1. Tujikumbushe

Sheikh: Ni hatari Muislamu kupuuza elimu ya dini

Licha ya kufanya kazi tukufu ya kuilea jamii kiroho na kimaadili, imefahamika kuwa walimu wa madrasa ni kundi la watumishi wa dini wanaoishi maisha magumu na wanakabiliana na changamoto lukuki.


“Ni hatari kubwa mno Muislamu
wa zama hizi kuipuuza elimu ya
dini…tumesahau kuwa walimu wa
madrasa ndiyo haswa wanaopas-
wa kuthaminiwa,”


Sheikh
Semkuya

Amir wa Shura ya Maimamu katika Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, Sheikh Hassan Semkuya ameyasema hayo hivi karibuni wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hii. Katika maelezo yake, Sheikh Semkuya alisema kuwa kwa kiasi kikubwa jamii ya Waislamu ime wapuuza walimu wa madrasa kiasi cha kutowaheshimu na kuwapa hadhi inayostahiki.

Sheikh Semkuya aliongeza kuwa wazazi wengi wamekuwa wepesi kulipia upande wa masomo ya mazingira kwa kuwa wanaamini elimu hiyo itampa mtoto ajira na anaweza hata kuwa kiongozi serikalini.

Ni hatari kubwa mno Muislamu wa zama hizi kuipuuza elimu ya dini…tumesahau kuwa walimu wa madrasa ndiyo haswa wanaopaswa kuthaminiwa,” alisema Sheikh Semkuya na kuongeza: “Katika viwango vya mishahara, walimu wengi wa madrasa wamekuwa wakilipwa kiduchu, hadi kufikia elfu 50 kwa mwezi ama chini ya hapo. Hali hii ndiyo inayowafanya baadhi yao kutegemea zaidi sadaka za kila mwezi, ambazo hata hivyo hazikidhi mahitaji yao.

Katika hatua nyingine, Amir huyo wa Shura ya Maimamu wilayani Ilala aliwataka wazazi na Waislamu wengine kuacha tabia ya kuwathamani walimu wa madrasa wakati wa kuwaombea maiti tu au katika mambo yahusuyo ndoa.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close