wa dini ya Kiislamu wamesema kuwa yeyote atakayefariki kwa tukio la kudhulumiwa na watu wengine basi atapata ngazi ya ushahidi. Kiuhalisia ni kwamba tukio hili linatuonyesha kwamba watu hawa walikuwa vipenzi wa Allah, na walikuwa karibu nae wakati walipokuwa wakiishi miongoni mwetu! Hatukujua tu hili hadi sasa. Subhanallah!

TATU

Mara nyingine Allah (SWT) anataka kumpa mja wake mahala katika pepo ambayo yeye mwenyewe (mja huyo) hawezi kuifikia kwa juhudi zake, hivyo mja huyu hupewa mitihani, na kwa kupitia subra yake, mja huyu huipata ngazi ya juu zaidi peponi. Tunamuomba Allah awape daraja ya juu mashahidi katika tukio hili, familia zao, na sisi wote tulioguswa na tukio hili. Amin.

NNE

Binadamu wamepewa uwezo wa kiakili na ni viumbe wenye uwezo wa kufanya maamuzi. Matukio haya yanafanya kwa maamuzi na wanaoyatenda watapata adhabu kutoka kwa Allah (SWT) duniani na ahera. Usiwe na shaka, machungu watakayoyapata yatazidi machungu ambayo wanahisi wameyasababisha.

TANO

Kwa familia ambazo zimekumbwa na msiba huu, naapa kwamba kifo sio mwisho, bali ni mwanzo. Waliofariki wako hai wakipata riziki kutoka kwa Mola wao, hivyo basi ni juu yetu sisi tushikimana na imani yetu, na kuifuata sunnah. Hii ni kwa ajili ya kutusaidia kurudi kwa mola wetu hali ya kuwa ameridhika na sisi, pale muda wetu utakapowadia, ilituweze kukutana na vipenzi wetu wakiotangulia, katika daraja la juu kabisa peponi.

Sina shaka, kwamba makutano hayo yakifanyika katika maisha ya akhera ya milele, huku mkizungukwa na uzuri na zawadi zisizokifani; kila mtu atasema :”Hakika kila akifanyacho Allah, anakifanya kwa wema!”

SITA

Kwa wale waliobaki katika mtihani huu wa maisha, dua ndio silaha ya waumini. Ni lazima tuombe na tuwasilishe mawazo ya mioyo yetu kwa Allah, huku tukimuomba msaada.

Omba, mashahidi wetu wapate daraja ya juu kabisa peponi. Omba kupata ulinzi wa imani yako na uwezo wa kuwa na subra. Omba majeruhi wapate shifaa ya haraka. Omba madaktari wanaowahudumia waendelee kuhamasika katika jitihada zao. Omba vyombo vya ulinzi viweze kuwadhibiti wahalifu waliotenda tukio hili. Pia tukumbuke kuwaombea ndugu zetu wote katika imani wanaoishi katika mateso kama haya duniani kote.

Tunamuomba Allah ashushe rehema zake juu ya waliofariki, azifanyie wepesi familia zao, asaidie haki itendeke juu ya wahalifu na atuunganishe wote katika pepo yake kwa uvumilivu tutakaouonyesha katika kipindi hiki. Amin.

Imetafsiriwa kutoka: Islamic21c. Ili kusoma kwa Kingereza bonyeza hapa

Tags
Show More

Shaykh Sajid Omar

Sheikh Sajid Ahmed Umar awali alipata shahada katika IT, akihitimu na matokeo ya daraja la kwanza. Aliendelea kwa kufungua biashara ya IT yenye mafanikio makubwa. Pamoja na masomo yake ya kisasa, Sheikh Sajid alimaliza kuhifadhi Qur'an akiwa na umri wa miaka 18. Kwa hiyo, alibadilisha dira yake kuelekea kwenye masomo ya dini. Alimaliza kozi ya miaka 3 katika lugha ya Kiarabu na Sayansi ya Kiislam katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Imaam Muhammed bin Saud , ambapo baadae alipata shahada katika Shariah kisha shahada ya uzamili katika Mahakama (Qadha), kwa kupata daraja la kwanza , kutoka Taasisi ya Juu ya Mafunzo ya Mahakama (Ma'had al-'āli li'l-Qa'dhā). Alifanya kazi kama hakimu na kukamilisha thesis yake juu ya mada ya 'Liquidity Management using the famous Repurchase Agreement' (REPO), pamoja na maamuzi yake na njia mbadala zilizoruhusiwa. Sasa anachukua PhD yake katika Taasisi ya Juu ya Mahakama katika Chuo Kikuu cha Al-Imam. Sheikh Sajid amekuwa na sehemu muhimu katika maendeleo ya kitaaluma ya kiislamu duniani kote akiwa ameandika makala kadhaa katika lugha zote mbili za Kiarabu na Kiingereza zinazohusiana na Sayansi za Kiislam; mihadhara katika Chuo Kikuu cha kimataifa cha elimu(Knowledge International University); ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kiislam katika Mercy Mission World; mihadhara katika Taasisi ya AlKauthar na Mhariri Mkuu wa Kiislamu wa gazeti, hivi vikiwa vichache kati ya jitihada zake nyingi za kupendeza.

Related Articles

Back to top button
Close