1. Tujikumbushe

Waislamu watakiwa kuwa makini na maudhui ya vyombo vya habari vya Magharib

Waislam nchini waombwa kuwa makini na maudhui ya vyombo vingi vya habari vya nchi za Magharibi, ambayo mara nyingi yanakuwa na taswira hasi kwa Waislamu na Uislamu.

Katika mazungumzo yake na waumini wa msikiti wa Alhidaya islamiya Chanika jijini Dar es Salaam, Katibu wa Baraza kuu la Jumuiya na taasisi za Kiislamu Wilaya ya Ilala, Sheikh Abdurahaman Salehe amesema Waislamu hawana budi kufuatilia zaidi maudhui ya vyombo vyao vya habari vya Kiislamu ambavyo hutoa habari sahihi kuhusu Uislamu na kuondoa propaganda za vyombo visivyo vya Kiislamu.


Sheikh Saleh aliwahimiza Waislamu waepuke kufarakana na badala yake washikamane katika masuala mbalimbali ili kuleta tija katika maendeleo ya Waislamu na Uislamu. Aidha aliwataka kushikamana na Qur’an na Sunna za Mtume Muhammad katika matendo yao mbalimbali huku akibainisha kuwa Uislamu haujaacha kitu katika maisha ya binadamu hapa duniani

Vyombo hivi vya Kiislamu ni muhimu sana tukavipa kipaumbele, maana ndivyo vinavyotusaidia kujua upande wa pili wa habari ambao haukuzungumzwa na vyombo vingine visivyo vya Kiislamu, lengo ni kufichua propaganda chafu dhidi ya Uislamu na Waislamu,” alisema Sheikh Saleh. Sheikh alisema kwamba licha ya vyombo hivyo kuwa vichache ila vina uwezo mkubwa wa kukabili propaganda chafu dhidi ya Waislamu na Uislamu na kuhimiza Waislamu wazidi kuviunga mkono ili vizidi kutoa habari zilizo na mrengo wa Kiislamu.

Wakati huo huo Sheikh Saleh aliwahimiza Waislamu waepuke kufarakana na badala yake washikamane katika masuala mbalimbali ili kuleta tija katika maendeleo ya Waislamu na Uislamu. Aidha aliwataka kushikamana na Qur’an na Sunna za Mtume Muhammad katika matendo yao mbalimbali huku akibainisha kuwa Uislamu haujaacha kitu katika maisha ya binadamu hapa duniani.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close