3. Kimatiafa

Corona yazidi kuiuliza Afrika maswali magumu

Tanzania tulichelewa kukaribisha wazo la chanjo kwa sababu za kisiasa, lakini baada ya mabadiliko ya uongozi yaliyotokana na kifo cha aliyekuwa Rais, John Magufuli, inaonekana utawala mpya sasa umeelewa kuwa hakuna namna Tanzania inaweza kujitenga na ulimwengu!

Umuhimu wa tangu ugonjwa wa Corona au COVID-19 ulipotangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa janga la kidunia Januari 30, 2020, chanjo sita zimeidhinishwa kuwa kinga.

Kwa mujibu wa tovuti ya Umoja wa Mataifa, chanjo hizo ni Pfizer/ BioNTech, AstraZeneca/Oxford, Moderna, Johnson & Johnson, Sinovac na Sinopharm. Chanjo hizo ni miongoni mwa chanjo zaidi ya 200 ambazo ziko kwenye utafiti ili kukabili Corona.

upatikana kwa chanjo kwa Watanzania unaonekana zaidi sasa ambapo WHO imeonya kuhusu uwezekano wa kuibuka kwa ]wimbi la tatu la Corona barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, ipo hatari kubwa kwa Watanzania kukosa fursa za kusafiri na kujichanganya ulimwenguni kwa sababu mbalimbali ikiwemo biashara, siasa, elimu au hata imani. 

Ni katika muktadha huo ndipo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiadhimisha siku 100 za utawala wake, alilitangazia taifa kuwa tayari taratibu zinafanyika ili kuingiza chanjo ya COVID-19. Pia, alisema katika wimbi la tatu la Corona, tayari kuna wagonjwa zaidi ya 100.

Rais Samia alisema: “Nataka niwe mkweli. Tanzania tuna wagonjwa katika hili wimbi la tatu. Mpaka taarifa nilizozipata juzi, nadhani kuna wagonjwa kama mia moja na kati yao si chini ya wagonjwa 70 wako kwenye matibabu ya gesi na wengine wako kwenye matibabu ya kawaida. Sasa ukiangalia si wengi lakini hatuna budi kujikinga wasiongezeke.”

Rais Samia pia alisema kuwa licha y a uamuzi huo wa kuchanja, bado chanjo hiyo itakuwa hiari. Rais Samia alisema:

“Kwa hiyo hatua tuliyochukua kwanza tuliamua kwamba twende na ulimwenguni unavyokwenda, tuchanje na tuchanje kwa hiari. Mtanzania anayetaka atachanja na asiyetaka ataangalia kwa nafsi yake.”

Kwa hiyo tukaharakisha watanzania tukasema na sisi tumo, mengine ya kuagiza na chanjo ipi yatafuata – Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania

Rais Samia alisema uamuzi wao umezingatia kwamba Watanzania wengi ambao ni wafanyabiashara wamepata tayari chanjo hizo nje ya nchi, iwe ni Dubai Falme za Kiarabu au Afrika Kusini. Alisema watanzania hao tayari wako nchini na wanaendelea na shughuli zao.

Afrika yapata uungaji mkono

Habari njema ni kuwa Tanzania imejiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuchagiza upatikanaji wa chanjo. Mpango huo uitwao kwa kifupi C O V A X , umelenga kusaidia nchi za kipato cha chini.

K w a bahati nzuri Tanzania iliwahi kabla ya tarehe 15 iliyokuwa tarehe ya mwisho ya kuthibitisha kukubali kuingizwa kwenye mpango huo ili tupate chanjo mwaka ujao wa 2022. 

Miongoni mwa nchi za Afrika zilifaidika na mpango wa COVAX ni pamoja na Rwanda, Uganda, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Matumaini yanaongezeka zaidi sio tu kwa Tanzania bali Afrika nzima baada ya Benki ya Dunia (WB) nayo kutangaza kuunga mkono mpango wa Muungano wa Afrika (AU) kuhakikisha asilimia 60 ya wakazi wa bara lake wamepatiwa chanjo ya Corona ifikapo mwaka 2022.

Ubia huo wa Benki ya Dunia na AU ni sehemu ya juhudi za kuunga mkono mpango wa AVATT, kikosi kazi cha Afrika cha kununua na kusambaza dozi za chanjo kwa ajli ya watu milioni 400 barani kote.

Makubaliano hayo yalikuja baada ya mkutano kati ya Benki ya Dunia na Mawaziri wa Fedha wa Afrika na hatua hiyo inaenda kuunga mkono ile ya kimataifa ya COVAX wakati huu ambapo kuna ongezeko la wagonjwa wa Corona barani Afrika. 

Mkurugenzi wa Operesheni katika Benki ya Dunia Axel Trotsenburg alisema lengo la mpango huo ni kuzuia mlipuko wa tatu wa Corona na kwmaba kwa sababu chanjo hizo zinahitaij ufadhili ndio maana WB inaingia kwa kutoa fedha zote. 

Benki ya Dunia ina dola bilioni 12 za kusaidia nchi kununua na kusambaza chanjo, ambapo mpaka sasa mataifa 36 yamefaidika huku lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Juni iwe imesaidia nchi 50 duniani huku theluthi mbili zikiwa Afrika. 

Chanjo gani?

Katika hotuba yake ya maadhimisho ya siku 100 za utawala wake, Rais Samia alisema, baada ya kuweka mipango sawa ya kupata fedha za chanjo, wataalamu sasa wanatafiti chanjo ipi ipekwe Tanzania na kwa vipi.

Labda hili ndio swala gumu zaidi hasa kwa sababu kuna tetesi nyingi zimekuwa zikienea kuhusu athari za chanjo hizi. Yapo madai kuwa kuna watu walikufa au walizimia baada ya kuchanjwa. Yapo pia madai ya chanjo hizi kuua nguvu za kiume au hata kuzuia mtu kupata kizazi.

Ukiacha hayo, kwa mujibu wa WHO, ubaridi unaotakikana kuhifadhi chanjo pia unatofautiana. Zipo zinazohitaji ubaridi mkali sana ili zibaki kwenye ubora wake na kwamba zikipoa tu ufanisi unafifia. Zipo ambazo zinahitaji ubaridi wa hadi -90°C!

WHO ishatoa wito kwa nchi ziwe na mkakati wa kitaifa wa sio tu utoaji wa chanjo nbali pia uimarishaji wa mnyororo wa kupokea, kuhifadhi, kuzisambaza na kuzisimamia ikiwa ni pamoja na usimamizi wa vifaa vinavyotakiwa kama mabomba ya sindano, majokofu na makasha ya kutupia sindano zilizotumika. 

WHO imetoa wito usambazaji huo ufikie hadi maeneo ya ndani kabisa ya nchi ili kila mtu anayehitaji kupata chanjo apatiwe.

Katika siku za hivi karibuni, maambukizi ya corona yanatajwa kuwa yameongezeka kwa asilimia 20. Afrika ikiwa ina asilimia 2.9 ya wagonjwa duniani kote huku idadi ya vifo ni asilimia 3.7 pekee. Mpaka sasa, ni asilimia mbili tu ya wakazi wa Afrika wamepata angalau dozi moja ya chanjo ikilinganishwa na asilimie 24 duniani kote. Hadi tarehe 3 Juni 2021, duniani kote kumekuwepo na wagonjwa 171,222,477 wa COVID-19, ambapo kati yao hao 3,686,142

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close