1. Tujikumbushe

Enyi vijana! Mwenye uwezo na aoe

Kutoka kwa Alqama amehadithia kuwa, siku moja akiwa anatembea na Abdullah bin Masoud, walikutana na Uthman bin Affan. Wawili hao walisimama wakazungumza naye. (Uthman) Akasema:“Ewe Abu AbdirRahman kwanini tusikuoze kijakazi? Huenda akawa anakukumbusha baadhi ya yale yaliyokupita.”

Abu AbdirRahman (Ibnu Masoud) akasema: “Ama ikiwa utasema hivyo, kwa hakika Mjumbe wa Allah (rehema za Allah na amani zimshukie) alishatuambia, ‘Enyi kundi la vijana! Mwenye uwezo miongoni mwenu wa kuoa basi na aoe, kwani ndoa husaidia kuinamisha macho, na kuhifadhi utupu, na yule asiyeweza basi ni juu yake kufunga kwani funga ni kinga kwake yeye (kwa kupunguza matamanio ya kimwili).’” [Bukhari na Muslim].

Mafunzo ya tukio

Tukio hili linatupa mafundisho kadhaa. Kwanza, tunajifunza upendo uliokuwepo baina ya Wema Waliotangulia na namna walivyokuwa wakiusiana na kusaidiana katika mazuri yaliyoweza kuwapa nguvu ya kutekeleza majukumu yao na kumuabudu Allah ipasavyo.

Tunamuona Uthman (Allah amridhie) akimuhamasisha Ibn Masoud kuoa. Tunaona pia Uthman akiahidi atalisimamia jambo hilo la kumuozesha, kama Ibn Masoud atakuwa tayari

Kuhamasishana katika jambo la ndoa

Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) amewaachia usia muhimu sana vijana wa umma huu ambao utawakinga na kuwasaidia kuepuka mambo mengi iwapo watashikamana nao. Huu ni usia wa kuoa, ambao kwa bahati mbaya vijana wengi, na hata wazazi na walezi, wameupuuzia.

Suala la ndoa limezingirwa na utamaduni na desturi za miji ambazo zimelifanya kuwa gumu na zito kiasi cha kuwafanya baadhi ya vijana waogope, walifumbie macho na kueneza ufisadi katika ardhi kwa kufanya machafu ya aina mbalimbali.

Ndoa ni kinga

Vijana watambue kuwa ndoa ndiyo silaha nyepesi na rahisi itakayowasaidia kupambana na matamanio ambayo ni sehemu ya maumbile ya kibinadamu. Ni vema kijana akaharakia kuoa kadiri atakavyoweza kwani hakuna jambo bora la kumuwezesha kuepuka maasi katika zama hizi kama ndoa.

Kijana atakapoona chochote kikaamsha hisia za matamanio katika nafsi yake, ataelekea kwa mkewe na kupooza matamanio hayo, lakini kama hana pakutuliza matamanio katika zama hizi zilizojaa fitna za aina mbalimbali, atayumba na kuangukia katika maasi.

Zama hizi, mazingira yamebadilika. Nyenzo za maasi zimekuwa nyingi. Unapotazama mara nyingi, macho yanaangukia katika haramu, masikio nayo yatasikia haramu. Hata ukiwa peke yako, moyo unagubikwa na fikra za mambo ya haramu na dhambi.

Vijana wengi wamekuwa wanaamsha hisia za matamanio lakini baada ya hapo hawawezi kuzipooza au kuzizuia. Hilo limesababishwa na kupuuza usia huu wa Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie).

Matamanio ya mwili hayapigwi vita bali yanatakiwa yabakie kwa ajili ya manufaa ya umma wa kiislamu, yawekwe mahala panapostahiki ili vipatikane vizazi vinavyomtambua Allah na kuitetea dini yake kwa kufuata mwenendo wa Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie).

Uwepo wa matamanio na fitna za aina mbalimbali ni sehemu ya maisha ya Muumini ili kudhihirisha umadhubuti na uimara wa imani yake.

Kujibidisha katika funga za Sunna

Watu wengi, hususan vijana wanajitahidi kufunga swaumu ya Ramadhan kwa sababu ni funga ya lazima (faradhi) lakini wanapuuza funga za Sunna. Tuelewe kuwa, pamoja na thawabu na fadhila za funga za sunna, pia ipo faida ya kudhoofisha, kuyadhibiti na kuyabana matamanio ya nafsi na mapito ya shetani. Hivyo basi, ni muhimu sana kujibidisha kufunga sunna ili kupata malipo bora kwa Allah na kujizuia na machafu.

Weka akiba ya afya yako kwa kujizuia na haramu ili uzidi kuimarika na kusalimika na maradhi au udhaifu wa mwili unaotokana na kuyaendea maovu. Harakisha katika kuyaendea maisha ya ndoa kwani faida zake ni nyingi na manuf a a yake yanarejea kwako kwa jamii na kwa umma kiujumla.

Kadhalika, zuia macho yasitazame haramu na masikio yasisikilize haramu kwani hiyo ni sababu ya kukufanya usiyaendee. Haramu inayokataz- w a kutazamwa au kusikiliza ni pamoja na miziki, ambayo sehemu kubwa ya maudhui yake inahamasisha mapenzi na uhusiano usiokuwa wa kisheria.

Vijana wengi wameingia katika makundi haya ya wapenda miziki na kuwa katika michanganyiko mibaya ya wanaume na wanawake. Lakini pia wapo vijana wengi wakiwamo Waislamu ambao hujihusisha na kuimba ama kucheza muziki kwa ajili ya kujipatia kipato, jambo ambalo linahatarisha usalama wa imani yao na matendo yao.

Ujana ni mtihani

Ujana ni ngazi miongoni mwa ngazi anazopitia mwanadamu katika maisha yake. Katika ujana, mtu huwa na mipango mingi na matumaini makubwa, hadi hughafilika.

Kikwazo kingine kikubwa kwa vijana ni kutochukua hatua za haraka na za papo hapo katika muda muafaka za kubadilisha mwelekeo wa maisha yao, na badala yake husema ‘Nitafanya.’

Wengi wanasema ‘nitaoa,’ ‘nitatubu,’ ‘nitaswali’, ‘hakuna
neno nitabadilika,’ kauli ambazo ni bahari isiyokuwa na mwisho. Waliozama
katika bahari hii wamekuwa wakisema ‘nitafanya’ mpaka kifo kikawafikia.
Hawakupata muda wa kufanya. 

Walipofikisha miaka 30 walisema nitatubu nikifikisha 40, walipofikia 40 wakasema ikifika 50. Walisahau kuwa, kila kukicha kifo kilikuwa kinawakaribia na makaburi yalikuwa yakiwangoja, hatimaye wakaingia makaburini na huku wakiwa na yale matumaini ya ‘nitafanya.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close