8. Wema Waliotangulia

Tujifunzayo katika maisha ya Salmaan bin Alfaarisy MAISHA YA MASWAHABA: 4

Tunapoipitia sira ya kila Swahaba katika Maswahaba wa Mtume, tunakuta maajabu na mazingatio makubwa yanayogusa maisha yetu kiimani, kifamilia, kiutamaduni na kijamii. Hata hivyo, safari ya Maswahaba ya kuitafuta neema ya Uislamu hutofautiana sana.

kwa mfano, safari ya kuufikia Uislamu ya Maswahaba kama vile Abubakr, Uthman, Ali, Abdurahman bin Auf zilikuwa fupi sana, lakini safari ya Swahaba Salmaan [Allah amri- dhie] ilikuwa ndefu na yenye mlolongo wa matukio mviringo ambayo hutupa wingi vile vile wa mazingatio.

Bila shaka, mpendwa msomaji aliyekuwa akifuatilia kisa na mikasa ya Swahaba huyu mtukufu ataweza kubaini mafunzo mengi tunayopaswa kuyachukua. Hapa tutataja baadhi ya mafunzo hayo.

Udanganyifu wa baadhi ya viongozi wa dini

Viongozi wa dini wakikosa uaminifu kwa Waumini wao hujishushia hadhi na hukera. Pia, viongozi wa aina hiyo ni chanzo cha uchafuzi wa imani husika na kusababisha mtafaruku. Tumeona jinsi mwalimu wa kwanza wa Swahaba Salmaan alivyokosa uaminifu, ambapo alikuwa akizikunja sadaka za waumini wake kwa jina la dini huku akijilimbikizia makasiki ya dhahabu nyumbani mwake.

Tunaelezwa katika historia kwamba chanzo cha kuibuka dhana ya ukoministi duniani ilikuwa ni viongozi wa dini kujifunika mwamvuli wa dini na kutenda maovu hususan kuwadhulumu wafuasi waona kujinufaisha binafsi. Hali hiyo ilipelekea watu kutoona haja ya kuwepo dini kama mfumo wa maisha, na hivy owakakana uwepowa Muumba wa ulimwengu na vilivyomo na pia wakakana uwepo wa maisha baada ya kufa.

Walimkana Mwenyezi Mungu mmoja sio tu kwa lengo la kukwepa kuwajibika mbele kwake lakini pia kwa ajili ya kukwepa udanganyifu, ubabaishaji na dhuluma za walojipa ukubwa na uongozi wa dini kwa maslahi yao.

Utulivu wa moyo uko katika kuifuata dini ya haki

Jambo jingine tunalojifunza kutokana na maisha ya Swahaba Salmaan [Allah amridhie] ni kwamba, dini aliyoiteremsha Allah kwa waja wake humpatia mja faraja na utulivu wa moyo. Dalili ya hayo ni kule kutangatanga na hamahama inayoonekana kwa baadhi ya watu kutoka dini hadi dini nyengine, lakini akifika kwenye Uislamu moyo hutulia na
hukinaishwa na hoja na mafunzo yake safi matakatifu. Siri ya hayo yote ni kwamba Uislamu ndio dini ya Muumba, nyenginezo ni usanii wa mwanadamu.

Swahaba Salmaan, tokea siku alipowaona watu wakiabudu kinyume na utaratibu wa dini yao na katika safari yake kuitafuta dini ya haki alikosa utulivu wa kiroho, lakini alipokutana na Mtume [rehema za Allah na amani zimshukie] pamoja na Maswahaba zake na kuupata Uislamu, alipata utulivu wa nafsi na safari yake ilifika mwisho. Wala Mtume hakumuuliza tena Mtume kwamba akifariki aelekee kwa nani.

Utume wa Muhammad kuthibitishwa na wanadini

Watu wanaokataa utume wa Muhammad na kukubali utume wa waliomtangulia wanapaswa kuizingatia kwa makini historia ya Swahaba huyu mtukufu. Utume wa Muhammad [rehema na amani za Allah zimfikie] tumeona umethibitishwa na Padri [mtawa] wa mwisho kule Ammuuriya alikosoma.

Tumeona jinsi padre yule alivyomuhakikishia kwamba hakuna tena msomi yoyote aliye juu ya dini sahihi kwa zama zile lakini tayari zimefika zama za kuja Mtume wa mwisho na kumpa wasifu wake. Ikiwa limethibitishwa hilo na wasomi wa Ukristo tokea zamani,.Mkristo wa leo ama mfuasi wa dini yoyote, kama ni mkweli wa nafsi yake, inafaa awe makini sana katika kuihakiki dini inayomkataa Mtume huyu wa mwisho, Muhammad [rehema za Allah na amani zimshukie] kwa usalama wake mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema: “Hakika dini ya kweli mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu….” [Qur’an, 3:19].

Pia anasema: “Je wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na ardhini kinamtii yeye kikipenda kisipende; na kwake mtarejeshwa.” [Qur’an 3:83].

Na anasema: “Na atakayetaka dini isiyokuwa Uislamu, basi hatokubaliwa na huko akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.” [Qur’an, 3:85].

Mvuto wa dini ya haki hauzuiliki

Watu wanaposafiri ndani ya maisha ya kila siku kwa malengo mbalimbali, safari zao huhusisha muda, maeneo pamoja na roho. Safari ya Muirani huyu, Salmaan ilikuwa ya kiroho zaidi. Licha ya kutumia muda kukata masafa, pia alisafiri baada ya kukata kamba na minyororo aliyotatizwa na baba yake.

Alisafiri huku moyoni mwake kukiwa na kitu kizito mithili ya chuma, haki ikiwa mbele naye akiwa nyuma yake. Kwa ajili ya hili, moyo wake ulipata msukumo wa ajabu, na haukutulia mpaka alipoikamata dini ya haki.

 

Udanganyifu wa baadhi ya viongozi wa dini

Viongozi wa dini wakikosa uaminifu kwa Waumini wao hujishushia hadhi na hukera. Pia, viongozi wa aina hiyo ni chanzo cha uchafuzi wa imani husika na kusababisha mtafaruku. Tumeona jinsi mwalimu wa kwanza wa Swahaba Salmaan alivyokosa uaminifu, ambapo alikuwa akizikunja sadaka za waumini wake kwa jina la dini huku akijilimbikizia makasiki ya dhahabu nyumbani mwake.

Tunaelezwa katika historia kwamba chanzo cha kuibuka dhana ya ukoministi duniani ilikuwa ni viongozi wa dini kujifunika mwamvuli wa dini na kutenda maovu hususan kuwadhulumu wafuasi waona kujinufaisha binafsi. Hali hiyo ilipelekea watu kutoona haja ya kuwepo dini kama mfumo wa maisha, na hivyo wakakana uwepowa Muumba wa ulimwengu na vilivyomo na pia wakakana uwepo wa maisha baada ya kufa.

Walimkana Mwenyezi Mungu mmoja sio tu kwa lengo la kukwepa kuwajibika mbele kwake lakini pia kwa ajili ya kukwepa udanganyifu, ubabaishaji na dhuluma za walojipa ukubwa na uongozi wa dini kwa maslahi yao.

Utulivu wa moyo uko katika kuifuata dini ya haki

Jambo jingine tunalojifunza kutokana na maisha ya Swahaba Salmaan [Allah amridhie] ni kwa heshima yake na kukubali usumbufu mkubwa, ikiwemo kuingia katika utumwa zaidi ya mara moja. Pia alitekwa na watu makhaini aliyewapa wanyama wake kama malipo ya kumpeleka alikoelekezwa na mwalimu wake.

Yote haya yanatufunza kuwa, haki ni kitu ghali zaidi, na mtu anayeitafuta ataipata. Muhimu ni kuwa, mtu akipata imani ya kweli hana budi kuitunza na kuishikilia kisawasawa kwani haifanani na kitu chochote chengine kwa thamani.

Dini ya haki huthibiti kwa hoja

Baadhi ya watu huridhika na imani walizozirithi kutoka kwa wazee wao. Watu hawa Allah anawaelezea kama ifuatavyo: “Na wanapoambiwa fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu husema,

Bali tunafuata tuliyowakuta nayo wazazi wetu.’ Je hata kama wazazi wao hawazingatii lolote wala hawakuongoka?” [Qur’an 2:170].

Kuomba ushauri na wasia

Katika maisha ya Salmaan tunajifunza pia umuhimu wa kuwaheshimu wanazuoni, kuwatumikia na kuomba ushauri katika masuala mbalimbali yakiwemo ya utekelezaji wa majukumu ya kidini kama alivyofanya swahaba huyu kila alipohisi mwalimu wake anakaribia kuondoka duniani.

Subira ndio ufunguo wa kheri

Mtu kamwe hawezi kuyafikia malengo kama vile kutafuta elimu, biashara nk, iwapo hatakuwa na subra na kuwa tayari kubeba mashaka ya safarini. Tumeona safari ya Salmaan ilivyomtoa Furs mpaka Sham, na kutoka Sham [Palestina] mpaka Iraq, na kutoka hapo mpaka Nasibiin, kisha mpaka Ammuuriya, na kutoka hapo mpaka Waadil-quraa [mji kati ya Madina na Sham] na mwisho akafika alipopakusudia, Madina.

Ilikuwa ni safari nzito iliyojaa mashaka ambayo ilikata maelfu ya kilomita kwa ajili ya kutafuta misk ya roho na utulivu wa nafsi.

Baada ya dhiki huwa faraja

Safari inapokuwa kwa ajili ya Allah, licha ya masumbufu yatakayomfika msafiri, mwisho huwa na kheri nyingi ambapo Allah hubadilisha dhiki mbele kuwa faraja.

Hili liko wazi katika safari ya Alfarisy [Allah amridhie]. Kwani hakuna faraja kubwa zaidi kuliko kukutana na Mtume na kuishi naye. Hapa tunajifunza pia kutokukata tamaa zinapotufika changamoto tunapokuwa katika shughuli zetu za kidaawa na za kimaisha kwa ujumla, madhalitunajua tupo katika yanayomridhisha Allah Aliyetukuka.

Allah Aliyetukuka awe radhi na Salmaan, Mwenda nyuma ya haki, na atunufaishe kwa historia na elimu yake, amiin.

 

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy, Maisha yake baada ya kusilimu

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close