6. Kutoka Katika Quran na Sunnah

Mtazamo wa Uislamu juu ya majukumu ya mwanamke

Hakika Mwenyezi Mungu ameviumba viumbe kwa aina tofauti kimaumbile na kijinsia. Pia, Mwenyezi Mungu akahuisha kila kiumbe kwa kukipa kazi na jukumu maalum. Hakuna awezaye kuyafanya haya isipokuwa Mola wetu, kama walivyothibitisha wataalamu wa viumbe hai waliozama katika fani ya uwiano wa mazingira.

Miongoni mwa viumbe hivyo ni mwanadamu aliyepewa jukumu lililotukuka zaidi la kumwabudu Mwenyezi Mungu kama alivyosema:

“Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” [Qur’an, 47: 56].

Pia, Mwenyezi Mungu alipoumba viumbe – hai, alivigawanya katika jinsia mbili, ya kiume na kike. Kisha, Allah akainisha sifa, majukumu na kazi maalum kwa kila jinsia kwa mujibu wa maumbile na tabia yake.

Maumbile yanawamujibisha mwanamme atoke nyumbani kwa ajili ya kutafuta riziki kupitia kazi. Naye mwanamke atakiwa akae nyumbani ambako ni mahali pa kawaida kwa mwanamke kutokana na sifa zake za kike. Kukaa nyumbani pia ni katika juhudi za kumlinda mwanamke kutokana na mabaya yanayoweza kumpata akitoka nje ya nyumba yake.

Mwanamke akikaa nyumbani anaepukana na maovu, fitina na ushawishi. Akikaa nyumbani, mwanamke anaweza kuzingatia urembo wake na hali yake kwa jumla bila ya kusumbuliwa na yeyote. Vilevile, mwanamke hupata utulivu wa kiroho na akili akiwa nyumbani, jambo linalomsaidia kutunza nyumba na kutekeleza majukumu yake humo.

Kwa kweli, kuunda na kutunza familia ni kazi kubwa mno inayotegemea ushirikiano wa mume na mke, ambapo kila mmoja ana wajibu wa kufanya. Mwanamme atagharamia matumizi ya kuendesha maisha ya familia kwa kufanya kazi, biashara au kilimo. Wakati huo huo, mwanamke ana wajibu wa kutunza nyumba na kuwalea watoto na kutekeleza majukumu mengine nyumbani mwake.

Inafahamika kwamba wajibu ambao mwanamke anatakiwa kuzitimiza kwa nyumba na familia ziko nyingi na nzito kwa kiasi ambacho kinambidi atumie wakati wake wote na juhudi zake kufanya kazi zake hizo. Kwa kuwa mwanamke anatakiwa kuwatunza watoto, nyumba, vyakula na mengine mengi, basi mazingira yanayofaa kwa mwanamke kupata mafanikio na ufanisi ni nyumba yake, kwa hiyo akifanikiwa katika kazi yake hii akitekeleza wajibu zake barabara huwa sababu ya msingi kuunda familiya yenye furaha, amani na utulivu ambayo huwa msingi mzuri wa kizazi kizuri kwa jamii.

Hatahivyo, mwanamke asiporuhusiwa kutoka kabisa, tutapata shida kubwa kwani baadhi ya kazi zinamtegea yeye, mathalan matibabu ya uzazi kwa wananwake, kufundisha watoto na wanawake wenzao. Kwa hiyo, umma wanatakiwa kuandaa baadhi ya wanawake wanaoweza kushughulikia mambo haya ili kukidhi mahitaji ya jamii.

Uislamu umezingatia sana haki na maslahi ya mwanamke kwa kubainisha kazi zinazofaa zaidi kwake ikiwa ni pamoja na kutunza nyumba, akiamriwa ajiepushe na mambo yanayovunjia heshima. Mwenyezi Mungu Amesema:

“Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani” [33:33].

Aya hii ina ishara ya kibalagha ambapo Mwenyezi Mungu amezihusisha nyumba na wanawake kubainisha kuwa nyumbani ndio makazi ya wanawake. Nyumba kwa mwanamke ni kazi, malazi na makazi, ila akitoka iwe ni kwa dharura tu.

Vilevile, Uislamu umemwondolea mwanamke baadhi ya wajibu na majukumu ambayo mwanamme anayo. Imefanyika hivi kwa sababu ya tofauti ya jinsi na maumbile ya wote wawili. Miongoni mwa wajibu ambao mwanamke kaondiyolewa ni sala ya jamaa na ile ya Ijumaa.

Sheria ya Kiislamu imebainisha kuwa bora ya sala ya mwanamke ni nyumbani mwake. Ibn Omar (Allah amridhie) amesimulia kwamba Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) alisema:

“Msiwazuieni wake zenu kwenda misikitini; ila kusali majumbani ni bora kwao.”

Uislamu haukuwakataza wanawake kwenda kusali msikitini. Uislamu umewashauri wanaume wawaruhusu kwenda misikitini kwa sharti ajisitiri kwa mavazi ya Kiislamu (Hijab) kiasi kwamba asishawishi watu. Lakini, tusisitize kuwa, kama ambavyo Uislamu umempa mwanamke haki ya kutoka, umempa pia mumewe haki ya kuombwa idhini, kama inavyoelezwa katika hadith iliyosimuliwa na Ibn Omar (Allah amridhie) akimnukuu Mtume kwamba amesema:

“Yeyote kati yenu mke wake aliomba ruhusu ya kwenda msikitini asimzuia.”

Hatahivyo, mwanamke atapata thawabu nyingi akisali nyumbani kwake. kwa sababu sala ya nyumbani humuepusha mwanamke na fitina na ushawishi.

Sheria ya Kiislamu ilipokuwa inatambua haki ya mwanamke kufanya kazi (hasa katika shughuli ambazo lazima zifanywe na mwanamke) iliainisha vidhibiti na masharti maalum, ambavy tutavitaja hapa kwa ufupi. Kazi iwe inafaa kwa mwanamke kimwili, kimaumbile na kiroho.

  • Kazi nzuri za mwanamke ni katika sekta ya elimu, kutunza watoto na kutibu wanawake wenzao.
  • Kazi isipingane na jukumu lake la msingi la kutunza nyumba na familia yake (mume na watoto). Hii ina maana nyumba yake isiathiriki sana kutokana na kazi yake hiyo.
  • Aombe ruhusa ya walii yake ambaye ni mzazi au mume, iwapo ameolewa.
  • Kazi isihusishe maovu wala vitu vya haramu kama ulevi na uasherati.
  • Ashikamane na uchamungu na awajibike na mwenendo wa Kiislamu na tabia zilizo bora kimaneno na kivitendo. Pia, aepuke kuwa sababu ya kushawishi wengine wala kushawishi wengine.
  • Awajibike kwa mavazi ya Kiislamu na adabu alizozieleza Mwenyezi Mungu Aliyetukuka katika kauli yake: “Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao. Wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao.” [Qur’an, 24: 31].

Hayo ni baadhi ya masharti na adabu za kisheria ambazo mwanamke anatakiwa kuzifuata akitoka kwenda kazini ili apate ridhaa ya Mwenyezi Mungu na afanikiwe duniani na Akhera.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close