6. Kutoka Katika Quran na Sunnah

Kudumu na ibada baada ya Ramadhani ni ishara ya kukubaliwa swaumu

Mpenzi msomaji na hasa wewe Muisla- mu uliyekuwa umesimama kidete kujitahidi na ibada katika Mwezi wa Ramadhani, unaelewa nini un- aposoma katika masiku ya mwisho ya Ramadhani Aya ya Allah katika Su- rat Al – Imran Aya ya 144?

Allah anasema; “Na Muham- mad si yeyote isipokuwa ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je, akifa au akiuawa mtageuka nyuma ya visigino vyenu (mrudi ukafirini)? Na atakayegeuka nyuma ya visig- ino vyake, basi hatomdhuru Al- lah kitu chochote. Na Allah ata- walipa wenye kushukuru. Na unaelewa nini unaposoma Hadithi ya Mtume iliyorekodiwa na Imamu Bukhari na Muslim kutoka kwa Anas ambapo aliele- za kuwa Mtume wa Allah (rehe- ma na amani ya Allah imshukie) alisema: “Mambo matatu atakayekuwa nayo, atapata uta- mu wa Imani; Allah na Mtume Wake wawe vipenzi zaidi kwake kuliko wengineo, ampende mtu na wala asimpende isipokuwa kwa ajili ya Allah, na achukie ku- rudi katika ukafiri baada ya Allah kumuokoa kutoka huko kama anavyochukia kuingizwa moto- ni”. Naam; kwa watu wengi ibada walizokuwa wakizifanya katika Mwezi wa Ramadhani zitaishia siku ya Idd sawa kabisa na mbio za sakafuni. Mpenzi msomaji. mafunzo ya ibada ya Swaumu yanakusudiwa kubakia na kutekelezwa na kila mmoja wetu baada ya kumal- izika kwa chuo hiki adhimu kwa muda wote utakaofuatia baada ya Ramadhani. Hebu tujikum- bushe kidogo falsafa ya Ramad- hani. Kwanza kabisa, suala zima la kujizuwia na kula, kunywa na matamanio ya kiwiliwili kutoka alfajiri hadi magharibi tunapata mafundisho maalumu. Katika mafunzo hayo ni pamoja na: Utulivu na upole, kuwa na tafakuri, kuishi ndani ya Qur’an, kuwafikiria waja wenzetu na hali ya Ummah wa Kiislamu kwa ujumla, kujiweka mbali na mapambo na matamanio ya vitu vya kidunia.Mafunzo haya na neema ny- ingi yanatuwezesha, kwa uwezo wa Allah, kutupa faida ya hali ya juuyauvumilivunaustahamilivu katika nafsi zetu. Allah anasema katika Qur’an: “Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na swala. Hakika Allah Yu pamoja na wanaosubiri,” (Qur’an, 2: 153). Kumpenda Allah na kumtii kwa maamrisho Yake ndiyo msingi wa ibada na ndiyo lengo hasa la sisi wanadamu kuwepo hapa ulimwenguni. Kwa ajili hiyo basi tunapojiuliza na kutafakari mafunzo tunayoyapata ndani ya Ramadhani na umuhimu wake kwa maisha yetu ya kila siku, in- atubainikia kuwa lengo hasa la kuingia kwenye chuo hiki adhimu ni kuziweka nyoyo zetu ndani ya taqwa ya kumtii Allah kwa muda wote unaofuatia baa- da ya Ramadhani. Allah anasema ndani ya Qur’an: “Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu, na poza kuponyesha yaliy- omo vifuani, na uwongofu, na rahma kwa Waumini. Sema, ‘Kwa fadhila ya Allah na rahmah Yake!’ Basi na wafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanay- oyakusanya,” (Qur’an, 9: 57–58).Hivyo basi, ni wazi kabisa kuwa ibada ya funga ya Ramad- haninikatikanguzokubwa iliyo muhimu ya Dini ya Kiislamu iliy- okusudiwa kutusaidia kama wa- nadamu katika kufanikisha len- go la kuwepo kwetu duniani kama Makhalifa wa Allah. Kwa kuwa Ramadhani ni chuo adhimu cha kutuleta ndani yake taqwa pale tunapokuwa wastahamilivu na wanyenyekevu katika kufuata maamrisho ya Al- lah ndani ya nafsi zetu tunapata faida ya kuwa waadilifu na kuipi- gania njia ya Allah ndani ya nafsi zetu kwanza. Vita hivi vya kuzilea nafsi kwa ajiliyaAllah,huitwajihad. Jihad inakusanya mambo kuanzia vita dhidi ya wanaowapiga vita Wais- lamu, hadi vita dhidi ya yale yote yaliyokatazwa na Allah ili kupata daraja ya juu kabisa ya mafanikio katika maisha ya Muislamu mbe- le ya Allah. Juu ya hili Allah anasema ka- tika Qur’an: “Wale walioamini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Allah kwa mali yao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Al- lah. Na hao ndiyo wenye kufu- zu,” (Qur’an, 9: 20). Wengi wetu huelewa neno ji- had ni kuchukua silaha na kwen- da vitani tu. Jihadi kubwa haswa ni kupigana na nafsi zetu kwa kuacha yale yote tuliyokatazwa na Allah na Mtume wake na ku- fanya yale tuliyoamrishwa ndani ya Uislamu. Hili ndilo lililokuwa hasa lengo la swaumu yetu ya Mwezi wa Ramadhani. Swaumu yetu iwe ni kichocheo cha kusimama katika njia ya haki kwa kumtii Allah kwa kufuata maamrisho yake na kujiweka mbali na makatazo yake. Ikiwa tutafanya hivi tutafuzu mbele ya Allah kwa kuishi maisha bora hapa duniani na kutarajia mema kesho Akhera. Ikiwa wahenga walinena Ku- vunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi, Hivyo basi kwisha kwa Ramadhani isiwe ndiyo mwisho wa sisi kufanya mema na kuishi nje ya mipaka ya Allah. Bali tubebe tabia zote njema tuli- zojifunza ndani ya mwezi huu mtukufu na kwa kufanya hivyo tu, ndiyo tutakuwa Waislamu wa kweli.Aliyekuwa anaabudu Ramad- hani basi Ramadhani imeshaaga, lakini aliyekuwa anamwabudu Allah, basi Allah Yu hai daima kama anavyosema: “Allah, hapa- na Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliye hai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo kati- ka ardhi. Nani huyu am- baye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi vi- wili hivyo. Naye ni Mwenye Ul- uwa,Ametuku- ka, Adhimu; Mkuu kabisa,” (Quran, 2: 255)

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close