1. Habari3. Kimatiafa

Madaktari wa Israel Washutumiwa Kutesa Wafungwa Wakipalestina

RAMALLAH, Kamati ya Kipalestina imewashutumu madaktari wa Israel kwa kuwatesa wafungwa wa Kipalestina walioko kwenye jela za Israel. Kamati hiyo ya chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO) imedai kuwa madaktari wa Israel wanaofanya kazi gerezani pamoja na maafisa usalama wamekuwa wakiwatesa wafungwa na kuwasababishia matatizo ya kisaikolojia.

“Madaktari kwa makusudi wamekuwa wakizipuuza afya za wafungwa, na hawazingatii madili ya kazi zao na mikataba ya kiutu pamoja na haki za binadamu,” ilisema kamati hiyo. Kwa upande wake Israel haijazungumzia lolote kuhusu madai ya kamati hiyo. Serikali ya Palestina, inasema kuwa Wapalestina 7,000 wako katika magereza ya Israel.

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close