6. Kutoka Katika Quran na Sunnah

Sayansi Mamboleo na Mafunzo Mbalimbali Ambatanishi

Mpenzi msomaji Allah amesema: “Kinatoka katika matumbo yao kinywaji cha rangi mbali mbali ndani yake mna shifaa (ya magonjwa) kwa watu. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aya (ishara, dalili, zingatio) kwa watu wanaotafakari (Qur’an, 16: 69).

Imamu Bukhari anasimulia kutoka kwa Abu Huraira (Allah amridhie) kwamba Mtume Muhammad (rehema na amani ya Allah iwe peke yake) amesema: “Habbat-sawdaa inatibu kila kitu isipokuwa mauti.” Mpenzi msomaji, katika makala iliyopita nilikuahidi kuwa katika makala hii tutafahamishana juu ya baadhi ya magonjwa yanayotibiwa kwa asali. Kabla hatujaingia kuyataja baadhi ya magonjwa hayo hebu tutaje dawa nyingine muhimu iliyotajwa katika hadithi mbalimbali za Mtume. Imamu Bukhari anasimulia kutoka kwa Abu Huraira (Allah amridhie) kwamba Mtume Muhammad (rehema na amani ya Allah iwe peke yake) amesema: “Habbat-sawdaa inatibu kila kitu isipokuwa mauti”. Hivyo, dawa hii ya asali ikichanganywa na habbatsawdaa inakuwa dawa juu ya dawa. Kwa faida ya afya kwa ujumla, kunywa kijiko kimoja cha mafuta ya habbat-sawdaa asubuhi na usiku, au kunywa japo asubuhi kabla ya kifungua kinywa kwa kuchanganya na kijiko kimoja cha asali safi. Kuondoa udhaifu kwa ujumla mtu atachukua unga wa habbat-sawdaa kiasi cha kikombe kimoja, uwatu mfano wake na ambari (ambergris) iliyoyeyushwa kiasi cha kijiko kidogo. Vyote atavichanganya katika chombo chenye asali iwe kama jamu; halafu awe akila kama jamu kila siku na wakati wowote apendao lakini kwa mkate wa ngano asili. Miongoni mwa magonjwa yanayotibiwa na asali ni matatizo ya kibofu cha mkojo/figo. Tiba hii Insha Allah inapatikana kwa mtu kunywa maji ya moto yaliyochanganywa na ½ (nusu) kijiko cha habbat-sawdaa pamoja na asali kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Inatakikana kuchanganya vikombe viwili vya habbat-sawdaa iliyosagwa na ½ (nusu) kikombe cha asali safi na kisha kunywa kijiko kimoja cha mchanganyiko huu pamoja na kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Mchanganyiko huu unaweza kukaa kwa siku 15 na ikiwa utatengenezwa kwa matumizi ya siku kadhaa basi ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi. Asali hutibu pia tatizo la jiwe la figo. Hapa inahitajika kikombe kimoja cha habbat-sawdaa iliyochanganywa pamoja na bilauri moja ya asali, vitunguu saumu vitatu vilivyosagwa na karafuu. Kisha atachanganya vitunguu swaumu, karafuu pamoja na asali na habbat-sawdaa na kisha kunywa kijiko kimoja kabla ya kula chakula na kwa pendekezo mgonjwa anashauriwa kula limau (bila ya kumenywa) na kurudia haya kwa wiki moja. Insha-Allah jiwe litaondoka. Hata shinikizo la damu (high blood pressure) linaweza kutibiwa kwa kutumia asali. Tiba hii ni kwa kuchanganya kijiko kimoja cha habbat-sawdaa iliyosagwa, k i – jiko kim o j a c h a asali safi na kitunguu kiasi kidogo. Mgonjwa atakunywa mchanganyo huu kabla ya kufungua kinywa kwa siku 20. Hata Kumbukumbu (memory) inaweza kuimarishwa kwa kunywa kijiko kimoja cha unga wa habbats a w d a a k w a kuchanganya na asali mara mbili kwa siku. Ama kuhusiana na nishati, a k i l i n i n a wepesi wa kuhifadhi, m t u atachemsha nanaa (mint leaf), kisha aichanganye na asali na aingize matone saba ya mafuta ya habbat-sawdaa. Kisha anywe kinywaji hiki kikiwa na vuguvugu wakati wowote apendao. Basi atajionea namna fahamu itakavyofanya kazi. Muhimu zaidi asali inaimarisha utaratibu wa ulinzi wa mwili. Kula kijiko kimoja cha habbat-sawdaa na asali mchana na usiku kunatibu tatizo la kutoweza kuzuia haja ndogo (mkojo). Mchanganyiko wake ni kijiko kimoja cha habbat-sawdaa pamoja na asali, kisha kunywa maji ya vugu vugu. Hata ngozi kavu inaweza kutibiwa kwa kuchanganya asali pamoja na robo kijiko cha habbatsawdaa na kuwa kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Matatizo ya upepo (gesi) pia yanaweza kutibiwa kwa kuchanganya asali pamoja na robo kijiko cha habbatsawdaa na kuwa kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Baridi yabisi (rheumatism) pia inaweza kutibiwa kwa kutumia asali. Kwa ajili ya tiba hii, mgonjwa atachemsha mafuta ya habbat-sawdaa na atasugua kwayo ile sehemu yenye ugonjwa kwa nguvu kama kwamba anasugua mfupa wala siyo ngozi! Na atayanywa baada ya kuyachemsha vyema na kuyachanganya na asali kidogo. Ataendelea na tiba hiyo huku akiwa ni mwenye imani na yakini kuwa Allah atamponya. Hata ukosefu wa usingizi ni maradhi yanayoweza kutibiwa kwa asali. Hapa mgonjwa atachukua kijiko kimoja cha habbatsawdaa, na kuchanganya na gilasi ya maziwa moto yaliyochanganywa na asali. Baada ya kupoa kiasi atakunywa. Maradhi ya wanawake na uzazi pia yanatibika vizuri kwa asali. Miongoni mwa dawa kubwa zinazosahilisha kuzaa ni habbatsawdaa iliyochemshwa ikachanganywa na asali na kiziduo cha babunaji (chamomile). Habat sawdaa ni kama burashi katika uke wa mwanamke yenye faida kubwa kwao pamoja. Vilevile ni faida kubwa kutumua mafuta ya habbat-sawdaa katika kila kinywaji cha moto kwa maradhi yote ya wanawake. Kutibu tatizo la utasa, BiidhniLlah, tumia mchanganyiko wa unga wa habbat-sawdaa, unga wa uwatu na mbegu ya figili kwa vipimo sawa, na kisha kula kijiko kimoja asubuhi na jioni ilihali imekorogwa katika nusu kikombe cha asali, na baadaye akifuatisha kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia. Hata tezikibofu (prostate gland) hutibika kwa asali. Mgonjwa anatakikana ajipake mafuta ya habbat-sawdaa chini ya mgongo na chini ya korodani (mapumbu) na kusugua kwa mzunguko pamoja na kula unga wa habbat-sawdaa kijiko kimoja na robo kijiko kidogo cha manemane katika nusu gilasi ya asali iliyotiwa katika maji yenye vuguvugu kila siku na wakati wowote apendao. Matone kadhaa ya mafuta ya habbat-sawdaa yaliyotiwa kwenye maziwa ya moto na asali humaliza asidi (acidness). Asali pia ni dawa nzuri ya kutibu majeraha kama ya kuungua na moto. Hata vidonda mgonjwa anaweza kujitibu kwa kutumia asali ambapo atayachanganya matone kumi ya mafuta ya habbat-sawdaa, katika kikombe cha asali na kijiko kimoja cha maganda ya komamanga yaliyokaushwa na kusagwa, kisha atakula kila siku kabla ya kula chakula na baadaye atakunywa gilasi ya maziwa yasiyotiwa chochote. Haya ni baadhi tu ya magonjwa yanayotibiwa kwa asali, kinywaji kinachotoka katika tumbo la nyuki ambacho Allah kakiita kuwa ni shifaa au ponyo la maradhi mbalimbali. Ametukuka Mola wetu aliyetuteremshia Qur’an Tukufu yenye haya na zaidi ya haya. Itaendelea…

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close