1. Habari3. Kimatiafa

Tatizo siyo Trump, ni Marekani

N i jambo linalogusa moyo sana kuona baadhi ya wananchi wa Marekani wakisimama pamoja na Waislamu kumpinga Donald Trump na sera zake za kibaguzi. Kuna matumaini kwamba maandamano makubwa ya raia wa Marekani kumpinga Rais Trump yanaweza kuleta tija. Hata hivyo, Waislamu ulimwenguni kote hawapaswi kudanganywa na mauzauza yanayoficha mwelekeo halisi ambao jamii ya Kimarekani imeamua kuuchukua na itaendeela kuuchukua. Ukweli halisi ni kwamba Donald Trump ana mamlaka (mandate) kutoka kwa wananchi wa Marekani na pia anaungwa mkono na sehemu kubwa ya jamii ya Marekani kwa sera zake za kibaguzi dhidi ya Waislamu. Donald Trump alikuwa muwazi sana na mkweli kuhusu kile atakachofanya iwapo angefanikiwa kukamata uongozi wa Marekani, na bado mamilioni ya Wamarekani walimuunga mkono na kumpigia kura. Ndugu zangu katika imani, swali la msingi tunalopaswa kuangazia hapa, siyo kuhusu Donald Trump na sera zake angamizi, bali kwa nini wananchi wa Marekani walimuunga mkono na vipi wamefikia hatua hiyo. Mtu anaongea mambo ya hatari kwenye kampeni za uchaguzi, lakini bado anaungwa mkono! Sasa anaanza kutekeleza kwa uadilifu kile alichowaahidi Wamarekani kwenye majukwaa ya kampeni kuhusu WaisIamu na wahamiaji wengine nchini humo, Wamarekani hao hao wanaandamana mitaani kwa maelfu kumpinga. Wanajifanya wako pamoja na Waislamu, wakati wao ndiyo waliomuingiza Trump Ikulu. Miye Marekani naifahamu kidogo. Sehemu kubwa ya jamii ya Kimarekani imekuwa na chuki dhidi ya wageni, ina msimamo mkali, na imejazwa hofu na chuki dhidi ya Waislamu. Jamii nyingine za wachache nchini humo pia zinaishi kwa mashaka. Wamarekani ‘wametengenezwa’ kisaikolojia kuwachukia Waislamu na wamemchagua mhubiri mkubwa wa ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni kuwa rais wao. Hakuna anayemwita Trump ‘extremist’ (mwenye msimamo mkali) nchini Marekani, kwa sababu yeye ni mweupe na mkristo, na kwamba hizi lebo zimebuniwa maalumu kwa ajili ya Waislamu. Bado Donald Trump anaitwa ni kiongozi wa ‘free world’ (ulimwengu huru) na anapewa heshima. Fikiria kama jina lake lingekuwa Muammar Gadaffi au Robert Mugabe, ambao wameweka maslahi ya nchi zao na watu wao mbele, vipi Donald Trump angerejewa, au namna gani angeshughulikiwa? Waislamu nchini Marekani na Uingereza, ambao wanatoa maoni yao yasiyo na madhara yoyote wanapachikwa lebo ya ‘extremists’ hatari na kupigwa marufuku. Pamoja na nia yao njema, Wamarekani wengi na Waislamu wanaoandamana mitaani kumpinga Donald Trump ni makundi ya jamii za watu waliotezwa nguvu nchini humo. Kwa upande mwingine, makundi ya mrengo wa kulia, wabaguzi wa rangi na wanaharakati wa Kikristo wenye msimamo mkali, yanapewa fedha za kutosha na kuwezeshwa nchini Marekani. Makundi haya yana taasisi zenye ushawishi mkubwa na yanatumia vyombo vya habari kusukuma ajenda zao. Kwa takriban miongo minne iliyopita, harakati hizi zimefanya juhudi kubwa za kuhubiri ujumbe wa chuki na kutovumiliana, na wale wanaow – a w e z e s h a w a m e j e n g a ngome madhubuti za kuwaunga mkon o n c h i n i Uingereza na Ulaya. Matokeo yake ni kwamba, kila rais wa Marekani anapoingia madarakani, sera za chuki dhidi ya Waislamu zinazidi kuwa mbaya. Ingawa marais wengine wa Marekani wamekuwa wakiwalenga Waislamu kwa sera zao, Donald Trump na kauli zake tata za kuwanyanyapaa Waislamu, ikiwa ni pamoja na kuwapiga marufuku kuingia nchini humo; amekwenda mbali zaidi. Trump ameisaidia jamii ya Kimarekani kuvuka kikwazo cha kisaikolojia. Ametengeneza mazingira ambayo sasa inakubalika wazi kuwasema vibaya Waislamu na kuishambulia imani yao. Hata kama mahakama nchini humo itaamua kwamba maagizo ya kitendaji ya Trump yako kinyume na katiba, lakini vinasaba vya chuki ya kupinga Uislamu vimeshasambazwa sana na tayari tunaona matokeo yake. Moto wa chuki unapowashwa ni vigumu sana kuu z i m a .Tr u m p ameanzisha jambo ambalo haliwezi kuondolewa k w a u r a h i s i . M a r e k a n i haitakuwa tena, kama ilivyokuwa awali, kwa Waislamu nchini humo, au mahali pengine. Tusikubali kudanganyika na kudh a n i k w a m b a ukimuondoa Donald Trump, basi hatari na mashaka yanayowakabili sasa Waislamu nayo yatakuwa yameondoka. Marekani imehusika kwa kiasi kikubwa na sera za mauaji

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close