1. Tujikumbushe

Al – Azhar: Utulivu wa familia ni kinga kwa mtoto

Imeelezwa kuwa utulivu ndani ya familia ni kinga muhimu kwa watoto dhidi ya uasi wa kifikra na tabia zisizofaa katika jamii. Sheikh Ashraf Shawadify, Mwalimu wa kituo cha Kiislamu cha Kimisri (Azhar Sharif), Tawi la Tanzania amesema hayo katika kongamano la kidini lililofanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya chuo hicho, eneo la Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Akiwasilisha mada, ‘Umuhimu wa utulivu wa familia katika kuwakinga watoto na uasi wa kifikra na tabia zisizofaa,’ Sheikh Ashraf alisema kuwa, familia kama taasisi ya kijamii ina umuhimu katika kuleta amani na utulivu katika jamii.

Kwa upande wake, Rais wa Taasisi ya Al-hikma Foundation ya jijini Dar es Salaam, Sheikh AbdulQadir al-Ahdal aliwataka vijana kuwatendea wema wazazi wao ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu, kuwatunza kwa kuwapatia mahitaji yao. Sheikh AbdulQadir alionekana kukerwa na vitendo vya baadhi ya watu ambao kwa makusudi huamua kuwapeleka wazazi wao kwenye nyumba maalum za kulelewa vikongwe na kwamba mwenye kuyafanya hayo atapata adhabu.

Haifai, na pia ni haramu kuwatekeleza wazazi au kuwavunjia heshima na kuonya kuwa hayo ni mambo ambayo Allah ameyaharamisha,” alisema Sheikh AbdulQadir.

Akitoa neno la shukrani, Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu cha Kimisri (Azhar Sharif), Sheikh Mohamed Hassan Attia, alisema amefurahishwa na mada zilizotolewa katika kongamano hilo na amewashukuru washiriki wote.

Kongamano hilo pia, lilihudhuriwa  na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, Sheikh Mohamed Mahmoud Abdelfattah, Mwalimu wa Azhar Sharif Tawi la Tanzania na Sheikh Hilary Shaweji maarufu Kipozeo.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close