1. Habari3. Kimatiafa

Rais Erdogan Amshutumu Merkel kufuga Magaidi

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameendeleza mashambulizi yake dhidi ya viongozi wa Ulaya kwa kumshutumu Kansela wa Ujermani, Angela Merkel kwa kuunga mkono magaidi, ingawa Merkel amepuuza shutuma. Msemaji wa Merkel Steffen Seibert amesema: “Kansela Merkel hana nia ya kuwa sehemu ya mchezo wa kuchokonoana.” Matamshi ya Erdogan ya kumshutumu Merkel yametolewa kupitia runinga ya ‘A Haber’ ya Uturuki mara baada ya viongozi wa Ujerumani na nchi kadhaa za Ulaya kuzuia kufanyika kwa maandamano ya kuunga mkono kura ya maoni inayolenga kumuongezea nguvu ya kikatiba Rais Erdogan. “Bi Merkel, kwanini unahifadhi magaidi katika nchi yako? Kwanini huchukui hatua. Madamu Merkel unaunga mkono magaidi,” alisema Rais Erdogan.

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close