6. Kutoka Katika Quran na Sunnah

Muislamu na swaumu

SEHEMU YA 3Mwanamke na Funga ya Ramadhani
Namna harakati za mapishi, hususan ya futari, zinavyo- mpotezea mwanam- ke muda wa kusoma Qur’an ndani ya Mwezi wa Ramadha- ni na suluhisho lake. Mpenzi msomaji Al- lah Aliyetukuka amesema ndani ya Qur’an Tukufu: “Mwezi wa Ramad- hani ambao imeter- emshwa humo Qur’an ili iwe muon- gozo kwa watu na hoja bayana za muongozo na upam- banuo (wa haki na batili),” (Quran, 2: 185).

Katika Hadithi, Mtume wetu Muhammad (rehema na amani za Allah zimshukie) amesema; “Anaposafiri mja au kuugua huwa anaandikiwa thawabu za yale ambayo alikuwa na ada ya kuyafanya wakati akiwa hajasa- firi na mzima.” Wanawake wengi wanap- opatwa na ada zao za kimaum- bile ndani ya Mwezi wa Ramad- hani, hukata tamaa kwa kuche- lea na kuhofia kupitwa na kheri na fadhila za Ramadhani. Kwa hakika hakuna sababu ya kuka- ta tamaa wala kuhisi simanzi na unyonge kwa kuwa kupatwa na siku hizi ni jambo la kimaum- bile ambalo Allah amewandikia wanawake. Katika utangulizi wa makala hii, baada ya kuleta Maneno Matukufu ya Allah, nimeleta Hadithi ya Mtume inayosema: “Anaposafiri mja au kuugua huwa anaandikiwa thawabu za yale ambayo alikuwa na ada ya kuyafanya wakati akiwa hajasa- firi na mzima.” Hedhi ni hali ya kimaumbile inayomjia mwanamke na kum- zuia kisheria kufanya baadhi ya mambo ambayo alikuwa akiya- fanya kabla hajapatwa na hali hii. Kwa muktadha wa hadithi hii ya Mtume niliyoileta, ikiwa mwanamke ana kawaida ya ku- fanya ibada na akifikwa na hali hii inayomzuia kisheria kuzi- fanya ibada kama mfano swau- mu, basi kwa fadhila za Allah, ataandikiwa mambo yote mazuri aliyokuwa akiyafan- ya kabla ya kufikwa na hali hii. Lakini hii haina maa- na kuwa hatatakiwa kulipa swaumu, bali atal- ipa ibada zile alizoam- rishwa kuzilipa baadaye akijitwaharisha. Mfano wa ibada anazotakiwa kuzilipa ni swaumu, na ambazo hatakiwi kuzilipa ni swala. Ulipaji wa swau- mu ni baada ya kwisha Ramadhani.Kwahiyo,mwanam- ke wa Kiislamu akiwa katika hali hii, ha- takiwi kukata tamaa wala kuhisi un- yonge.Ukwe- li wa hili la mtu kuandikiwa thawabu za mambo ya kheri ambayo anatamani kuyafanya lakini akapatwa na udhuru uliomzuia kuyafanya, tunaupata katika maneno ya Mtume wa Allah pale alipow- aambia Maswahaba zake waki- wa katika ji- had, kuwa k i l a ali-yekuwa anatamani kwenda ka- tika jihad akiwa na nia ya kweli na kuwa hakwenda kwa sababu ya kuwa na udhuru atapata tha- wabu sawa na waliotoka kwen- da katika jihad. Imamu Bukhari amepokea hadithi kutoka kwa Anas (Allah amridhie) kuwa Mtume wa Al- lah amesema: “Tumewaacha katika mji wa Madina watu am- bao hamjavuka bonde wala njia ila nao wanashirikiana na ny- inyi katika malipo, ni udhuru tu ndiyo uliowazuia kuwa na ny- inyi.” Kutokana na ukweli huu ni muhimu basi kutoa tanbihi kuwa wanawake wengi wana- pofikwa na ada zao za kila mwe- zi kipindi cha mwezi wa Ram- adhani au wakati mwingine, huwa wanaghafilika moja kwa moja na kumtaja Allah. Na kama ikiwa ni Mwezi wa Ram- adhani huwa hawahisi fadhila na ubora wa Ramadhani, kama vile Ramadhani haiwahusu kwa lolote. Wanawake hawa hujikuta wakijishughulisha na kuan- galia runinga na vya mfano wake wakidhani kwamba inafaa kwao kupoteza muda wao kwa njia hii. Jambo hili huwapelekea kuwa na hisia za uzito na uvivu wa kuja ku- fan- ya ibada wanapomaliza ada hizo za siku zao na wakati mwingine kujikuta wazito kufanya ibada ambazo walikuwa wanazifanya kwa wepesi kabla ya kufikwa na siku zao. Mpenzi msomaji, ndani ya Mwezi wa Ramadhani kuna Usiku wa Cheo (Laylatul Qadr) wenye fadhila na kheri nyingi. Zawadi hii ya fadhila na kheri hizi kubwa za Lailatul Qadr hajanyimwa mwanamke kuto- kana na udhuru wa kisheria. Alichokatazwa mwanamke ndani ya Mwezi wa Ramadhani ni kuswali, kufunga, kuzunguka al-Kaaba na kufanya Itikafu msikitini. Kwa mantiki hii, mwanamke akiwa katika siku zake anaruhusiwa kufanya iba- da zote isipokuwa hizo. Ilikuwa ni kawaida ya Mtume wetu Muhammad kuz- idisha juhudi katika ibada liki- fika kumi la mwisho la Ramad- hani, kiasi hata akiwaamsha wake zake. Hii ina maana hata wakiwa katika siku zao alikuwa aki- waamsha ili washughulike na ibada nyingine zisizokuwa zile walizokatazwa. Ibada hizo ny- inginezo ni kama kumtaja Al- lah, kuleta dua, Istighifaar nk. Yote haya yanawafanya nao wawe na fungu sawa na watu wengine katika Mwezi wa Ra- madhani. Kwa mnasaba huu, niwaam- biekundijinginelawanawake nao ni wale wanaoshughulika sana na shughuli za mapishi jikoni katika Mwezi wa Ramad- hani. Shime Alaykum, tusishu- ghulishwe na uandaaji wa ma- hanjumati mchana wote wa Ramadhaani na kusahau ku- fanya ibada zingine. Wanawake makini huandaa mahanjumati huku wakisoma au kusikiliza Qur’an, wakimtaja Allah na mfano wa haya.Hata hizo shughuli za kupi- ka, kuwandaa watoto na kuihu- dumia nyumba ikiwa patanui- wa kupata thawabu na radhi za Allah, basi zitageuka kuwa iba- da zenye thawabu kedekede. Hii ni kusema kuwa badala ya wa- nawake kushughulika na kupi- ka tu basi wapike huku wakiso- ma au kusikiliza Qur’an, waki- leta dua mbalimbali na mfano wa haya. Mpenzi msomaji, Ra- madhani hiyooo inaondoka. Ni kama jana tu tulikuwa tunain- gojea, leo tunakaribia kuiaga!!!. Namuomba Allah atuku- balie swaumu tulizokwisha funga na atu- wafikishe ku- funga zili- zosalia. Itaendelea…

 

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close