7. Visa Vya Mitume

NABII MUSA: Mtume aliyepasua bahari kwa fimbo

SEHEMU YA 12 Katika makala iliyopita tuliona Allah Ali- yetukuka akimtaka Musa na ndug- uye Harun ku- tumia lugha nzuri na ya sta- ha katika kufik- isha ujumbe wa Allah kwa Firauni. Katika makala hii, Al- lah Aliyetuku- ka anawahak- ikishia wao ku- wapa ulinzi wa uhakika. Sasa endelea…

Msihofu nipo pamoja

Musa (amani ya Allah imshukie) alifika katika ardhi ya Misri na kwenda moja kwa moja kwamamayakenakakayake Harun. Awali, hawakumjua lakini baadaye wakam- baini na kumsalimia. Musa alimwambia kaka yake Harun (amaniyaAllahimshukie):“Hakika Mola wangu Mlezi ameniamuru niende kwa Firauni ili ni mlinganie kwa Allah..Na Mola wangu Mlezi pia amekuamuru wewe uni- saidie mimi katika jukumu hili.” Harun akasema: “Nimekubali na kutii amri ya Mola wanguMlezi.” Musa na Harun (amani ya Allah iwashukie) walienda kwa Firauni majira ya usiku, akaupiga kwa fimbo yake mlango wa kasri. Firauni, aliposikia kishindo hicho, akaghadhibika na kusema: “Ni nani huyu jasiri anayegonga mlango wangu namna hii!” Mabawabu na walinzi wakamuhabari- shayakuwa hapaamefikamwendawazimu mmoja anadai eti ya kuwa yeye ni Mtume wa Allah. Firauni akasema: “Hebu niletieni mtu huyo.” Musa na Harun wakaingia kwa Firauni na kumwambia: “Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache wana wa Is- rail watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tu- mekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani itakuwa juu ya aliyefuata uongofu.” (Qur’an 20: 47). Kwa maana, tumekujia na muujiza uto- kao kwa Mola wako Mlezi na amani iwe juu yako iwapo utafuata uongofu. “Hakika tu- mefunuliwa sisi kwamba hapana shaka ad- habu itamsibu anayepinga na akapuuza,” (Qur’an 20:48). Kwa maana, hakika Allah ametuhabari- sha kwa njia ya wahyi uliohifadhiwa ya kuwa adhabu itamshukia yule anayepinga alama za uwepo wa Allah na akakataa kumtii yeye, (Taz: Mukhtasar wa tafsri ya Bin Kathiri 3/138).

Sasa uso kwa uso na Firauni

Musa (amani ya Allah imshukie) alianza kuusemesha moyo wa Firauni kwa maneno laini akiamini huenda labda moyo wake ukalainika au kumwamini Mola Mlezi wa viumbe wote. Musa akamsimulia kuhusu rehema za Allah na pepo yake, na kwamba yeye hana lengo la kupora ufalme wake, bali anachotaka ni kumuongezea ufalme mkuu kushinda hata huo alikuwa nao hivi sasa. Firauni aliahidiwa ufalme huo wa kupa- ta pepo zenye neema, iwapo atamuamini AllahAliyetukuka na kunyenyekeakwake. Pamoja na hivyo, Firauni alikuwa ak- isikiliza manenoyaMusa(amaniyaAllah imshukie)kwadharaunakisha Musa(am- ani imshukie) akamuuliza kwa kejeli: “Sawa, sasa kitu gani unachohitaji kutoka kwangu!?” Musa akajibu: “Nataka unikabidhi hawa wana wa Israil.” “Basi waache wana wa Is- raili waende nami” (Qur’an, 7:105). Kwa maana, waachie wawe huru waepukane na vitisho vyako na waache wafuate ibada ya Mola wao Mlezi. Hakika wao ni uzao wa Nabii Mtukufu Israil, am- baye ni Yakubu bin Is’haka bin Ibrahim rafiki wa Allah, (Taz: Mukhtasari wa tafasiri ya ibn Kathiri 2/227). Wakati Musa alipomwambia maneno hayo, Firauni alimdharau na kamkumbu- sha fadhila zake alizomfadhili huko nyuma kwa kumwambia: “Hivi sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi? Na ukatenda kitendo chako ulichotenda nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani?” (Qur’an 26”18- 19) Hayandiyomalipoyetu tuliyokuleana kukukirimu katikarikalautotowako?Leo unatujianakupinga diniyetu?Nakutaka kumtoa mfalme ambaye wewe mwenyewe umekulia nyumbani kwake, na unamlinga- nia katika dini ya Mwenyezi Mungu asi- yekuwa yeye?! Wewe una jipya gani-si umeishi pamoja nasi miaka chungu zima- hujawahi hata siku moja katika kipindi hicho kutuhadithia haya unayotueleza leo, na wala hukutuhofi- sha na ishara yoyote ile ya jambo hili kubwa?! Na Firauni anamkumbusha tukio lake la kumuua yule Muisraili kwa nia ya kumti- sha na kulikuza jambo hilo. “Na ukatenda kitendo chako ulichotenda nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani?” (Qur’an 26:19). Kitendo ulichokifanya wakati ule ki- likuwa kibaya na cha kufedhehesha kinatia kinyaa kukisema hivi sasa! Wewe ulikifanya kitendo hicho. “Nawe ukawa miongoni mwawasionashukrani?”(Qur’an, 26:19). Kwamaana,ulikuwanikatikawatu waasi. Hivi ndivyo Firauni alivyokusanya hoja zake zote ambazo alifikiri itakuwa mwiba mchungu kwa Musa (amani ya Allah im- shukie) kiasi ashindwe kuzijibu hoja hizo. Firauni alitegemea kutumia simulizi ya tukio la kuua, akionesha uwezakano wa tukio hilo kuchukua sura ya ulipizaji kisasi.

Firauni anamtisha kwa maneno mazito!

Lakini Musa Allah aliyetukua akiwa ameshamuondolea kitata (kigugumizi) ka- tikaulimiwake, akaanzakuzipanguahoja zake kwa kujibu: “Nilitenda hayo hapo nilipokuwa miongoni mwa wale walio- potea. Basi nikakukimbieni nilipo kuogo peni, tena Mola wangu Mlezi akanitunukia hukumu, na kunijaalia niwe miongoni mwa Mitume. Na hiyo ndiyo neema ya kuni- simbulia. na wewe umewatia utumwani wana wa wa Israil?” (Qur’an, 26:20-22).

 

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close