1. Tujikumbushe

Uelewa Sahihi wa Kuagiza Mema, Kukataza Mabaya

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka amewatuma Mitume na Manabii kufanya kazi ya da’awah ikiwemo kuwabashiria watu, kuwaonya na kuwaongoza kwenye njia iliyonyooka. Aliyehitimisha kazi hiyo si mwingine bali Mtume wetu Muhammad (rehema za Allah na amani zimshukie).

Miongoni mwa malengo mahsusi ya ujumbe wa Mtume Muhammad (rehema za Allah na amani zimshukie) ni kumrekebisha mwanadamu kitabia. Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) amesema:

“Kwa hakika nimetumwa kwa lengo la kukamilisha tabia njema.” [Muwatta].

Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) alitumia mbinu za kipekee kuwaingiza watu katika imani ya Mwenyezi Mungu mmoja na kuwafundisha tabia njema.

Mtume alitumia mbinu hizo akielewa vema changamoto ambazo wenzake walikumbana nazo, kama zilivyotajwa katika Qur’an Tukufu:

“Basi ndiyo hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema, ‘Huyu ni mchawi au mwendawazimu.’” [Qur’an, 51:52].

Mbinu alizotumia Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) zilitokana na tabia yake ya upole na huruma, na kwa kutumia mbinu hizo aliweza kuwavuta wengi na kuwakinaisha wajiunge na dini. Mbinu hizo ni pamoja na mawaidha wema, subira, ulaini na utulivu. Alitumia mbinu hizi kukabiliana na watu wa aina tofauti ikewemo wale wenye tabia mbaya na misimamo migumu.

Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) aliweza kuzigeuza na kuokoa nyoyo za watu hao kutoka katika giza la ujahili na ubedui kwenda kwenye nuru ya imani. Watu hao walibadilishwa wakawa sababu ya kuimarisha dini badala ya kuwa maadui wake.

Qur’an Tukufu inatutanabaisha kufuata mbinu hiyo ya Mtume katika harakati za ulinganiaji, Mwenyezi Mungu Aliyetukuka amesema:

“Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walio ongoka.” [Qur’an, 16: 125].

Pia Mwenyezi Mungu Aliyetukuka anasema: “Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo umekuwa laini kwao. Na lau ungelikuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfi ra, nashauriana nao katika mambo. Na ukishakata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.” [Qur’an, 3: 159].

Mwenyezi Mungu katika aya hizo tulizozinukuu na nyinginezo kadhaa wa kadhaa amembainishia Mtume wake (rehema za Allah na amani zimshukie) njia bora na mbinu muafaka za kufuata katika shughuli zake za da’awah. Ni muhimu walinganiaji katika njia ya Mwenyezi Mungu, hasa wa zama hizi, kufuata mbinu hizo.

Katika zama za kisasa, kuna mbinu nyingi zisizoafi kiana na msingi wa dini ikiwemo kuwatishia wanaolinganiwa na kuwahofi sha. Mbinu za aina hiyo zinapalekea watu kuwachukia walinganiaji wa aina hiyo. Walinganiaji hawa wanaotegemea maneno makali hawafai kuongoza shghuli za ulinganiaji katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka amebainisha misingi ya shughuli za da’awah na nguzo za ulinganiaji aliposema:

“Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi aliyeipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.” [16: 125].

Anasema tena Mwenyezi Mungu: “Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni, ‘Tumeyaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake.’” [Qur’an, 29: 46].

Aidha, Mwenyezi Mungu ameelezea namna ya kuwalingania watu wa dini nyingine katika kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja ambaye hana mshiriki: “Sema, ‘Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi. Ya kwamba, tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa miungu walezi badala ya Mwenyezi Mungu.’ Na wakigeuka basi semeni, ‘Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.

“Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili hazikuteremshwa ila baada yake? Basi hamzingatii? Angalieni! Nyinyi mlibishana katika yale mliyoyajua. Mbona sasa mnabishana katika yale msiyo yajua?Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye, na nyinyi hamjui. Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina” [3: 64-67].

Akibainisha namna ya kujadiliana na kuwalingania washirikina, Mwenyezi Mungu Aliyetukuka anasema: “ Sema: Ni nani anayekuruzukuni kutoka Mbinguni na kwenye Ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uwongofu au upotofu ulio wazi. Sema, Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya, wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda nyinyi. Sema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki; na Yeye ndiye Hakimu Mwenye kujua.

Sema: Nionyesheni mlio waunganisha naye kuwa washirika. Hasha! Bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” [34: 24-27].

Kwa hiyo, ulinganiaji katika Uislamu haukuwa kwa nguvu wala kulazimisho, bali kwa hekima na mawaidha mema yanayovuta akili na miyoyo kwenye njia ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Kulingania hakuhitaji kuwalazimisha watu, bali kufuata njia na mbinu ambazo Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na Mtume wake (rehema za Allah na amani zimshukie) wametubainishia.

Mwenyezi Mungu amewasifu wale ambao wanawalingania watu kwa hikima. Watu hao ndiyo wametimiza sifa, misingi, malengo na masharti ya kazi hiyo adhimu:

“Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema, ‘Hakika mimi ni katika Waislamu?’ Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafi ki jamaa wa kukuonea uchungu.” [Qur’an, 41: 33-34].

Walinganiaji wanapokuwa na sifa na tabia hizo, huchangia sana mafanikio ya harakati za da’awah Mwenyezi Mungu anasema:

“Sema, ‘Hii ndiyo Njia yangu – ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua – mimi na wanaonifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina,’” [12: 108].

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka amebainisha kuwa upole na ulaini katika da’awah ndizo sifa zinazotakiwa na ndiyo maana akamwambia Mtume wake (rehema za Allah na amani zimshukie):

“Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfi ra, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaomtegemea.” [3:]

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close