5. Ramadhan

Ushauri wa kuifanya Ramadhani yako iwe yenye mafanikio

Imetafsiriwa na Mariam Mzingi

  1. Tia nia, jitahidi na omba dua kwa wingi, Allah (swt) akujaalie Ramadhan yenye mafanikio.
  2. Panga siku yako, kila siku katika mwezi wa Ramadhani. Jitahidi kufanya hivyo usiku kabla siku haijaanza. Chagua mambo matatu muhimu unayotaka kuyakamilisha siku ijayo na uyaandike katika mipango yako.
  3. Usikose daku (suhur) hata siku moja. Amka saa moja kabla ya Alfajiri na ule chakula cha kutosha na kilicho bora.
  4. Anza kufanya mambo yaliyo muhimu zaidi asubuhi na mapema, baada ya swala ya alfajiri na ujitahidi kumaliza jambo moja au mawili.
  5. Jitahidi kulala kidogo mchana kabla au baada ya dhuhr, ila sio zaidi ya dakika 20.
  6. Fanya mipango yako kwa kuzingatia wakati wa swala, na si kinyume chake.
  7. Tenga angalau saa moja kwa ajili ya kusoma Qur’an kila siku.
  8. Futuru kwa tende na maziwa au tende na maji, nenda kaswali kisha rudi na ule mlo mwepesi.
  9. Toa sadaka kwa wingi. Jihusishe katika kuandaa futari, kujitolea na kuwasaidia mayatima n.k. Pata thawabu kwa kuwatumikie wengine
  10. Usiache fursa ya kufanya da’wah! Mtu akikuuliza kwanini hauli, wape maelezo mazuri kuhusu Ramadhani na Uislamu.

Ili kusoma kwa kingereza, bonyeza hapa

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close