6. Kutoka Katika Quran na Sunnah

muislamu na swaumu

SEHEMU YA 1 UFAFANUZI JUU YA BAADHI YA HUKUMU MUHIMU ZINAZOHUSIANA NA SWAUMU
Allah anasema; “Enyi mlioamini! Mmefaradhishwa kufunga (swau- mu) kama ilivyofaridhishwa kwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kuwa wacha Mungu. (Swaumu ni) Siku za kuhesabika.

“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safa- rini, basi akamilishe idadi katika masiku mengineyo. Na kwa wale wanaoiweza lakini kwa mashaka watoe fidia; kulisha masikini. Na atakayefanya kwa hiyari yake jema lolote, basi hilo ni bora kwake. “Na mkifunga Swaumu ni bora kwenu mkiwa mnajua. Mwezi wa Ramadhani ambao imeterem- shwa humo Qur’an ili iwe muon- gozo kwa watu na hoja bayana za muongozo na upambanuo (wa haki na batili). Basi atakayeshuhu- dia miongoni mwenu mwezi na afunge Swaumu. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi katika siku nyinginezo,” (Qur’an,183-185). Mpenzi msomaji, tukiwa kati- ka masiku ya awali kabisa ya Ra- madhani nifungue makala yangu hii ya leo katika ukurasa wetu wa, ‘Kutoka Katika Qur’an na Sunnah’ kwa furaha na bashasha niliyo- nayo kwa kuidiriki Ramadhani. Nianze kwa kukutakia Ram- adhani yenye kheri, fanaka na baraka, ‘Ramadhani Mubarak’. Hili ni neno lenye asili na limekuja katika Hadithi za Mtume wetu Muhammad. Tukipongezana tuseme ‘Ramadhani Mubarak’, wala tusiseme, ‘Ramadhani Kar- imu,’ maneno tuliyozoea kusema lakini hayanaasli. Hivyo tujifunze kusema, ‘Ram- adhani Mubarak’, badala ya kuse- ma, ‘Ramadhani Karimu,’ tuliyo- zoea kusema. Kwanza nianze kwa kusema kuwa nawashukuru sana wazazi wangu wale waliotangulia mbele ya haki (Allah awarehemu) na wale walio hai, Allah awape tawfi- iq kwa kunizoeza kufunga tangu nikiwa mdogo. Hakika, ni jambo jema kwa wazazi kuwazoeza wa- toto wao kufunga tangu wakiwa katika umri mdogo hata kama ni kwa masaa kadhaa. Swaumu ya mtoto, ni musta- habb (imependekezwa) na si waji- bu. Mtoto akifunga, anapewa tha- wabu; na ikiwa ataacha kufunga, hapati dhambi. Hata hivyo, ina- takikana kwa mlezi wake kumua- mrisha kufunga ili azowee. Wavulana na wasichana waki- fikisha umri wa miaka saba, wan- apaswa kuamrishwa kuanza swaumu ili wajizoeze. Hivyo ni juu ya wazazi kuwaamrisha watoto hao kufunga hali kadhalika kama wanavyopasa kuwaamrisha Swa- la. Wanapobaleghe, Swaumu im- ewawajibikia. Ikiwa watakomaa wakati wa swaumu, siku zao (wanazofunga) ni sahihi. Ikiwa mvulana atafiki- sha miaka kumi na tano mchana wakati yuko na swaumu, siku yake ni sahihi. Mwanzo wa siku hiyo (swaumu kwake) ilikuwa ni Sun- na na mwisho wake itakuwa ni wajibu ikiwa tayari kishatokwa na nywele za sehemu za siri au kashaanza kutokwa na manii. Hali kadhalika, hii inawahusu wa- nawake ambao wanabaleghe kwa kutokwa na damu ya hedhi. Mpenzi msomaji, swaumu ni ibada ya masiku machache yenye kuhesabika, ikianza tu baada ya masiku machache hiyooo inaisha. Swaumu kama zilivyo ibada ny- ingine ni nyepesi kutekeleza na kama ilivyo kawaida ya Sharia ya Kiislamu, imezingatia namna na njia mbadala za kuwawepeshia waja wa Allah ambao wanapata aina fulani za tabu na shida katika kuziendea ibada mbalimbali zili- zoamrishwa ikiwemo swaumu. Hili linaonekana wazi katika maneno ya Allah aliposema; “Atakayekuwa mgonjwa miongo- ni mwenu, au yuko safarini, basi na aje akamilishe idadi katika masiku mengineyo, (Qur’an, 184,185). Hii ni kwa sababu aghalabu maradhi na safari ni miongoni mwa vitu vinavyoathiri uwezo wa mwili wa mwanadamu kutekeleza kwa wepesi baadhi ya majukumu zikiwemo ibada mbambalimbali. Kwa hiyo kwa kuzingatia hili, Sharia ya Kiislamu imemruhusu mgonjwa kufungua katika Mwezi wa Ramadhani na kulipa. Ukiangalia kwa kina, utaona kuwa ugonjwa unaozungumziwa unaofanya iruhusike kufungua swaumu si kila aina ya ugonjwa au magonjwa yote bali ni yale ma- gonjwa ambayo mtu akiwa anau- gua akifunga atapata tabu au anaweza kuchelewa kupona.Mgonjwa ana hali kadhaa kuhusiana na swaumu. Kuna mgonjwa ambaye swaumu haim- dhuru wala haimtaabishi. Huyu haruhusiwi kufungua. Wa pili ni mgonjwa ambaye swaumu in- amtaabisha lakini haimdhuru, naye kufunga kwake ni makruhu kwa kuwa si jambo zuri kuke- ngeuka ruksa ya Allah. Wa tatu ni mgonjwa ambaye swaumu inam- dhuru na huyu inampasa kufun- gua, na kufunga kwake kwake haifai. Mpenzi msomaji, Allah Ameruhusu msafiri kufungua ak- iwa safarini. Kuna hali tatu za msafiri na ruksa ya kufungua swaumu; Kwanza kuna safari am- bayo hakuna shida wala tabu yoy- ote. Yaani safari yake iwe ni sawa na kutokusafiri kwake. Katika hali hii iliyo bora kwa msafiri huyu ni kufunga lakini akifungua hapana tatizo. Hali ya pili ni pale mtu anapo- funga akiwa safarini anapata tabu lakini sio tabu kubwa. Katika hali hii, jambo bora ni kufungua. Hali ya tatu ni pale msafiri anapofunga anataabika sana. Hapa kinacho- takiwa ni kufungua. Mpenzi msomaji suala la mtu kufungua akiwa safarini halifun- gamani na muda wala umbali wa safari au aina ya usafiri. Kama nilivyotanguliza kusema kuwa wasafiri wameruhusiwa ku- fungua Mwezi wa Ramadhani la- kini hapa linakuja suala ambat- anishi ambalo ni hukumu ya Muislamu kufungua mgahawa au hoteli, mfano, katika sehemu zi- sizokuwa na Waislamu au mfano mzuri hoteli zilizojengwa njiani kwa ajili ya wasafiri katika bara- bara zinazotoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine. Je ina- faa kufungua hoteli hizo mchana wa Ramadhani kwa ajili ya ku- wauzia wasio Waislamu au kwa ajili ya kuwauizia wasafiri? Hili ni jambo lililoruhusiwa kisharia. Hivyo hakuna matatizo kwa Muislamu kufungua hoteli au mgahawa wake au duka amba- lo wanauza chakula, na vitu vinginevyo, kwa kuwauzia wale ambao hawaingii katika hii huku- mu (ya kufunga) kama Mayahudi, Manaswara, Waislamu Wasafiri nk. Hata hivyo, Muislamu hatak- iwi kuwauzia chakula Waislamu ambao wamefunga au Waislamu ambao anajua kabisa kwamba watakila mchana. Lakini akijua kuwa watakihifadhi chakula hi- cho mpaka wakati wa adhana ya Magharibi, hakuna tatizo (ku- wauzia). Hakuna ubaya kwa Muislamu kuwauzia chakula au kinywaji hata Waislamu ambao hawakuwajibika na swaumu mchana wa Ramadhani kama watoto, wanawake walio katika siku zao au wagonjwa nk. Mpenzi msomaji, yule ambaye anashindwa kufunga, na hatarajii ‘kushindwa huko’ kutaondoka ka- tika maisha yake, kama vile mgonjwa, anatakiwa badala ya kufunga awalishe masikini kila siku. Afanye hivyo yeye mwenyewe au atolewe hicho cha kuwalishia masikini na ndugu zake au wa- naomlisha yeye kama hana uwe- zo.Ni vizuri ndugu zangu tukazi- chukua hukumu hizi kwa kushau- riana na wataalamu wa tiba am- bao ikiwa watakupima wanaweza kukwambia hali yako kwa uhaki- ka na wewe mwenyewe ukajua hukumu yako ni ipi; aidha ni mtu wa kufungua na kuja kulipa baa- daye au hupaswi kabisa kufunga na hivyo uwajibike kutoa kibaba na kulisha masikini. Si vema mtu kujiamulia kivyake wakati tuko katika wakati ambao mambo kama haya yanaweza kuelezwa vizuri sana kitiba. Tena kuna sisitizo la Allah juu ya kuuliza wale wanaojua. Daktari anaweza kujua zaidi hali ya mgonjwa kuliko mgonjwa mwenyewe kwani wakati mgonjwa anachojua zaidi ni mau- mivu, daktari anakwenda mbali zaidi kiasi anaweza kumueleza mgonjwa afunge au asifunge kutokana na ugonjwa alio nao na kama atafunga atapata madhara gani.

Hivyo tu- waulize wataalamu wa tiba na tu- fuate ushauri wao watakao- tupatia kuhu- siana na ku- funga kwetu.

Itaendelea…

Kwa maoni wasiliana na
m w a n d i s h i kwa namba 0717 326055

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close