7. Visa Vya Mitume

Kisa cha Nabii Yunus Aliyemezwa Na Samaki

Katika mji mmoja ulioitwa (Ninawaa), aliishi Nabii Mtukufu Yunus (amani iwe juu yake). Allah alimtuma Yunus kwa watu wa mji ule ambao waliishi katika mazingira ya ujinga na ushirikina kwa muda mrefu.

Allah alimtuma Nabii Yunus (amani iwe juu yake) ili awahubirie watu wake katika kumwamini Allah pekee na kumwabudu Yeye Aliyetukuka. Lakini watu wa mji wa Ninawaa walikataa kumwamini Mwenyezi Mungu mmoja na wakaendelea kuishi katika giza la ushirikina na ukafiri. Wakati Nabii wa Allah, Yunus (amani iwe juu yake), alipokata tamaa aliondoka katika mji wa Ninawaa na akawaahidi wakazi wake adhabu ya Allah itakayowashukia baada ya siku tatu. Toba ya watu wa Nabii Yunus Nabii Yunus (amani ya Allah iwe juu yake) hakusubiri kupata maelekezo kutoka kwa Mola wake Mlezi ya amri ya kuondoka Ninawaa ambako watu walikataa mafundisho ya Allah. Badala yake Nabii Yunus akajichukulia mwenyewe maamuzi ya kutoroka huku akiwa na huzuni pamoja na ghadhabu. Hakutambua kuwa kufanya hivyo ni kosa na kwamba kuongoa watu si jukumu lake, bali jukumu lake ni kuwahubiria watu mafundisho ya Allah. Hakika anayemiliki suala la kuongoa si binadamu wala malaika isipokuwa Allah aliyetukuka. Nabii Yunus alipoondoka katika mji wa Ninawaa, ambako watu walizidhulumu nafsi zao, naye akaamini kuwa wapo tayari kuikabili adhabu itakayoshuka juu yao; Allah alizilainisha nyoyo zao wakaleta toba na kumrejea Yeye na kujutia mabaya waliyokuwa wakimfanyia Mtume wao Yunus. Watu wa Ninawaa wakaleta toba kwa kumtenganisha kila mnyama na mtoto wake, kisha wakamrejea Allah aliyetukuka na kumyenyekea pamoja na kujikurubisha kwake. Watu wazima wanaume kwa wanawake, watoto wa kike na wa kiume walilia, mifugo yao ikapiga kelele, majike ya ngamia, ng’ombe na kondoo wakatenganishwa na ndama zao . Hali ilikuwa nzito, Allah kutokana na uwezo wake, upole wake na rehema zake aliwaondoshea adhabu kali mfano wa usiku wenye kiza kinene ambayo lau kama si toba yao ingeliwapata, (Taz: Albidaya Wannihaya:1/232) Na kwa kuzingatia hilo, Allah aliyetukuka anasema: “Kwa nini usiwepo mji mmoja ukamwamini na imani yake ikafaa isipokuwa kaumu ya Yunus? Waliamini na Sisi tukawaondolea adhabu ya hizaya katika maisha ya dunia, na tukawastarehesha kwa muda.” (Qur’an, 10: 98). Mola wetu Mlezi aliyetukuka ametuhabarisha kwamba imani ya watu wa Yunus iliwanufaisha Allah akawaondolea adhabu baada ya kuwa imeshawazunguka wao kila upande. Na siku tatu zilipopita, Yunus alirudi kutazama adhabu aliyowaahidi jamaa zake, na ni kitu gani Allah angefanya. Yunus aliamua kujitenga nao na wala hakuwa anajua kwamba walileta toba na kumrejea Muumba wao. Nabii Yunus aliwakuta watu wa Ninawaa wapo hai, salama salimini, jambo lililomkasirisha Nabii Yunus. Na kwa desturi ya mji wa Ninawaa, malipo ya mtu muongo ni kuuwawa. Hivyo, Nabii Yunus, haraka, akawatoroka kwa jamaa zake kwa kuhofia kuuwawa. Wajibu wake Yunus ulikuwa ni kuridhia maamuzi ya Mola wake Mlezi na kukubali matokeo yake. Mja hana ruhusa ya kughadhibika kwa uamuzi wa Allah. Na ilikuwa haitakikani kwa Yunus kuondoka bila ya maelekezo ya Mola wake. Kwa kuzingatia hilo, ndiyo maana Allah amemkataza Mtume wetu Muhammad (rehema na amani ziwe juu yake) asiwe kama Yunus aliyemezwa na samaki katika mkasa ambao Allah aliyetukuka a m e t u h a b a r i s h a ndani ya Qur’an pale aliposema: ”Basi ingojee hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama mmezwa na samaki” (Qur’an, 68: 48). N a b i i Yu n u s amezwa na samaki baharini Kukataa kuaSEIF RUGA Visa Vya Mitume 1 sehemu ya Katika mji mmoja ulioitwa (Ninawaa), aliishi Nabii Mtukufu Yunus (amani iwe juu yake). Allah alimtuma Yunus kwa watu wa mji ule ambao waliishi katika mazingira ya ujinga na ushirikina kwa muda mrefu. Kisa cha Nabii Yunus aliyemezwa na samaki mini kwa jamaa zake kulimfanya Yunus (amani iwe juu yake) aghadhibike na kuamua kupanda jahazi baharini, lakini jahazi hilo likakumbwa na mtikisiko wa bahari na kuyumba kwa kuzidiwa uzito hadi wasafiri waliomo ndani yake kukaribia kughariki. Kutokana na hali hiyo, wasafiri wakashauri ipigwe kura, na ambaye kura itamwangukia basi ndiye mwenye nuksi na watamtumbukiza baharini ili wapate wepesi katika safari yao. Kwa mara ya kwanza walipopiga kura ilimwangukia Nabii wa Allah Yunus (amani iwe juu yake). Mara ya pili ikamwangukia tena Yunus. Hivyo, akataka kuvua nguo zake na kujitupa baharini mwenyewe lakini wasafiri wenzake wakamkatalia kufanya hivyo Kisha wakarudia tena kupiga kura mara ya tatu, na kwa mara nyingine kura ikamwangukia Yunus. Na hii iliyokea kwa sababu kuna jambo kubwa Allah alitaka litokee kwa Nabii Yunus. Allah aliyetukuka anasema: “Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume. Alipokimbia katika jahazi lililosheheni. Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walioshindwa. Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa” (Qur’an, 37: 139- 142). Yunus alitumbukizwa katika bahari, na Allah aliyetukuka akamwamuru samaki mkubwa sana wa bahari ya kijani ammeze Nabii Yunus. Vilevile, Allah aliyetukuka alimwamuru samaki huyo asimtafune na wala asivunje mifupa yake. ”Huyu Yunus si riziki yako.” Hivyo, akammeza na kuzunguka naye bahari zote. “Wakasema: Yunus alipothibiti katika tumbo la samaki alidhani ya kuwa amekufa, akatikisa viungo vyake vikatikisika, ghafla akajikuta yu hai. Hivyo akamnyenyekea Mola wake kwa kusujudu na kusema: ‘Ewe Mola wangu, ewe Mola wangu nimekujaalia msikiti katika sehemu ambayo hajawahi kukuabudu wewe yeyote’” (Taz: Kisasaul Anbiyaai uk 329). Ghafla, Nabii Yunus (amani iwe juu yake) akastushwa kwa kujikuta yupo katika viza vitatu, kiza cha usiku, kiza cha kina cha bahari na kiza cha ndani ya tumbo la samaki. Hapa Yunus akahisi kosa lake na kukubali yakuwa amefanya kosa, pale alipotoka katika mji wa Ninawaa bila ya idhini ya Allah aliyetukuka. Hivyo, ikawa anaswali na kuleta tasbihi na kumtaka msamaha Allah aliyetukuka akiwa katika tumbo la samaki. Uwezekano wa Yunus kubaki katika tumbo la samaki hadi Siku ya Kiyama ulikuwepo, lakini kulikuwa na jambo moja tu lilimuokoa kutoka katika adhabu hii chungu, nalo ni kumsabihi, na kumdhukuru Allah pamoja na kuleta dua. Allah anasema: ”Na ingeli kuwa hakuwa katika wan a o m t a k a s a Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka angelikaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa“ (Qur’an, 37: 143-144). Itaendelea inshaallah

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close