1. Habari2. Taifa

Azhar Sharif yataka vita ya kimkakati dhidi ya dawa za kulevya

Mwalimu wa Kituo cha Kiislamu cha Kimisri (Azhar Sharif) Tawi la Tanzania, Sheikh Ashraf Ibrahim Al–Shawadify amesema inahitajika vita ya kimkakati dhidi ya dawa za kulevya duniani.

Sheikh Al–Shawadify aliyasema hayo hivi karibuni katika kongamano la maimamu na wahubiri wa dini ya Kiislamu, lililoandaliwa na Azhar Sharif, Tawi la Tanzania na kufanyika kwenye ukumbi wa Iddy Nyundo, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Sheikh Al–Shawadify alisema dawa za kulevya ni janga la dunia na ndio maana mataifa mengi ulimwenguni yameweka sheria kali zinazozuia au kupambana na watu wanaojihusisha na dawa hizo kutokana na ukubwa wa madhara yake kwa jamii husika.

Sheikh Al–Shawadify aliwaasa kwa maimamu na walinganiaji kuitahadharisha jamii juu ya hatari ya dawa za kulevya kwani wao wana nafasi kubwa katika kuwashawishi Waumini wao kujiepusha na vitendo hivyo viovu.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum aliwakumbusha washiriki wa kongamano hilo kushikamana pamoja, kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanailinda amani ya nchi.

Wengine waliohudhuria kongamano hilo ni Mudir wa Azhar Sharif, Tawi la Tanzania, Sheikh Mohamed Hassan Attia, Sheikh wa Bakwata wilaya ya Temeke, Zailai Hassan Mkoyogole na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata wilaya ya Temeke, Sheikh Ally Mtulya.

Kituo cha Dini cha Kiislamu cha Az’har Shariif ni miongoni mwa vituo vya dini vilivyo mstari wa mbele katika kuandaa makongamano ya kidini katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa lengo la kuhamasisha mshikamano na kutoa mafundisho sahihi ya Uislamu.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close