6. Kutoka Katika Quran na Sunnah

Kilicho Wajibu Kwenu ni Nafsi Zenu!

Mama wa Waumini, Zainab bint Jahsh (Allah amridhie) amehadithia kwamba, Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) aliingia chumbani kwake akiwa amefadhaika huku akisema: “Laailahaillallah. Ole wao Waarabu na shari inayowanyemelea. Leo hii ukuta wa Yaajuj wamaajuj umefunguliwa kiasi hiki!” Kisha Mtume akachora duara dogo kwa kutumia kidole cha shahada na kidole gumba halafu akainua juu vidole vyote viwili, ikiwa ni ishara ya onyo kwa umma wake. Mama Zainab akamuuliza: “Ewe Mjumbe wa Allah, hivi tunaweza kuangamizwa sote ilihali miongoni mwetu wamo watendao wema.” Mtume akamjibu: “Ndiyo, maovu yatakapokithiri (nyote mtaangamizwa).” [Bukhari na Muslim]

Mafundisho ya tukio

Kuenea kwa maasi na ufi sadi katika ardhi ndiko kunakopelekea ongezeko la majanga ya zilzala (tetemeko la ardhi), tufani, dhoruba, mvua za mawe au maporomoko ya milima, vimbunga na kadhalika. Allah ameweka sharia na kanuni zake ambazo ni wajibu kuzichunga na kuzilinda ili maisha yaweze kuendelea na watu wasalimike na adhabu za duniani na Akhera.

Kwenda kinyume na sharia za Allah ni kujiangamiza sisi wenyewe. Historia ya Uislamu imejaa mifano ya watu mbalimbali ambao waliishi kinyume na muongozo wa Allah hatimaye wakaangamizwa.

Qur’an inasema: “Lau (Allah) angewachukulia kwa mujibu waliyoyachuma, bila shaka angewafanyia haraka kuwaadhibu. Lakini wanayo miadi ambayo hawatapata makimbilio yoyote ya kuepukana nayo. Na miji hiyo tuliwaangamiza watu wake walipodhulumu. Na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.” [Qur’an, 18:58– 59].

Kwa mantiki hiyo, kila mwenye mamlaka kuanzia ngazi ya familia hadi taifa ananapaswa kuyadhibiti maovu yanayotokea katika jamii, vinginevyo itapoteremka adhabu ya Mwenyezi Mungu itatukumbuka sote.

Kunyamazia maovu ni sawa na kuyahalalisha

Allah na Mtume wake wametutaka kukemea maovu kadiri tuwezavyo. Allah anasema:

“Na jikingeni na fi tina ambayo haitowasibu waliodhulumu peke yao kati yenu. Na juweni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Qur’an, 8:25].

Naye Swahaba Abdullahi bin Abbas (Allah amridhie yeye na baba yake) amesema:

“Watu watakapoiona dhuluma na wasiiondoe Allah atawaadhibu wote.”

Katika zama tulizonazo shari imekithiri na mbaya zaidi watu wengi wamejiweka mbali na muongozo wa Allah. Imefi kia wakati wale wanaohamasisha maovu ndiyo wanaothaminiwa kwa kupewa heshima na kuombwa ushauri wa namna ya kukabiliana na maovu katika jamii.

Kutokana na muonekano wao mbele ya jamii, watu hao wanaohamasisha maovu wamekuwa wakichukuliwa kama kioo cha jamii na hivyo kuwafanya vijana kuiga kila wanachokifanya. Hili ndilo linalotufanya tuamini kuwa kuondoa maovu katika jamii ni jambo kubwa linalohitaji nguvu ya ziada.

Inawezekana kuepuka majanga Wanadamu hatuwezi kuzuia majanga yasitokee kwani jambo hilo liko katika mamlaka ya Allah ‘Azza Wajallah’. Hata hivyo, tunaweza kuepuka majanga kwa kupambana na sababu zinazoweza kupelekea kuibuka kwa majanga.

Kutumia sheria zilizotungwa na binadamu kupambana na janga ambalo msingi wake ni matendo machafu yanayofanywa na binadamu hakuwezi kutatua tatizo la kuenea kwa maovu katika jamii. Njia pekee ya kupambana na maasi ni kuepuka yale yote yanayosababisha majanga na si vinginevyo.

Kama nilivyotangulia kusema awali, kuenea kwa maasi na ufi sadi katika ardhi ndiko kunakopelekea ongezeko la majanga duniani. Kwa hiyo, hatuwezi kuepuka majanga isipokuwa kwa kufanya yale anayoyapenda Allah na kuyaridhia.

Mwenyezi Mungu anatuambia: “Na misiba (majanga) inayokupateni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye (Allah) anasemehe mengi.” [Qur’an, 42:30]. Mahala pengine Mwenyezi Mungu anasema: “Ufi sadi umeenea nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale yaliyofanywa na mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyoyatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.” [Qur’an, 30:41].

Kutokana na aya hizi, ni bayana kuwa Allah hateremshi janga ardhini isipokuwa kwa sababu ya maasi yanayofanywa na wanadamu. Ulevi, uzinzi, wizi, dhuluma na ghushi ni baadhi tu ya maovu yanayofanywa na watu wengi ulimwenguni. Kuchuma mali kwa njia za haramu limekuwa jambo la kawaida siku hizi.

Uislamu, ambao ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu unatutaka tushike njia za halali katika kuchuma mali hasa katika zama hizi ambazo dhuluma, unyang’anyi na udanganyifu vimetamalaki kila kona.

Imepokewa kutoka kwa Abubakr As–Swidiq (Allah amridhie) kuwa siku moja aliwaambia watu waliokuwa wamemzunguka:

“Enyi watu! Hakika nyinyi mnaisoma aya hii na kuiweka mahali pasipokusudiwa (mmeielewa vibaya): “Enyi mlioamini! Kilicho lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa nyinyi mmeongoka. Kwa Mwenyezi Mungu ndiyo marejeo yenu nyote; basi atakuambieni mliyokuwa mkiyatenda.” [Qur’an, 5:105].

Kisha Abubakr akasema kwa sauti kubwa: “Hakika nimemsikia Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) akisema: “ Watu watakapomuona dhalimu na wasimshike mikono yake ( wakamuacha adhulumu) basi watu wote watakaribia kupata adhabu ya Allah.” [Abu Daudi na Tirmidhi].

Na miongoni mwa mambo mema yaliyosisitizwa na dini ni kuamrisha mema na kukataza maovu. Kwa bahati mbaya sana wapo baadhi ya watu wanaodhani kuwa kutenda kwao mema kunaweza kuwanusuru na majanga yatokanayo na kukithiri kwa maasi katika jamii.

Dhana hii ni batili na haina ukweli hata kidogo. Nasema hivyo nikirejea maneno ya Allah Aliyetukuka yasemayo:

“Na jikingeni na fi tina ambayo haitowasibu waliodhulumu peke yao kati yenu. Na juweni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Qur’an, 8:25].

Watu wanapojishughulisha na biashara na shughuli nyingine za kujipatia riziki na wakasahau wito wa kufanya ibada, Allah huwateremshia adhabu kutokana na kuacha kwao jukumu la msingi, ambalo ni kumuabudu Allah

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close