8. Wema Waliotangulia

Maisha Ya Hind Bint Utba

Wanawake wakiongozwa na Bibi Hind bint Utba, wakati vita vinashika nafasi yake, walisimama wakiimba na wakipiga madufu kwa kuwahamasisha mashujaa wa kikureishi, na kwa kweli Hind alikuwa na mchango mkubwa katika kuwaletea Makureishi ushindi kwa kuitumia sanaa yake ya utunzi na uimbaji mashairi wa papo kwa papo

Kabla ya kusilimu Leo tunaendelea kuhadithia na kisa cha Swahaba Hind na mumewe Abuu Sufian bin Harb tulichokianza toleo lililopita ambapo tuliona kuwa kabla ya kusilimu, kwa muda usiopungua miaka 20, alitumia mali, vipawa na muda wake kuendesha uadui dhidi ya Uislamu. Tuliona pia miongoni mwa waliouawa katika Vita vya Badr ambavyo Waislamu licha ya uchache na uhaba wa silaha, Allah aliwapa ushindi, ni baba wa Hindi bint Utba bin Rabi’ah, ami yake Shaiba bin Rabi’ah, na kaka yake Al-Waliid bin Utbah. Kutoka katika jeshi la Uislamu, aliyewaua baba na kaka yake Hind ni Sayyidna Hamza bin Abdil-Muttalib. Hili lilikuwa pigo kubwa sana lililozidisha hasira na uchungu moyoni mwa Hind, na akawa anafikiri usiku na mchana jinsi gani ataweza kulipiza kisasi cha jamaa zake hawa wapendwa. Hind katika Vita vya Uhud Baada ya kushindwa vibaya, Makureishi walishikwa na fazaa, vilio na myoyo yao kujawa na huzuni na majonzi na kuazimia kulipiza kisasi dhidi ya Waislamu. Mwaka mmoja baada ya tukio la Badr, Makureishi walikuwa tayari wameshajiandaa vya kutosha kwa kisasi. Likiwa na silaha za kutosha, jeshi lililozidi elfu tatu liliondoka na kuelekea Madina chini ya uongozi Abu Sufian. Makureish na mkakati wa kumuua Hamza Hakuna mtu ambaye Makureishi walimtaja muda wote kuelekea vitani na hadi kumpangia mkakati wa kipekee wa kummalzia, kama Hamza. Makureishi walikumbuka jinsi Hamza alivyowaua ndugu zao mwaka uliopita na uchungu walioupata. Hivyo basi, walimchagua kijana hodari kwa shabaha aitwaye Wahshy amuue Hamza. Wahshy, mwenye asili ya Kihabeshi, alikuwa ni mtumwa wa Jubeir bin Mut-im, mmoja wa mabwana wakubwa wa Kikureishi na alisifika kwa uhodari wa kurusha mikuki bila kukosea. Bwana wake alimtaka asijishughulishe na lolote wala yeyote na kumuahidi iwapo atafanikiwa kumuua Hamza atamuacha huru. Makureishi hawakutosheka na hilo, bali walimpeleka Wahshy kwa Hind akamuandae na kumpanga zaidi. Hind, ambaye alikuwa na hamu ya vita kuliko wengi miongoni mwa Makureishi, aliamini kwamba hakuna jambo lingempa faraja zaidi duniani kuliko kumuona Hamza amekatwa kichwa chake tena kwa gharama yoyote. Hind alitumia wakati wake mwingi kuujaza moyo wa Wahshy husda na kuuchochea moto wa chuki pamoja na kumchorea jukumu lake pekee (linalompasa) katika vita vya Uhud, nalo ni kumtowa roho Hamza tu. Hind amuahidi Wahshy vito vyake vya thamani Katika kumuandaa, Hind alimwambia Wahshy iwapo atamuua Hamza atamvulia mapambo yote ya thamani, ya fedha na dhahabu, yaliyoizunguka shingo na kifua vilevile kumpatia gharama za kuoa, ili siku moja Hind ayaone yametulia shingoni mwa mkewe, wakati huo akiwa huru, si mtumwa tena wa Kiafrika anayedhalilika mbele ya wakuu wa Makureishi (Taz. Swahabiyaat hawla rasuli Uk 507-508) Wahshy – ambaye naye alisilimu baadaye – aliiona kuwa hii ni fursa na bahati. Na kwa kuwa bahati haiji mara mbili, aliitumia vilivyo akiamini mwanga wa faraja utamjia katika maisha yake, iwapo atatimiza matakwa ya wakubwa. Hind alipowaongoza wanawake Uhud Abu Sufian aliwaandaa wanawake kadhaa kwenda vitani ili kuwahamasisha wapiganaji na kuwajaza moyo wa ushujaa na kujitoa muhanga wakati jiwe la vita likizunguka. Wanawake wakiongozwa na Bibi Hind bint Utba, wakati vita vinashika nafasi yake, walisimama wakiimba na wakipiga madufu kwa kuwahamasisha mashujaa wa kikureishi, na kwa kweli Hind alikuwa na mchango mkubwa katika kuwaletea Makureishi ushindi kwa kuitumia sanaa yake ya utunzi na uimbaji mashairi wa papo kwa papo. Kuuwawa kwa Hamza Maajabu na ufundi mkubwa wa kuzifyeka shingo za maadui ulionekana kwa Simba wa Mwenyezi Mungu, Hamza (Radhi za Allah zimfikie) bila ya kujua kwamba kuna mtu anamsubiri kwa shauku ya pekee ili amuue. Wahshy alikuwa akimvizia na kumfata kwa karibu sana, na kwa hakika alifanikiwa kwa vile Allah alishakadiria. Lipangwalo na Mola halipanguki. Wahshy alifanikiwa kumuua Asadullah (Simba wa Mungu) na Makureishi walifurahi na kupaza sauti zao kwa mayowe na vifijo k u o n e s h a k u w a wameshinda kwa kumuua Hamza na Maswahaba wengine wapatao jumla 70. Hata hivyo, miongoni mwa waliofurahi zaidi siku hii ni Hind ambaye alipanda juu ya kilima na kutumbuiza kwa kuimba mashairi huku wanawake wenziwe wakicheza. Makureishi walifanya unyama wa ajabu dhidi ya maiti za Mashahidi. Waliwakatakata viungo vyao na kulipasua tumbo la Hamza ambapo Hind alilitafuna ini lake na kulitema. (Taz: Swahaabiyaat hawla rasul Uk 511) Kusilimu kwa Hind Hind alibaki katika ushirikina yeye na mumewe mpaka Allah akafungua mioyo yao katika mwaka wa nane Hijriyya, Makka i l i p o t e k w a . Hapo wakasilimu. N a hapa ni vyema turejee kisa cha kusilimu kwao. Wakati Mtume na jeshi lake wanaingia Makka kuiteka; ami yake, Abbas bin AbdilMuttalib, pamoja na familia yake nao walikuwa njiani kuelekea Madina wakiwa Waislamu tayari. Mtume alimrudisha Abbas alikotoka na kumuamrisha aiachie familia yake iendelee na safari. Abbas akiwa amepanda nyumbu wa Mtume, alikutana na Abu Sufian usiku akiwa na wenzake akina Hakim bin Hizaam na Badiil bin Warqaa kwenye lindo lao kuangalia usalama wa mji wao bila kujua ujio wa Mtume Makka. Abbas akamwambia Abu Sufyan: “Wewe! Mtume wa Allah yupo karibu na asubuhi anaingia hapa akiwa na jeshi kubwa hamuliwezi.” Abuu Sufian akamwambia: “Sasa nini la kufanya Abaa Fadhl?” Akamwambia: “Wallahi akikupata nina uhakika anakukata shingo yako. Panda nikupeleke umuombe amani.” Alipofika, naye Mtume akamwambia Abbas: “Nenda, kuwa naye Abuu Sufian katika hifadhi yako ikifika asubuhi mlete.” Majadiliano ya Mtume Na Abuu Sufian M t u m e : “Hivi haujakufikia wakati Abaa Sufia n w e w e k u a m i n i k w a m b a h a k u n a Mola wa kuabudiwa kwa haki ila Allah?” Akasema: “Nakiri upole, ukarimu na usamehevu wako, imeshanibainikia kwamba pangelikuwa na mungu zaidi ya Allah angelinisaidia leo hii (nakubali hilo).” Mtume akamuuliza tena: “Abaa Sufian, hivi haujafika wakati wewe kuamini kuwa mimi ni Mjumbe wa Allah?” Akasema: “Hili bado nina mashaka nalo.” Abbas akamdakiza na kusema: “Sikiliza wewe, tamka Shahada kabla hujauwawa. Mwenyezi Mungu akatia nuru ya Uislamu katika moyo wa Abuu Sufian, na akatamka Shahada yote pale pale.” Abbas akamwambia Mtume: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wewe unajuwa kwamba Abu Sufian anapenda ukubwa na kutajwa, basi naomba umpe nafasi yoyote (wadhifa) ili ajisikie.” Mtume akasema: “Atakayeingia nyumba yako amesalimika, atakayeweka silaha chini amesalimika na atakayeingia msikitini amesalimika na atakayejifungia mlango wake amesalimika.” Kisha Mtume (amani ya Allah iwe juu yake) akamuagiza Abbas (radhi za Allah ziwe juu yake) amsimamishe Abuu Sufian juu ya kilima ili aone vikosi vya jeshi la Mtume vikipita. Baada ya kuliona jeshi, alishangazwa na kutishwa zaidi na wingi na uchangamfu wao. Hapo alitoka mbio na kwenda kuwatahadharisha Makureishi kwa kuwaambia: “Enyi Makureishi, ole wenu, Muhammad amekuja na nguvu msiyoiweza kamwe, basi atakayeingia nyumba ya Abuu Sufian ameokoka.” Ndipo mkewe kwa hasira akamshika ndevu zake akamtikisa na kumwambia: “Kwa nini hamumuui mchonganishi huyu muovu! Ah! Siku mbaya ilioje hii kwangu!” Hofu yawatanda Makureishi Kauli ya Abu Sufian iliwatia hofu na fazaa kweli kweli Makureishi na kumwambia: “Mungu akulaani wewe! Unadhani nyumba yako itatusaidia nini leo.” Akawaambia: “Na atakayejifungia mlango au kukimbilia msikitini atakuwa salama.” Watu wakatawanyika. Yasemekana Abu Sufian alikwenda kumwambia Mtume: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi umekuja kuwamaliza jamaa zako (Makureishi)?” Mtume akamwambia: “Hapana”. Kisha akayakariri yale maneno tena. “Atakayeingia nyumba yako amesalimika, atakayeweka silaha chini amesalimika na atakayeingia msikitini amesalimika na atakayejifungia mlango wake amesalimika” Hind amfuata mumewe Hind bint Utba (radhi za Allah zimshukie) akaishiwa na hila na kujiona kama yuko sehemu amezibiwa njia zote ila njia ya kuuelekea Uislamu. Na baada ya uadui wa miaka takriban 20, Allah Ta’ala naye akaufungua moyo wake. Alimfuata mumewe na kumwambia: “Mume wangu, mimi nataka kumfuata Muhammad.” Abuu Sufian akamwambia: “Si nimekuona ukimchukia mpaka jana?” Akasema: “Wallahi sijapat a p o k u o n a Mu n g u kuabudiwa kwa usahihi kabla ya siku hii! akashahadia shahada ya haki.” (Swahabiyaat hawla rasuli uk:513)

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close