8. Wema Waliotangulia

Maisha Ya Hindu Bint Utbah, Mke Wa Abuu Sufiani

Msimamo wake mbele ya Mtume

Hindu baada ya kusilimu alikwenda kwa Mtume na kuudhihirisha msimamo wake kwa kusema: “Ewe mjumbe wa Allah, Wallahi hawakuwepo watu ninao wachukia na kuwatakia kila baya liwafike kuliko wafuasi wako, lakini nashangaa sasa kuwa hakuna katika mgongo wa ardhi watu niwapendao na kupenda Allah awape heshima kuliko wafuasi wako.” Mtume alifurahi na kumwambia: “Na ndivyo hivyo yatakavyozidi mapenzi yako kwa Waislamu kadri imani yako inavyotulia ndani ya moyo wako, na bughudha inavojitenga nawe mpaka hapatabaki athari yoyote.” Khutba ya Mtume kwa wanawake Mtume alipofanikiwa kuikomboa Makka, haki iliwabainikia Makureishi na wakajua kuwa hakuna njia ya salama na uamuzi wa busara ila kuukubali Uislamu, wakasilimu. Wakiwa wamenywea na kusubiri maamuzi ya Mtume (nini atawafanya), Mtume aliwasamehe na akawaita kwa ajili ya kuchukuwa ahadi zao za utiifu (bay-ah ). Ndipo Mtume akakaa mbele ya mlima wa Swafaa huku Sayydina Umari akiwa ubavuni kwake, akachukuwa ahadi ya utiifu kutoka kwa hadhara kubwa ya watu wa Makka. Alipomaliza kwa wanaume akaenda kwa wanawake.

Hindu aikatiza khutba ya Mtume mbele ya wenzake

Katika hotuba yake, Mtume alisema: ”Nachukua ahadi zenu kwamba hamtamshirikisha Allah na chochote…na hamtoiba.” Hindu akasema: “Abuu Sufian ni mtu bahili, hivi nitakuwa na kosa nikichukuwa sehemu ya mali yake bila ya idhini yake?” Mtume akamwambia: “Chukua katika mali yake kiasi cha kukutosha wewe na watoto wako kwa uangalifu.” Mtume akiendelea na hotuba yake akawaambia: “Wala msizini.” Hindu akakatiza tena na kusema: “Hivi kweli mwanamke muungwana huzini?!” Mtume akaendelea: “Wala msiuwe watoto wenu” Hindu akasema: “Tuliwazaa na kuwalea wakiwa wadogo mkawaua walipokuwa wakubwa (siku ya Badr).” Umar akacheka sana. Mtume akaendelea: “Wala msilete uongo kwa mikono yenu na miguu yenu” Hindu akasema: “Wallah! Uongo ni kitu kiovu sana na wewe unayotuamrisha ni kweli tupu, uongofu na tabia njema.” Mtume akasema: “Na wala msiniasi kwa kila jema” Hindu akasema: “Wallahi hatukukaa hapa tukiwa na chembe ya uasi katika nafsi zetu.” Bukhari kutoka kwa Aisha (Taz: Swahabiyyat hawla rasuul Uk 514, Almuntaqa: 1/83).

Nafasi ya Hindu baada ya kusilimu Baada ya kusilimu,

Hindu alijitolea kwa kila aliloliweza kwa ajili ya kuitumikia dini hii tukufu, Hindu alibadilika na kuwa mpya kabisa na akawa mwanamke wa kipekee katika ulimwengu wa wanawake wa Kiislamu. Allah Ta’ala aliufungua moyo wake akausafisha na taka za ushirikina, hasadi, ujinga, kibri, ubabe na kumuweka mbali kabisa na upotofu; na hakurejea tena katika itikadi potofu. Inasemekana kwamba, aliposilimu alikwenda kulichanja sanamu lake la chumbani kwa shoka vipande vipande na kuliambia: “Tumep otoka kwa muda mrefu kwa sababu yako, huna maana yoyote (niondokee hapa) Pia Hindu alishiriki harakati zote za kuulinda na kuustawisha Uislamu, sambamba na kushiriki katika ‘Jihad fii Sabiili Llah’.

Kifo chake

Hindu baada ya kipindi kirefu – tangu kusilimu – cha kuutumikia Uisla mu, na kujipinda kwa aina zote za ibada zilizo ndani ya uwezo wake, ulifika wakati sasa mwili huu mtaharifu kurudi kwa Mola wake ukiwa na zawadi bora za toba, imani, ibada, jihad, mapenzi kwa Uislamu na Waislamu na ikhlasi. Vitabu vingi vya historia ya Uislamu vinaeleza kuwa bibi huyu alifariki katika ukhalifa (utawala) wa Sayidna Umar (Allah amridhie) na ndiyo siku alipokufa mzee Abu Quhafa baba wa Khalifa wa kwanza Abubakr Sidiiq (radhi za Allah ziwe juu yake) (Taz: Al-istiiaab).

Show More

Related Articles

Back to top button
Close