6. Kutoka Katika Quran na Sunnah

Sayansi Mamboleo Na Mafunzo Mbalimbali Ambatanishi

SEHEMU YA 13 Mpenzi msomaji, Allah aliyetukuka anasema ndani ya Qur’an Tukufu: “Na hakika Yunus bila shaka ni miongoni mwa Mitume. Alipokimbilia katika merikebu iliyosheheni. Akapiga kura akawa miongoni mwa walioshindwa. Basi samaki mkubwa akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.

“Na lau kama hakuwa mion – goni mwa wenye kumsabbihi Al – lah. Angelibakia tumboni mwake mpaka Siku watakayofufuliwa (viumbe). Basi Tukamtupa kwenye ardhi tupu ufukweni (al – ipomcheua samaki) naye akiwa mgonjwa. Na Tukamuoteshea mti unaotambaa aina ya mung’unya. Na Tukamtuma kwa (watu wake) laki moja au wanaoz – idi. Wakaamini, basi Tuka – wastarehesha kwa muda,” (Qur’an, 37:139-148). Mpenzi msomaji, katika makala kadhaa zilizopita tulizun – gumzia kwa kina na kuakisi juu ya nyuki na asali na hata kufanya vipindi viwili viitwavyo, ‘Akisi ya Mdadisi’ katika vituo vya redio na televisheni vya Imaan. Katika vipindi hivyo tuliangazia kwa mapana aya ya 68 na 69 ya Suratu Annahl (sura ya 16). Katika makala hii tutaanza ku – zungumzia aya ya 146 ya Suratu Asw-Swaffaat (sura ya 37). Kati – ka utangulizi wa makala hii tume – kuja na aya tisa (9) zikizungumzia kisa cha Nabii Yunus ambacho kimetajwa katika sura kadhaa ndani ya Qur’an. Tutakuja kuzi – taja aya hizi pale tutakapokuwa tunazungumzia mafunzo ambat – anishi ya kisa hichi. Ndani ya Aya hizi tisa tulizoan – za nazo katika utangulizi wa makala hii, kuna aya zinazoonye – sha uwezo na miujiza ya Allah pale ambapo mmoja wa Mitume wake, Nabii Yunus alipomezwa na samaki mkubwa aina ya chewa na kukaa tumboni kitambo fulani pasina kutafunwa na kuyeyushwa na vitu vinavyoyeyusha chakula tumboni mwa samaki (digestive enzymes). Wiki iliyopita tulizungumzia kwa kirefu kinywaji kizuri chenye rangi tofauti na am – bacho ni tiba na ponyo ya mara – dhi mengi nacho ni asali, leo tutazungumia ukweli wa Qur’an kisayansi katika moja ya chakula kilichotajwa katika aya ya 146 ya Surat Asw-Swaffaat. Aya yenyewe inazungumzia chakula alichokula Nabii Yunus baada ya kucheuliwa na samaki. Aya mbili; ya nyuma yake na aya hii zinasema hivi: “Basi Tukam – tupa kwenye ardhi tupu ufukweni (alipomcheua samaki) naye akiwa mgonjwa. Na Tukamuoteshea mti unaotambaa aina ya mung’unya.” Mpenzi msomaji, kama ilivyo kawaida, tutaanza kuzungumzia sayansi katika aya kwanza kabla ya kuzungumzia mafunzo mbalimbali ambatanishi. Leo tunazungumzia mmea au mti aina ya ‘Yaqtwiin’ (mung’unya) mti ambao unataambaa. Tunawe – za kujiuliza kwa nini Nabii Yunus alioteshewa mti huu? Je kucheuli – wa kwake kutoka katika tumbo la s a m a k i a k i w a anaumwa kunahusianaje na mti huu? Leo hii elimu na sayansi ya tiba inatueleza kuwa kuna vyakula vya wagonjwa lakini kumbe kimsingi haya ni mambo yaliyokwishata – jwa katika Qur’an ingawa wana – sayansi hawataki kukiri hilo! Mpenzi msomaji, bila shaka un – alijua mung’unya linalopatikana sehemu nyingi hapa nchini kwetu Tanzania hasahasa katika msimu wa mvua. Mung’unya ni miongoni mwa vyakula alivyokuwa akivipenda sana Mtume wetu Muhammad (rehema na amani ya Allah im – shukie). Katika hadithi iliy – osimuliwa na Anas bin Malik (Al – lah amridhie), Khayyaat alimua – lika Mtume akale chakula ali – chomtengenezea. Anas anasema kuwa alienda pamoja na Mtume wa Allah kula naye chakula kile. Chakula alichoandaliwa Mtume ambacho aliletewa ki – likuwa ni mkate uliochanganywa na mchuzi na ndani yake ku – likuwa na mung’unya na mishikaki. Mtume akawa akili – fuata sana mung’unya katika sinia lile. Maana yake ni kuwa alilipen – da kuliko vyakula vile vingine. Anasi anasema baada ya hapo, naye akawa ni mwenye ku – penda sana mung’unya. Mpenzi msomaji ukii – soma aya hii: “Na Tuka – muoteshea mti unao – t a m b a a a i n a y a mung’unya,” utaona kuwa imekuja kilugha kwa usulubu wa kuonesha kuwa aina hii ya mti siyo mti mmoja bali kuna aina nyingi (species). Na hili ni kweli kisayansi kwani kuna aina kadhaa za miti ya mung’unya. Huu ni ukweli mwingine wa kisay – ansi wa Qur’an wana – sayansi walitumia ngu – vu na utafiti mkubwa kwa kubaini na kuaini kuwa kuna aina (species) nyingi za mimea hii! Hadi sasa zimegunduliwa aina zi – sizopungua 1000! Wanazuoni wa Kiislamu wa zamani wameelezea tangu zama – ni kuwa mmea wa mung’unya una faida nyingi kiafya. Kwanza, wao walikuwa wanatumia mung’unya katika kumuiga Mtume ambaye alikuwa anapen – da sana mung’unya na wakiamini kuwa bila shaka katika kupenda kwake Mtume tunda hili ni ishara kuwa lina faida nzuri kiafya licha ya ladha yake nzuri. Lakini, wanazuoni walikuja baadaye kugundua faida hizo nyingi. Moja kati ya faida za mung’unya kwanza ni chakula baridi, laini na rahisi sana kuyeyushwa tumboni. Pia lina kiwango kizuri cha kamba lishe. Katika hali ya udhaifu aliokuwa nao Na – bii Yunus baada ya kucheuliwa na samaki, Mwenyezi Mungu al – imuoteshea mmea huu uli – omsaidia kumpa nguvu. Mung’unya lina nini hasa kil – ishe hadi liwe ni chakula muwa – faka kwa Mtume wa Allah ali – yekuwa amecheuliwa na samaki chewa hali ya kuwa akiwa mnyonge baada ya kukaa tum – boni mwa samaki kwa muda fu – lani? Ni upi mnasaba kilishe wa tunda hili na faida zake kwa mgonjwa? Mung’unya lina viini lishe na virutubisho gani hadi liwe chakula cha awali cha Nabii Yu – nus alipocheuliwa? Kwa nini iwe m u n g ’ u ny a n a s i m m e a mwingine? Haya na mengine tut – ayaangazia kwa mapana katika makala ijayo Inshaallah. Hakika hii Qur’ani ni muujiza. . Itaendelea…

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close