1. Habari3. Kimatiafa

Ahed Tamimi (17), awa alama mpya ya ukombozi palestina

Ahed Tamimi kwa sasa ni jina kubwa ulimwenguni likiwa ni alama ya upinzani na ukombozi wa ardhi ya Wapalestina inayokaliwa kimabavu na taifa la kizayuni la Israel kwa miaka 70 sasa.

Tamimi ni binti wa miaka 17 wa Kipalestina ambaye Desemba mwaka jana mkanda wake wa video ulisambaa duniani ukionesha akiwapiga makofi na mateke wanajeshi wawili wa Kiyahudi kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi.

Ahedi alikuwa akipinga uvamizi wa Israel katika ardhi yao ya Palestina, na pia akipinga kadhia nyingine zinazowaandamana Wapalestina kutokana na uvamizi huo.

Binti huyo aliamua kuwavaa wanajeshi hao wa Kiyahudi akiwazuia kuingia nyumbani kwao ili kuwakinga watoto.

Hata hivyo kitendo chake hicho kilimfanya ashitakiwe yeye pamoja na mama yake mzazi na utawala wa Israel kwa makosa makosa 12 ya kushambulia na kuwazuia wanajeshi hao wa Kiyahudi
kutekeleza majukumu yao.

Mama yake Ahedi Tamimi, aitwaye Nariman Tamimi, alishitakiwa kwa kosa la kurikodi mkanda huo wakati mwanae akiwapiga makofi wanajeshi hao Waisrael.

Binti huyo ambaye wakati anawavaa wanajeshi hao alikuwa na miaka 16, na mama yake, walihuku-
miwa kwenda jela kwa miezi nane.

Lakini Jumamosi ya Julai 29, binti huyo aliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo chake hicho cha
miezi minane huku mama yake akitumikia wiki tatu baada ya kupunguziwa muda wa kifungo mapema mwaka huu

Kuachiwa huru kwa binti huyo kulipokelewa kwa furaha na Wapalestina na watu mbalimbali duniani wanaopinga uonevu wa Israel kwa Wapalestina.

Akiongea baada ya kuachiwa huru, Tamimi alisema kuwa furaha yake haijakamilika kwa kuwa bado ndugu zake wengine wa Kipalestina wako katika magereza ya Waisrael.

“Furaha yangu haijakamilika bila dada zangu (wafungwa wa kike)
ambao hawako nami leo. Natumai ipo siku nao watakuwa huru,” alisema Tamimi.

Pia, binti huyo alisema kwamba ataendelea kupigania maslahi ya Wapalestina huku akiwatolea wito Wapalestina wenzake kusimama pamoja dhidi ya uonevu Waisrael.

Ahedi Tamimi ambaye alipokelewa kwa kishindo na Wapalestina mara baada ya kutoka jela, kwa sasa anachukuliwa kuwa miongoni mwa mashujaa na watetezi wakubwa wa taifa la Palestina.

Na mara baada ya kutoka jela, Tamimi alikutana na Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, ambapo Rais huyo alimpongeza kwa ujasiri wake.

Baadhi ya vyombo vya habari vinamtaja binti huyo kama mtu ambaye ataingia kwenye rikodi za akina Yaser Arafat aliyetumia sehemu kubwa ya uhai wake kupigania taifa la Palestina.

Maisha yake ya awali
Binti huyo alianza kugonga vichwa vya habari duniani miaka miwili
iliyopita baada ya kuonekana kwenye picha akimpiga mwanajeshi wa Kiyahudi ambaye alikuwa anamkamata mdogo wake wa kiume.

Mwaka 2012, alitunukiwa zawadi nchini Uturuki na pia kupewa fursa ya kukutana na rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya video kumuonesha akimpiga askari wa Israel kusambaa.

Kwa miaka 70 sasa tangu kuundwa kwa taifa la Israel hapo mwaka 1948, Wapalestina wamekuwa wakipitia mateso na mauaji mbalimbali yanayofanywa na taifa hilo la Kizayuni.

Pia Israel imeendelea kukiuka sheria za kimataifa ikiwemo kuvamia mipaka ya Palestina kama ilivyoainishwa na Umoja wa Mataifa wakati wa kuigawa Palestina hapo mwaka 1947 na kujenga
makazi yao.

Mgogoro mkubwa unaoendelea sasa ni kutambuliwa na kutangazwa kwa mji wa Jerusalem kuwa mji wa Israel hatua ambayo imeendelea kusababisha vurugu kubwa katika eneo hilo la Mashariki ya Kati

 

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close