7. Visa Vya Mitume

NABII MUSA

mtume aliyepasua bahari kwa fimbo
SEHEMU YA 10 Katika makala iliyopita tuliona Nabii Musa ak- ipewa ufunuo na Mola wake Mlezi katika Jangwa Tukufu laTuwa. Katika makala hii tut- aangazia Nabii Musa akipewa miujiza na Mola wake. Sasa ende- lea…

Moto katika Jangwa Takatifu la Mlima Tuwa

Musa aliutazama moto katika Mlima wa Tuwa na kurejea nyuma huku akiwa anatetemeka. Musa pia aliona mti wa ki- jani inayokurubia weusi huku ukiungua. Lakini kila moto ulipokuwa ukizidi na rangi ya kijani nayo iliendelea kuzidi. Musa (amani iwe juu yake) aliondoka huku akitetemeka, licha ya kupata vugu- vugu la moto. Mti huu ulikuwa katika mli- ma upande wa magharibi kuliani mwake. Na hili jangwa alilokuwa Musa amesima- ma ndani yake ni Jangwa la Tuwa. Ghafla Musa akasikia sauti ya Mwenye- zi Mungu Aliyetukuka ikimwita: “Basi al- ipoufikia akaitwa, ‘Ewe Musa! Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde Takatifu la Tuwa,’” (Qur’an, 20:11-12) Akiwa katika jangwa la Tuwa, Musa (amani iwe juu yake) alikuwa anaelekea upande wa Qibla, na mti huo ulikuwa up- ande wa Magharibi, kuumeni kwake. Mola wake Mlezi akamwita na kumua- mrisha kuvua viatu vyake kwa taadhima na kutukuza pamoja na kulipa hadhi eneo hilo lililobarikiwa na katika usiku huo ul- iobarikiwa. Musa akazidi kupatwa na mshangao, pale sauti ya juu kutoka kwa Mola Mlezi wa viumbe wote ilipoita: “Na Mimi nime- kuteua wewe, basi sikiliza unayofunuliwa. Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana Mungu ila mimi tu. Basi niabudu mimi na ushike sala kwa jili ya kunikum- buka Mimi” (Qur’an, 20:13-1). Fimbo ya Nabii Musa (amani iwe juu yake) Hakika kiwiliwili cha Nabii Musa (am- ani iwe juu yake) kilikuwa kikichemka kutokana na haiba na utukufu wa mahali adhimu huku akisikiliza muongozo na mafundisho kutoka kwa Muumba wa ar- dhi na mbingu saba. Kisha, Mwenye haki Aliyetukuka akamwambia Musa: “Na nini hicho kili- chomo mkononi mwako wa kulia ewe Musa?” (Qur’an, 20:17) Nabii wa Allah Musa (amani iwe juu yake) akapatwa na hali ya mshangao. Al- lah anamuuliza na hali ya kuwa Yeye ndiye Mjuzi wa kila kitu. Hivi ni kwa nini amu- ulize Musa swali hilo? Bila ya shaka kuna hekima kubwa ambayo yeye Musa (amani iwe juu yake) haijui. Musa (amani iwe juu yake) akamjibu akajibu: “Akasema, ‘Hii ni fimbo yangu, naiegemea na ninawaangushia majani kondoo na mbuzi wangu. Tena inanifaa kwa matumizi mengine,” (Qur’an, 20:18). Na ilitosha Musa (amani iwe juu yake) kujibu kwa neno moja tu. “Hii ni fimbo yangu,” (Qur’an, 20:18), lakini alirefusha jibu kwa sababu anahisi raha ya ajabu ndani ya nafsi yake kuongea na Mola wake Mtukufu na kumsikia moja kwa moja. Allah Aliyetukuka akamwambia Musa: “Itupe fimbo hiyo, ewe Musa!” (Qur’an: 20:19). Musa akaitupa fimbo yake haraka, na akatishika pale alipoona imegeuka kuwa nyoka mkubwa mnene akiwa na meno na chonge akitikisika kama nyoka wa kweli…Musa hakuona njia nyingine isipokuwa, “Akarudi nyuma wala hakuta- zama” (Qur’an, 28:31). Musa alikuwa akimkimbia nyoka huyo bila ya kugeuka nyuma. Mola wake Mlezi akamuita: “Ewe Musa! Njoo mbele wala usiogope. Hakika wewe ni miongoni mwa waliosalimika,” (Qur’an, 28: 31). “Ewe Musa usihofu! Hakika hawahofu mbele yangu Mitume,” (Qur’an, 27). Na wakati aliporejea tena Allah Ali- yetukuka alimuamrisha kuichukua tena fimbo yake, “Akasema, ‘Ikamate, wala usi- ogope! Tutairudisha katika hali yake ya kwanza,” (Qur’an, 20:21). Husemwa ya kuwa Musa aliiogopa fimbo hiyo, hivyo akaweka mkono wake pembeni yake, kisha mkono wake mwingine akauweka katikati ya mdomo wake. . . Musa alivyotulizana ikarejea kuwa fimbo yenye pande mbili kama ilivyokuwa mwanzo. Utukufu ni wake aliyekuwa na uwezo mkubwa. Mola Mlezi wa Mashariki mbili na Magharibi mbili!

Muujiza wa mkono wa Nabii Musa

Kisha Allah Aliyetukuka akamwamuru Musa kuingiza mkono wake katika mfuko wake, kisha akamwamuru kuutoa. Kwa mshangao ukawa mkono unang’ara na kumeremeta kwa weupe mithili ya mbalamwezi. Allah Aliyetukuka anasema: “Ingiza mkono wako kwenye mfuko wako, uta- toka mweupe pasipo na ubaya. Na jiam- batishe mkono wako ukihisi hofu” (Qur’an, 28: 32). Maana yake, mkono utakapofifia nuru yake uweke juu ya moyo wako kwa kufan- ya hivyo hofu itaondoka. Na katika hali hiyo, ulikuja wito kutoka kwa Mtukufu Mwenye hekima kumwam- bia Musa: “Basi hizi ni dalili mbili zitokazo kwa Mola wako Mlezi kumpelekea Firauni na wakuu wa umma wake. Hakika hao walikuwa watu mafasiki,” (Qur’an, 28:32). 10 Katika makala iliyopita tuliona Nabii Musa ak- ipewa ufunuo na Mola wake Mlezi katika Jangwa Tukufu laTuwa. Katika makala hii tut- aangazia Nabii Musa akipewa miujiza na Mola wake. Sasa ende- lea… Nabii Musa alijua ya kuwa ameamrish- wa kufikisha ujumbe wa Mola Mlezi wa vi- umbe wote, na ni juu yake kuufikisha ujumbe aliyoamrish- wa. Allah amem- chaguayeyemwenyewe kusimamia jambo hilo na inatosha kwake yeye na Kwa maoni wasiliana kufanya hivyo. Na jam- bo la Allah Aliyetukuka litatimia kwa idhini yake. Itaendelea…

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close