8. Wema Waliotangulia

Tujifunzayo kutoka maisha ya Asmaa bint Umais

Sira ya Asmaa bint Umais (radhi za Allah zimfikie) ina wingi wa mazingatio kwa Waislamu wote, lakini zaidi yamejikita kwa upande wa kinamama wa Kiislamu wenye pupa la kutaka kuujua na kuutekeleza vyema Uislamu .

Wanaume kuingia katika majumba ya wengine bila ya nidhamu, kimaumbile na kisheria, ni jambo linalowakera sana waume na wazazi. Na hapa ndipo tunapogundua siri ya agizo lililokuja ndani ya Qur’an, (24:27) la kuwataka waumini wasiingie majumba yasiyo yao ila kwa rukhsa. Ukweli huu uko wazi katika sira ya Asmaa pale Abubakr kununa (kuhisi wivu) baada ya kuwakuta jamaa fulani (wanaume) nyumbani kwa Asmaa, na kwenda kulifungua duku duku lake kwa Mtume, kisha Mtume kuwaita waumini na kutoa onyo kali kwa wanaume wenye tabia ya kuingia majumba ya watu ovyo wakome. Licha ya kutoa onyo hilo, Mtume alimtakasa Asmaa kwamba ni mwanamke mchamungu. Yote haya yanatufunza unyeti wa kadhia hiyo na hekima kubwa iliyo katika Sharia ya Uislamu . Wanawake wanapaswa kumuiga Asmaa katika sifa ya kujiamini na uzuri wa kujieleza pamoja na kujenga hoja katika kuzitetea haki zao za msingi. Asmaa, bila ya hofu alimjadili Swahaba mkubwa, Umar pale alipomuhisi amekosea kwa kuyasema yale yale (ya dharau) wayasemayo watu mitaani kuwahusu Muhajiril-Habasha. Ukweli ni kwamba, Uislamu unapomtaja mwanamke kuwa mpungufu wa dini na akili hauna maana ya kuwa kiumbe huyu aliyekosa kheri, bali lengo ni kuwajuvya makaka zao (wanaume) kwamba kuna tofauti ya kiakili na kihisia baina yao kama wanavyotofautiana kimaumbile, (Walaysa dhakaru kal-unthaa) na kwa hiyo kimajukumu pia. Basi wanawake wanahitaji kutunzwa na kuonewa huruma pamoja na kupewa kila msaada waweze kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Jamii zinashuhudia kuwepo wanawake wanaowapita wanaume kiakili, kielimu, ukomavu wa fikra na kujiamini katika kufanya maamuzi, sifa ambazo baadhi ya wanaume hawana kabisa, ingawaje kimsingi na kwa mujibu wa Qur’an wanaume ni bora kuliko wanawake “…na nyinyi mna daraja kuwazidi wao…” (Quran, 2:228). Mfano mzuri wa hoja yetu ni Bi Asmaa (Allah amridhie) na hatua aliyoichukua kumpa ukweli Swahaba mkubwa Umar na kisha kumkabili Mtume mwenyewe kuonesha hisia zake, kitendo ambacho kilipongezwa sana na wanabahari wenziwe wakiwemo kina Abuu Mussa al-Ashariy. Wanabahari wenzake walishindwa kuondoa kero lile kwa hiyo baada ya tukio lile walimuona Asmaa kama shujaa aliyewatetea na hivyo kuwa sababu ya hadhi yao kutambuliwa Madina mjini Madina. Huu ndio mchango wa mwanamke katika jamii anapoiva kiimani, kitaaluma, kimalezi na kiharakati na kuwa mwenye kujitambua na kuielewa nafasi yake katika jamii yake. Hata hivyo, nafasi hii hawezi kuifikia mwanamke aliyeilemaza na kuiendekeza nafsi yake akawa hawazi ila namna ya kupata kila wiki aina mpya ya mavazi, mapambo na vipodozi vya gharama, asiyejishuhulisha na taaluma ya dini yake. Nafasi kama ya Asmaa haifikiwi na ambaye ameipenda dunia kwa kiwango cha kutisha na kuifanya kuwa ndipo pahala pekee pa kumaliza starehe zake, mwisho akawachukia hata viongozi wa dini na walinganiaji kama tunavowaona akina-Hawa wengi hivi leo. Tujifunze pia jinsi wanawake wema walivyokuwa wakiwajibika katika kazi za nyumbani na kuwatunza watoto wao kwa usafi na kuwaandalia milo mizuri, Hakika ni jambo tunu la kuigwa. Wa l i j u e hilo zai d i wapendao raha kupindukia, wanaowalazimisha waume zao kuwawekea wafanyakazi majumbani ili wao wabaki bila ya shughuli yoyote. Mwanamke anayejielewa na anayejuwa udhaifu wa maisha haya hakai bila ya kuwajibika na huzingatia utendaji wake wa kazi za nyumbani mwake kuwa ni sehemu ya sadaka itakayomfaa katika maisha ya baadaye kwa vile hayo yameshafanywa na watuku- fu kuliko yeye.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close