1. Habari3. Kimatiafa

Mfalme Salman: Jitihada za kimataifa Zitamaliza Migogoro Mashariki ya Kati

Mfalme wa Saudi Arabia Salman amesema kuwa zinahitajika jitihada za kimataifa ili kuitanzua migogoro ya Mashariki ya Kati ikiwemo ya Palestina, Syria na Yemen, linaripoti Shirika la Habari la Saudi Arabia (SPA). Mfalme Salman alizungumza hayo wakati alipokutana na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, mjini Tokyo ambapo walijadili mambo ya amani. Mfalme Salman alisema ugaidi umekuwa janga kubwa kwa usalama wa nchi na watu. “Sisi sote tunahitajika kupambana na migogoro hiyo, na tunahitaji juhudi na nguvu za pamoja kuimarisha dhana ya mazungumzo baina ya wafausi wa dini na tamaduni mbalimbali na pia kuzidisha ari ya kuvumiliana na kuishi pamoja,” alisema Mfalme Salman. Migogoro ya Mashariki ya Kati imeathiri vibaya uimara na maendeleo ya eneo hilo kwa kuzuia ukuaji wa biashara ya kimataifa na kutishia ugavi wa nishati, aliongeza Mfalme Salman. Katika mazugumzo yao walijikita pia katika kuimarisha mahusiano ya kimkakati na kiuchumi. Nchi hizo pia zilikubiliana mpango wa dira ya mwaka 2030 wa kuimarisha ushirikiano baina yao. Licha ya Japan, Mfalme huyo katika ziara yake hiyo atatembelea mataifa sita ya Asia.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close