6. Kutoka Katika Quran na Sunnah

Muislamu na swaumu

SEHEMU YA 2 Ufafanuzi juu ya baadhi ya hukumu muhimu zinazohusiana na swaumu

Allah anasema: “Enyi mlio- amini! Mmefaridhishwa kufun- ga (swaumu) kama ilivyofari- dhishwa kwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kuwa wachaMun- gu. (Swaumu ni) Siku za kuhesa- bika. Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safa- rini, basi akamilishe idadi katika masiku mengineyo. “Na kwa wale wanaoiweza la- kini kwa mashaka watoe fidia; kulisha masikini. Na atakayefan- ya kwa khiari yake jema lolote, basi hilo ni bora kwake. Na mki- funga Swaumu ni bora kwenu mkiwa mnajua. “Mwezi wa Ramadhani am- bao imeteremshwa humo Qur’an ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za muongozo na up- ambanuo (wa haki na batili). Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge Swau- mu. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi ka- tika siku nyinginezo,” (Qur’an, 183-185]. Mpenzi msomaji, katika makala iliyopita miongoni mwa mambo tuliyozungumzia ni pamoja na ruhusa ya Muislamu kufungua mgahawa au hoteli mchana wa mwezi Ramadhani katika sehemu zisizokuwa na Waislamu au njiani mfano kwa ajili ya wasafiri katika barabara zinazotoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine. Nilisema kuwa hili ni jambo lililoruhusiwa Kisharia. Hakuna tatizo kwa Muislamu kufungua hoteli au mgahawa au duka am- balo atauza vyakula, kuwauzia wale ambao hawaingii katika hii hukmu ya kufunga kama Maya- hudi, Manaswara na hata Wais- lamu wasafiri nk. Tulisema kuwa hatakiwi ku- wauzia chakula Waislamu am- bao wamefunga ili wale pale au Waislamu ambao anajua kabisa kwamba watakila mchana. Laki- ni akijua kuwa watakihifadhi chakula hicho mpaka wakati wa adhana ya Magharibi ili wale kama futari hakuna tatizo ku- wauzia vyakula hivyo. Vilevile, hakuna ubaya kwa Muislamu kuwauzia chakula au kinywaji Waislamu ambao hawakuwajibika na swaumu mchana wa Ramadhani kama watoto, wanawake walio katika siku zao, wagonjwa nk. Mpenzi msomaji, watu wenye udhuru wa kisheria wa kula mchana wa Ramadhani, mfano wanawake walio katika siku zao ambao hawajulikani kuwa wako katika siku hizo wanapaswa wa- sile hadharani. Hii ni rai ya baadhi ya wana- zuoni wakitoa angalizo kuwa ku- fanya hivyo yaani kula kwao had- harani mchana wa Ramadhani, japo wao wanajijua kuwa wana udhuru kisheria; kunaleta picha ya kuonyesha kama vile wanait- weza swaumu katika macho ya wale wasiojua kuwa watu hao wana dharura kisheria. Baadhi ya wanazuoni wanase- ma kuwa ikiwa mtu anayeruhusi- ka kula mchana wa Ramadhani sababu yake imejificha kama vile mgonjwa ambaye haonekani yu taabani lakini yeye anajijua basi na afanye hivyo kisirisiri pasina kuwaonyehsa watu dhahiri kuwa anakula mchana wa Ramadha- ni. Ama wale ambao sababu zao za kula mchana wa Ramadhani zinaonekana wazi kabisa kama wagonjwa waliozidiwa, basi hakuna ubaya wakala waziwazi. Na hii ndiyo kauli yenye nguvu zaidi. Kwa hakika hili ni suala li- naloweza kuonyesha kiwango cha haya ya Mtu na kwa hakika mtu kuwa na haya ni katika ima- ni au ni alama za imani yake. Mwisho wa kula daku Mpenzi msomaji, hebu sasa tugeukie kidogo na kuiangazia daku; chakula chenye baraka ki- nacholiwa kwanzia theluthi ya mwisho ya usiku. Je ni upi muda hasa wa kikomo chake na je mtu anaruhusiwa kuendelea kula daku wakati muadhini anaadhi- ni adhana ya pili? Mpenzi msomaji, suala la mtu kula daku au kuacha kula daku kutokana na adhana linategem- ea Muadhini anaadhini kwa ajili ya jambo gani. Kama Muadhini anaadhini kwa ajili ya Alfajiri, yaani anatoa Adhana ya kuwa Alfajiri imeshaanza (Adhana ya pili), basi lazima usimame kula na kunywa kwa sababu Mtume wetu Muhammad (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Msisimamishe daku yenu mnaposikia adhana ya Bi- lali, kwani yeye anaadhini usiku, kwa hiyo kuleni na kunyweni mpaka Ibn Ummu Maktuum aadhini.” Bilali alikuwa akiadhini mapema sana kama tanbihi kuwa wakati wa Alfajiri unakar- ibia. Ama Ibn Ummu Maktuum yeye alikuwa anaadhini wakati wa Alfajiri ya kweli unapoingia. Aya inasema: “Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapam- bazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku),”(Qur’an, 2:187). Vilevile, ikijulikana kama Al- fajiri imeingia mtu, iwe ni mahali ambapo adhana inasikika au haisikiki, na aache kula na kunywa, hata kama hakusikia adhana. Lakini kama Muadhini anaadhini mapema au kama kuna shaka na adhana yake kama imewafikiana na Asubuhi au siyo, basi mtu anaweza kula na kunywa mpaka atakapokuwa na uhakika kuwa Alfajiri ime- shaanza, ikiwa inajulikana hivyo kutokana na saa maarufu zina- zothibitisha kuanza Alfajiri au kutokana na Muadhini mwenye kuaminika anayejulika- na kuwa anaadhini wakati wa Alfajiri. Kwa hali hii ikiwa adhana im- eadhiniwa mapema sana basi mtu anaweza kula wakati adha- na inaadhiniwa, kwa sababu hakuna hakika kama adhana in- aadhiniwa kwa wakati wake ulio sahihi, bali huenda kulikuwa tu ni kwa makisio na si kwa uhaki- ka. Pamoja na hili, ni makosa watu kushika vifungua kinywa wakisubiri hadi muadhini aa- dhini hata kama wakati umefika. Tunatakiwa tufungue kwa kuwa wakati umefika na si kwa kuwa muadhini anaadhini au hadi muadhini aadhini. Mpenzi msomaji, katika makala hii namili na kuegemea zaidi kauli inayosema kuwa mwenye mimba na mnyonye- shajiwakihofiamadhara kwenye afya zao, hukumu yao itakuwa kama ya mgonjwa; yaani itabidi wale na wasifunge na watalaz- imika kulipa masiku yajayo. Na ikiwawaobinafsihawaku- weza kufunga siku miongoni mwa siku kwa sababu za kisheria kama ugonjwa hapo waataingia haswa kwenye hukumu mion- goni mwa hu- kumu za mgonjwa tuli- zotangulia kutaja katika makala iliyopi- ta. Itaendelea…

Show More

Related Articles

Back to top button
Close