1. Habari2. Taifa

Hijja ilivyowajumuisha wasomi, wanasiasa

Mahujaji waisifu programu ya Hijja ya M falme

Mahujaji 10 wa Tanzania waliopata fursa ya kwenda Hijja mwaka huu kupitia ufadhili wa Programu ya Msimamizi wa Misikiti Miwili Mitukufu, Mfalme Salman bin Abdulaziz Al–Saud kwa ajili ya ibada ya Hijja, Umrah na ziara, wamesema kuwa Programu hiyo ina manufaa makubwa kwa Waislamu duniani.

Wakizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita katika mahojiano maalumu na gazeti Imaan jijini Jeddah, nchini Saudi Arabia, wakiwa katika harakati za kurejea nyumbani baada ya kukamilisha ibada tukufu ya Hijja, Mahujaji hao wamefurahia programu hiyo wakisema kuwa imewawezesha kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya Kiislamu (Hijja) na kuwakutanisha na ndugu zao Waislamu kutoka maeneo tofauti duniani.

Mmoja wa Mahujaji hao, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo amesema Pro– gramu hiyo imewakutanisha Waislamu wa kada mbalimbali kutoka mae– neo na hadhi tofauti, bila ya ubaguzi wowote.

“Si rahisi kwa mtu kama mimi kukaa pamoja na Profesa kutoka Marekani. Au kulala na Profesa Lipumba kitanda kwa kitanda. Tumenyoana mpaka nywele na Profesa Lipumba baada ya kutoka Jamaraat. Kwa hiyo, programu hii imetuunganisha na kutukumbusha ya kwamba sisi ni Waislamu kwanza, hadhi zetu na itikadi za kisiasa si chochote. Bila ya programu hii, watu hawa pengine wangekaa na ‘V.I.P’ wenzao,” alisema Chaurembo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alisifu jinsi wafanyakazi wa programu hiyo walivyoji– panga kuwahudumia wageni wao kwa bashasha, upendo na tabasamu.

Profesa Lipumba alisema: “Kwa kweli tumehudumiwa vizuri sana. Tangu tulipowasili Makka mambo yetu yalikuwa mazuri. Tumepata huduma ya kiwango cha juu mno kuanzia chakula, malazi, usafiri na huduma nyinginezo. Mwenyezi Mungu awalipe kwa hisani yao, Mfalme Salman wa Saudi Arabia na wafanyakazi wote wa programu yake. Si rahisi kuhudumia zaidi ya watu 2,000 kwa ufanisi na ubora wa kiwango kile bila ya changamoto kubwa.”

Naye, Fatma Taufiki, mbunge wa viti maalum mkoa wa Dodoma ameisifu programu hiyo kwa kuwaun– ganisha Waislamu. “Hii programu imenikutanisha na mtani wangu wa kisiasa, Profesa Lipumba na imetukumbusha kwamba sisi wote ni Waislamu, itikadi yetu ni moja na mambo ya kisiasa yasitugawe.”

Naye, Afisa Fatawa na Utafiti kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, kanda ya Pemba, Sheikh Said Mohammed amezitaka taasisi zinazosafirisha Mahujaji hapa nchini kutoa huduma bora kwa Mahujaji wao.

“Kama unavyojua Hijja ni utulivu. Sisi tumepata ladha ya Hijja kwa sababu tulikuwa na utulivu kutokana na huduma tulizopata. Kwa hiyo nazitaka taasisi zinazosafirisha Mahujaji nchini kuwapa huduma bora Mahujaji wao na kuwawekea mazingira mazuri ya kutekeleza ibada hii tukufu,” alisema Sheikh Mohammed.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi amesema huduma bora alizopatiwa zimemfanya atekeleze ibada ya Hijja kwa wepesi.

“Kubwa ni kushukuru, kwa sababu kutokana na huduma bora tuli– zowekewa na wenyeji wetu, ibada yetu imekuwa nyepesi.Tumesali vipindi vyote vitano kwa jamaa na ndani ya wakati wake. Kwa kweli nashukuru sana,” aliongeza Profesa Janabi.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close