1. Habari3. Kimatiafa

Trump Awazulia Wakimbizi Waislamu

NA MWANDISHI WETU

Wahenga walisema, “Ukitaka kumuua mbwa, mpe jina baya kisha ndiyo umuue”. Wala hakutakuwa na wakukulaumu. Inaonekana hilo ndilo analofanya Rais wa Marekani Donald Trump ambaye hivi karibuni amejikuta akiingia matatani kwa kuwazushia wakimbizi wa Kiislamu walioko nchini Sweden kuwa wamekuwa wakifanya vitendo vya ugaidi nchini humo. Akijenga hoja ya kuhalalisha kuwazuia wakimbizi wanaokimbilia nchini Marekani kupata hifadhi, Rais Trump alitolea mfano wa nchi ya Sweden kuonesha athari za kupokea wakimbizi. Hata hivyo, kumbukumbu zote zinaonesha hakujawahi kuwepo tukio lolote la ugaidi nchini Sweden kama Rais Trump alivyodai katika matamshi yake na kwamba maneno yake ni uongo mtupu. Trump alidai: “Lazima tulinde usalama wa nchi yetu, angalia yanayojiri nchini Ujerumani, angalia kilichotokea jana usiku nchini Sweden. Sweden, nani anaweza kuamini hili? Sweden. Sweden ilichukua wakimbizi wengi sana. Wana matatizo kibao ambayo hawakuwahi kuwa nayo huko nyuma. Angalia kinachotokea huko Brussels. Angalia kinachotokea dunia nzima. Tazama vizuri. Tazama Paris.” Matamshi hayo yalizua maswali mengi kuhusiana na wapi Rais Trump alizipata taarifa hizo za uwepo wa uhalifu nchini Sweden katika siku hiyo ya Ijumaa aliyoitaja. Waliokasirika siyo Waislamu tu bali hata raia wa Sweden ambao wanaona nchi yao inachafuliwa. Baada ya watu wengi kuhoji matamshi hayo ya Trump, ilimbidi Rais Trump kufafanua kwenye akaunti yake ya ‘Twitter’ ambako aliandika akisema kuwa matamshi yake yalitokana na taarifa aliyoiona kwenye runinga. “Maelezo yangu juu yakinachotokea nchini Sweden inatokana na stori iliyotangazwa kwenye kituo cha runinga cha Fox News kuhusiana na wahamiaji walioko Sweden,” aliandika Rais Trump. Hata hivyo baadae ilikuja kubainika kuwa Rais Trump aliyapata maelezo hayo kupitia kipindi cha runinga hiyo ya Fox News cha Tucker Carson ambapo mtangazaji huyo alimuuliza mtengenezaji filamu Ami Horowitz aliyehusianisha uwepo wa watafuta hifadhi wengi nchini Sweden na uongezekaji wa vitendo vya kihalifu. Muda mfupi baadaye, ubalozi huo wa Sweden ulisema kuwa hata wao hawaelewi alichokuwa anakizungumzia Rais huyo wa Marekani na kuwa wamewauliza viongozi wa Marekani kwa ufafanuzi zaidi. Naye Waziri Mkuu wa zamani wa Sweden, Carl Bildt, aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuhoji ni tukio gani la kigaidi lililokuwa limetokea nchini Sweden na sigara gani alikuwa amevuta Rais Trump. Katika kutetea matamshi ya Rais Trump, Msemaji wa Ikulu ya Washington, Sara Sander aliwaambia waandishi wa habari, kuwa Rais Trump alikuwa anazungumzia ongezeko la uhalifu na matukio ya hivi karibuni na hakuzungumzia tukio maalumu na hakuamanisha ‘usiku wa jana’ bali alikuwa akizungumzia ongezeko la uhalifu nchini Sweden. Pamoja na utetezi huo, ukweli unabaki kuwa alichokuwa akikifanya Trump ni kuwapaka matope Waislamu ili ahalalishe sera zake za chuki, ubaguzi dhidi ya dini tukufu

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close