6. Kutoka Katika Quran na Sunnah

Viungo vitakaposemeshwa Siku ya Kiyama

Imepokewa na Jabir bin Abdillah (Allah amridhie) kwamba, wahamiaji wa Habasha (Ethiopia) waliporejea Makka, Mtume (rehema za Allah na amani imfikie) alikuwa amekaa na Maswahaba zake (Allah awaridhie). Mtume aliwauliza: “Je, hamsimulii jambo la kushangaza mliloliona katika ardhi ya Habasha?” Baadhi yao wakasema: “Ewe Mjumbe wa Allah! Siku moja tulikuwa tumekaa sehemu, akapita ajuza mmoja miongoni mwa watawa wa Kinasara huku akiwa amebeba birika la maji (lililotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi).”

kijana mmoja, ambaye baadaye alimuwekea mkono begani na kumsukuma kwa nguvu. Bibi kizee huyo aliangukia magoti na kupelekea birika lake kuvunjika.” Baada ya kunyanyuka, alimgeukia kijana aliyemsukuma na kumwambia:

“Mtakuja kujua enyi wenye hiyana pindi Allah atakapoweka kiti chake (kwa ajili ya kutoa hukumu). Allah atawakusanya watu wa mwanzo na wa mwisho katika siku ambayo mikono na miguu yao itasema mambo yote iliyoyatenda. Hapo ndipo utakapojua nani ana hadhi zaidi mbele ya Allah kati yangu mimi na wewe.”

Mtume akawaambia Maswahaba: “Amesema kweli (Ajuza). Vipi Allah atawatukuza watu ilihali haki ya mnyonge haichukuliwi kutoka kwa mwenye nguvu?” [Ibnu Majah].

Mafunzo ya tukio

Hijra ya kwanza kwenda Habasha (Ethiopia)

Makafiri wa Kikureish waliwatesa na kuwadhulumu waumini. Wanazuoni wa Sira (Historia ya Mtume) wameeleza kuwa makafiri wa Kikureish walithubutu kumpiga Mtume wa Allah (rehema za Allah na amani zimshukie) mara kadhaa katika mji wa Makka.

Mateso yalipozidi, Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) aliwaamuru Waislamu wahamie Habasha (Ethiopia) ili waishi kwa amani, utulivu na usalama. Habasha ndiyo ilikuwa nchi ya kwanza kutembelewa na Maswahaba wa Mtume (Allah awaridhie).

Maswahaba walipofika Habasha walimuona mfalme Najash na kumuomba kukaa nchini mwake, naye akawakubalia kwa moyo mkunjufu.

Kuna mambo mengi ambayo Maswahaba waliyaona huko Habasha (Ethiopia). Hivyo, Mtume alitaka kusikia baadhi ya mambo waliyoyashuhudia huko Habasha. Maswahaba wakamsimulia Mtume kisa cha ajuza ambaye alikuwa mtawa wa kinasara katika mji wa Habasha.

Ukaribu wa kiongozi kwa raia wake

Tukio hili linatupa mafundisho kadhaa. Kwanza, tunajifunza upendo wa Mtume (rehema za Allah na amani imshukie) kwa watu na namna alivyokuwa akizungumza nao juu ya masuala ya kidini na yale yanayohusiana na maisha yao binafsi.

Mtume hakuwa mbaguzi, mwenye makuu na wala hakujikweza, bali alikuwa rafiki wa kila mtu. Allah ‘Azza Wajallah’ameizungumzia tabia hii ya Mtume kwa kusema:

“Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo umekuwa laini kwao. bila ya shaka wangeli kukimbia. Na lau ungekuwa mkali na mwenye moyo mgumu, bila shaka wangekukimbia. Basi wasame – he na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo.” [Qur’an, 3:159].

Athari za kukosa malezi mazuri

Ujana ni ngazi miongoni mwa ngazi anazopitia mwanadamu katika maisha yake. Kijana huhisi kuwa ana nguvu zinazomuwezesha kufanya jambo lolote atakalo. Kwa kuzingatia haya, wazazi na walezi wanapaswa kuwa imara katika kusimamia malezi ya watoto na vijana wao na kuwapa maelekezo ya kutosha juu ya kujiepusha na tabia mbaya ambazo zina athari kubwa katika maisha yao binafsi na jamii kwa ujumla.

Katika tukio hili, tumeshuhudia kijana mmoja akimsukuma bibi kizee badala ya kumsaidia. Kijana huyo alikuwa anapenda kumuona bibi yule akipata tabu na matatizo. Tabia hii ya vijana kutowaheshimu wazee siyo kilema wala ugonjwa usioweza kutibika. Ni hulka ambayo kila mtu hana budi kuikomesha ili isiathiri maisha yake. Vijana wanapaswa kuwaheshimu wazee, kuwahuruma na kuwafanyia hisani wakati wote, na wazee pia hawapaswi kuwavunjia heshima vijana.

Kuhukumiwa Siku ya Kiyama

Katika tukio hili, tunajifunza kwamba, Allah ‘Azza Wajallah’atawahukumu waja wake Siku ya Kiyama kulingana na yale waliyoyafanya katika maisha yao ya duniani. Katika mazingira haya magumu, kitakachomfaa mtu na kumpa hadhi na utukufu mbele ya Allah, ni matendo yake mema alilyoyafanya wakati wa uhai wake. Allah ‘Azza Wajallah’anasema: “.

Wanyonge wana haki ya kutetewa

Ili tupate mafanikio katika maisha yetu, ni lazima kila mmoja wetu ahakikishe anachunga na kulinda haki hasa za wanyonge. Uislamu unatuhimiza kuchunga haki za watu wote hasa wanyonge ambao mara nyingi tunawaona wakihangaika mitaani na katika vyombo vya habari kutafuta msaada wa kisheria.

Kuchunga na kulinda haki za wanyonge ni moja ya sababu zinazopelekea mtu kukunjuliwa riziki. Mtume amesema: “Hakika hampati riziki wala nusra isipokuwa kwa sababu ya wanyonge wenu.” [Bukhari]. Kuwatetea wanyonge ni jambo lililotiliwa mkazo katika Uislamu kutokana na ukweli kwamba, kila mtu ni lazima apitie hali ngumu katika maisha yake.

 Qur’an inasema: “Allah ndiye ambaye amekuumbeni kutokana na udhaifu, kisha akajaalia baada ya udhaifu nguvu, kisha akajaalia baada ya nguvu udhaifu na ukongwe. (Allah) anaumba atakacho. Naye ndiye Mjuzi wa yote, Mweza wa yote.” [Qur’an, 30:54].

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa mataifa na makabila (mbalimbali) ili mpate kujuana. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu mbele ya Allah ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Allah ni Mwenye kujua, Mwenye habari.” [Qur’an, 49:13]

Viungo vitasemeshwa mbele ya Allah

Katika yale aliyoyasadikisha Mtume (rehema za Allah na amani imshukie) ni viungo vya mwili kutoa ushahidi wa mambo aliyoyatenda mwanadamu hapa duniani. Mfano mikono itasema:

“Niliiba kadhaa wa kadhaa.” Miguu itasema: “Nilikwenda sehemu za maasi.” Macho yatasema: “Nilitazama machafu.” Na masikio yatasema: “Nilisikiliza nyimbo, au umbea au ghiba (usengenyi).”

 Allah anasema: “Watakapoufikia moto yatawashuhudia masikio yao, na macho yao na ngozi zao kwa waliyokuwa wakiyatenda.” [Qur’an, 41:20]. Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Allah Siku ya Kiyama.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close