1. Tujikumbushe

China ‘kuwavua’ raia wake Uislamu wao

Ripoti za Vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni vimefichua kambi maalumu nchini China ambako Waislamu wa jamii ya Uyghur nchini humo wanashikiliwa, lengo likiwa ni kuwabadili itikadi zao za kidini kwa kuwapa mafundisho mapya.

Shirika la habari la BBC hivi karibuni lilifanikiwa kunasa baadhi ya majengo hayo ambayo yako chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya usalama nchini humo. Duru mbalimbali zinaarifa kuwa mamlaka za Beijing zinawashikilia Waislamu hao takribani milioni moja katika jimbo la Xinjiang, kwa kuwapa mafundisho mapya yanayoendana na taifa hilo ili, kile ambacho serikali hiyo inadai ‘waondokane na misimamo mikali’.

Aidha, Waislamu hao inadaiwa wamekuwa wakilazimishwa kula kiapo cha utii kwa Rais Xi Jinping kama zinavyoonesha ripoti za mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Amnesty International and Human Rights Watch zilizowasilisha mbele ya hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa Agosti mwaka huu na kunakiliwa na vyombo kadhaa vya habari.

Nao Umoja wa Wa Uyghur Duniani (WUC) katika ripoti yake inasema kuwa wafungwa hao wa Kiislamu wanalizimishwa kuimba nyimbo za chama cha Kikomunisti. Aidha, ripoti hiyo inasema kuwa Waislamu hao hawapewi chakula cha kutosha na kumekuwepo na mateso ndani ya kambi hizo.

Kwa upande wake China inadai kuwa haiwashikilii Waislamu hao badala yake inachokifanya ni jitihada za kupambana na ugaidi na misimamo mikali. Runinga ya Al Jazeera imewahi kuripoti kuwa wazazi wengi wa Uyghur wanalalamika kutowaona watoto wao kwa miaka mingi sasa.

Mtandao wa habari wa Huffington Post hapo mwaka jana uliarifiwa kuwa China ina Waislamu takribani milioni 23 kati ya raia wa nchi hiyo takribani bilioni moja. China ni Taifa linalofuata itikadi za Kikomunisti zilizoasisiwa na Karl Marx, itikadi ambazo zinapinga imani za kidini kama za Uislamu na Ukristo. Kwa kutumia itikadi hizo na visingizio vingine kama kupambana na ugaidi, watawala wa China wamekuwa wakiweka sheria kali dhidi ya Waislamu.

Jimbo la Xinjiang, ambalo lina Waislamu wengi wa kabila la Uyghur ndio unatajwa kutawaliwa na chuki kali dhidi ya Waislamu. Pia iliwahi kuripotiwa na Mashirika ya habari kuwa Waislamu katika mji huo wa Xinjiang walizuiwa kuwapa watoto wao majina ya Mohammed na majina mengine ya Kiislamu.

Pia gazeti la The Independent la Machi 30, 2017 liliarifu kuwa Waislamu nchini humo wamepigwa marufuku kuvaa ushungi, burqa na kufuga ndevu nyingi. Na hapo mwaka 2015 kituo cha habari cha International Business Times kiliarifu kuwa, maduka na migawaha ya Kiislamu nchini humo iliamuriwa kuuza pombe, sigara ili kudhoofisha nguvu za Waislamu wengi katika jimbo la Xinjiang.

Nalo gazeti la The Washington Post la nchini Marekani hapo mwaka 2015 liliandika kuwa Waislamu jimbo la Xinjiang walizuiliwa kuhudhuria misikitini au kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

 

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close