1. Tujikumbushe

Kanuni za Allah Katika Kufuata Uongofu na Upotovu

Kwa hakika matukio yanayojiri duniani hayatokei kwa bahati mbaya, bali kwa kanuni za Allah, Muumba wa mbingu, dunia na vilivyomo ndani yake. Mwanadamu ni sehemu ya viumbe wa Allah hivyo hubadilika kutoka hali moja hadi nyingine kulingana na umbile lake. Kanuni hii inahusiana na hali ya wema, uovu, nguvu au udhaifu aliokuwa nao mtu. Kwa kiasi kikubwa kanuni hii inatokana na mawazo hasi ya mtu, namna ya kufikiri na namna ya kutenda. Kanuni hii hujulikana kama ‘Mwenenedo wa Kiuungu katika kuuendesha ulimwengu.’ Mwanadamu anatakiwa azingatie kanuni hii na kuifanyia kazi katika maisha yake ya kila siku. Allah Aliyetukuka amebainisha kanuni za uendeshaji wa ulimwengu kupitia Kitabu chake Kitukufu (Qur’an) na katika maisha yetu ya kila siku. Katika makala hii, tutazungumzia suala la kuongoka na kupotoka kwa mwanadamu kama mojawapo ya kanuni za Allah katika uendashaji wa ulimwengu.

Anayetaka uongofu anatakiwa azingatie mambo kumi muhimu.

Kwanza: Amtambue Allah

Aliyetukuka Anayetaka uongofu ni lazima amtambue Allah Aliyetukuka, majina yake na sifa zake. Kumtambua Allah ni kumtii Yeye na kumuabudu bila ya kumshirikisha na chochote. Allah anasema:

“Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu…” [Qur’an, 47:19].

Pili: Kufungamana na Allah kila wakati

Kufungamana na Allah maana yake ni kuitakidi uwepo wake, kumsadikisha moyoni na kutekeleza yote aliyoyaamrisha na kuacha makatazo yake. Kufungamana na Allah kunazidi kwa kumtii Yeye na kunapungua kwa kufanya maasi. Allah anasema: “Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake.” [Qur’an, 64:11]. Pia Allah amesema: “Hakika wao (vijana wa pangoni) wlaikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao. Nasi tukawazidisha uongofu.” [Qur’an, 18:13].

“Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake.” [Qur’an, 64:11]. Pia Allah amesema: “Hakika wao (vijana wa pangoni) wlaikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao. Nasi tukawazidisha uongofu.” [Qur’an, 18:13].

Tatu: Kufuata amri za Allah na kuepuka makatazo yake

Allah anasema: “Na lau kama wangefanya waliyowaidhiwa ingekuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi. Na hapo tungewapa malipo makubwa kutoka kwetu. Na tungewaongoza katika njia iliyonyooka.” [Qur’an, 4:66–68].

Nne: Kuomba uongofu kwa Allah

Uongofu ni neno linalojumuisha mambo yote yanayohitajia uongofu katika mambo ya dunia na Akhera. Mwenye kuruzukiwa uongofu, uchamungu na utajiri wa moyo hupata furaha mbili. Kwanza, anapata kila linalotakiwa na anaokoka na kila linaloogopwa. Na haya ndio maisha mema.

Sita: Kupambana na Iblis Uislamu unawataka waumini kupambana na maadui wakubwa wawili ambao ni Iblis (shetani aliyelaaniwa) pamoja na nafsi. Muislamu anatakiwa apambane na nafsi yake na kuielekeza katika njia za kheri. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema.” [Qur’an, 29:69].

Saba: Kuchagua rafiki mwema

Haifai Muislamu kusuhubiana na marafiki waovu kwa sababu wao ni hatari zaidi kuliko ugonjwa wa corona. Mwenyezi Mungu anasema:

“Marafiki vipenzi Siku hiyo (ya Kiyama) watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wachamungu.” [Qur’an, 43:67].

Nane: Kushikamana na Qur’an

Tukufu Mwenye kushikamana na Qur’an Tukufu kwa kuisoma, kuihifadhi, kuizingatia na kuifahamu, moyo wake hupata utulivu na amani.

Tisa: Kudumisha dhikri

Dhikri ni kinga na ulinzi tosha dhidi ya vitimbi vya Iblis na watu wabaya. Kupitia dhikri nafsi hupata utulivu na hivyo kujiweka mbali na maovu. Allah Aliyetukuka anasema:

“Hakika Waumini ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa hofu…” [Qur’an, 8:2]. Aidha Allah amesema: “Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumdhukuru Allah. Kwa kumdhukuru Allah nyoyo hutulia!” [Qur’an, 13:28].

Na katika Hadith iliyosimuliwa na Abu Musa Al–Ash’ariy (Allah amridhie), Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) amesema:

“Mfano wa mtu anayemdhukuru Allah na asiyemdhukuru ni kama mtu aliye hai na maiti.” [Bukhari].

Kumi: Kukikumbuka kifo

Mwenye kutaka uongofu ni lazima amhofu Mungu, aache maovu na kukikumbuka kifo mara kwa mara. Kuna faida nyingi za kukikumbuka kifo, na miongoni mwa hizo ni:

Mosi: Mwenye kukitafakari na kukikumbuka kifo, daima hujibidiisha kufanya matendo mema na kuridhika na kichache.

Pili: Mwenye kukikumbuka kifo hufanya toba ya kweli kwani hukumbuka madhambi yake na kumuomba msamaha Allah kwa sababu anajua siku na muda wowote anaweza kuiaga dunia. Na katika sifa za waumini wa kweli ni kujiepusha na mambo machafu, maovu na yenye kutia shaka (Shubuhaat). Kwa kufanya hivyo, utaisalimisha nafsi yako na hatari ya kufanya dhambi.

Sababu za upotovu

Kama ilivyo kwa uongofu, pia upotevu una sababu zake ikiwamo kutotafakari Ukubwa na Utukufu wa Allah, kukithirisha maasi, kufuata matamanio, kushirikiana na waovu na kumtii shetani. Ikiwa tunahitaji uongofu ni lazima tuepuke sababu zinazopelekea katika upotovu, lakini pia tushikamane na Qur’an na mafundisho ya Mtume.

Uongofu ni tunu na fadhila itokayo kwa Allah ‘Azza Wajallah’. Allah anasema:

“Hata ukiwa na pupa ya kutaka kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu hamuongoi yule anayeshikilia kupotea. Wala hawatapata wa kuwanusuru.” [Qur’an, 16:37].

Uongofu na upotovu unatokana na mwenendo na kanuni zake Allah Aliyetukuka ambazo hazibadiliki. Allah humpoteza anayestahiki upotevu kulingana na kanuni zake. Na yeyote aliyepotezwa na Allah hakuna awezaye kumuongoa.

Allah ndiye aliyeweka nidhamu ya sababu, ndio maana suala la uongofu na upotovu limeegemezwa kwake. Allah hamlazimishi mtu kufuata uongofu au upotovu bali humuacha mtu aende upande autakao kama anavyobainisha:

“Na wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema.” [Qur’an, 29:69].

“Na wale walioongoka anawazidishia uongofu na anawapa uchamungu wao.” [Qur’an, 47:17]. Uongofu wa Allah kwa wanadamu unaegemea katika kuwahurumia w

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close