9. Khutbah

NAO NI UMAUTI

IMAMU mkuu wa msikiti wa Haqq sheikh Ibrahim Twaha amewataka waumin wa dini ya kiislam kuyakumbuka mauti ili waweze kujitathmini na kuacha kumuasi Allah sw.

Sheikh Ibrahim Twaha ametoa wito huo katika Khutba ya swala ya Ijumaa iliyoswaliwa katika msikiti wa Haqq uliopo karume manispaa ya Morogoro na kusisitiza kuwa ni muhimu kwa muislam kujitathmini ili kuweza kuacha vitendo visivyompendeza Allah Tabaraka Wataalah.

Waislam leo tena tumekutana katika Khutba inayoenda kwa jina la umauti, kwanini nimekuja na khutba hii nzito kwa ajili ya kupeana nasaha ya jambo hili zito ambalo Allah Tabaraka Wataalah, aliwaambia Maswahaba katika surat Zumarah “Hakika ya wewe Muhammad ni mtu wa kufa, na hao wafuasi wako ni lazima wafe, kisha ninyi siku ya Qiyama mbele ya Mola wenu Mtagombana” nikisema Mauti Hakika kila mtu anahisi na anatafakari juu ya mali zake na wake na watoto wake, anafikiria vipi siku atakayotoka Roho na kuacha kila kitu alichokua nacho
Siku ya Qiyama Mtahombana kila mmoja wetu mbele ya Allah Tabaraka Wataalah atakua akimlalamikia Allah Tabaraka Wataalah kua huyu Alinifanyia hivi na yule alinifanya vile, wakati tunagombana Allah Tabaraka Wataalah Anajua nini Hukmu yetu,Na kwa Uadilifu wa Allah atahukumu.

Katika Hadith Nabawi Mtume Muhamad swalallahu 3alayhi wasalam anasema

“Uadilifu wa Allah atahukumu mpaka ugomvi wa wanyama watakaogombana mbele ya Allah Tabaraka Wataalah, wakiwaambia Allah kua huyu alinipigia na Mapembe yake, Allah atahakikisha mbuzi mwenye Mapembe aliyempiga mbuzi asiyekua na Mapembe atahukumu kisha atasema kuweni mchanga na Binadamu huku anaangalia, Mwanadamu akisubiri Hukmu yake nae Atasema Laiti ningalikua Mchanga”

Ndipo Mtume wetu Amesema yakumbukeni sana Mauti Hamtomuasi Allah Tabaraka Wataalah,

“Mauti ni Mamoja hakuna mauti ya Namna Mbili”,

lakini sababu sasa ndo zinaikhtilafiana Sababu za kifo ni nyingi Huyu amekufa sababu yake ni kisukari na huyu amekufa sababu yake ni maradhi mengine

Wachamungu waliopita walikuwa wanafikiri sana umauti, mpaka wengine walikuwa wakifikia anajichimbia kaburi na anajivisha sanda mwenyewe kisha anaingia katika mwanandani wa kaburi lake aliyojiandalia kwa ajili ya mazoezi ya kukumbuka umauti, kisha ndani katika lile kaburi anajiweka ubao wakati anapata joto na anakosa pumzi anajiachia kwa nguvu anaiambia nafsi yake

“Ewe nafsi ulikuwa ndani hapa unafikiria vipi hilo shimo litavokuwa sasa unatubia vipi utarejea kwa Allah subuhana wataalah”?

Anahakikisha anayafanya upya matendo yake, Anayafikiria Mauti kwa mda mchache tu wa Joto alilojionea ama Tabu aliyoipata katika Kaburi lile na Kufikiria vipi wale tunaowazika na Tunawaacha kwa Miaka mingi, vipi wanavyoishi katika ulimwengu huu na wanajiandaa tena kwaajili ya Ulimwengu mwingi yaani Siku ya Qiyama.

Wachamungu waliotangulia walikua wakihamasishana na kupeana khabari na kuwaeleza na watoto wao kua wajipange kwaajili ya Umauti na wakiwaambia watoto wake na wote waliomzunguka Mgonjwa yupo kitandani anafikiria Ataelekea vipi kwa Allah Tabaraka Wataalah Na akisema “Jamani, Macho yanaweza yakakataa mwangaza wa jua na Mdomo unaweza ukakataa Chakula” Alikua Akipenda kula vyakula yofauti na kunywa vinywaji yofauti ila Anakataa kula na kunywa! Kwanini? Ni kwaajili ya Umauti Unamfanya hivi, Roho inataka kuelekea kwa Allah Tabaraka Wataalah, waislamu Mimi na wewe tumejiandaa nini? Kwanini tunaishi katika Mazingira ya Umbumbumbu?.

Asiyekua na Dini anafikiria Umauti, Mwenye Dini anafikiria kufa, Je mauti yanahitaji Elimu? Hapana! Hakuna hitajio la Elimu hapa, Bali hitajio la mauti ni Mazingatio/Kufikiria Mauti vipi itakua, ikiwa anatulilia mimi na weww! Mtume Muhamad swalallahu 3alayhi wasalam, Maswahaba wamembeba na anawaambia nataka nikazuru makaburi ya Uhud, watu wa uhud, watu wa Badir wameinusuru Hii Dini mpaka Allah amewaridhia akasema Mtume Muhamad swalallahu 3alayhi wasalam “Allah kawachunguza na kawaangalia watu wa Badir na akawasamehe kisha akawaambia fanyeni yale mnayoweza”

Hawa ni wenzetu Ambao Wamemridhia Allah na Allah akawaridhia na wao, je, sisi tumemridhia Allah Tabaraka Wataalah?
Mtume Muhamad swalallahu 3alayhi wasalam anawaambia maswahaba yakua “Hakika katika Mauti kuna kilevya” na bado akiwaasa kua msije mkaswali katika msikiti yenye Makaburi kwani Mayahudi na manaswara waliokua akizikwa kiongozi/ Mtukufu wao wanamjengea kaburi au Hekalu na kuna kua na makaburi katika sehemu zao za Ibada, Mtume wetu anatuhadharisha na ushirikina na tusijeingia katika hayo kisha Mtume anaonea Huruma Ummah wake ambao utakuja!

Aidha Imamu Mkuu wa Msikiti wa Haq amesema kitendo cha mja kuyakumbukaka mauti kila mara kitamfanya aweze kudumu katika dunia kwa kuwa na hofu ya Mwenyezimungu.

Waislamu!!

Tukizungumzia masuala mazima ya umauti tunazungumzia ni mtu kubadilika Mtume alivyo tuhimiza twende tukazuru makaburi ameashiria na amekusudia tubadilike Wallahi yeyote yule ambaye akajitahidi kujikumbusha na umauti atamuonea huruma mtoto wake kwamba mpaka sasa hivi kwanini hajahifadhi juzuu moja, kwanini sasa hivi mbona mtoto wangu simuhimizi madrasa ataona huruma lakini nani yule anayefikiria umauti

Na hivi karibuni vijana wetu watajiunga na kidato cha kwanza je tunajiona vipi angalia tunavyoangaika na mambo ya kidunia
Angalia watu wanavyo tembea huku na kule kutafuta shule bora kutafuta yenye mazingira mazuri Anatafuta na kusema kabisa “hii milioni moja lah nataka ya milioni sita”

Anamtafutia mtoto wake mazingira ya dunia lakini mtu huyo anasahau akhera wallahi huu ndo msiba mkubwa na ndio miongoni mwa sababu zilizopelea kuzungumzia khatba hii, lau ukakaa na kufikiri wewe na kujiona si lolote mbele ya Allah kama vile uchafu au mzoga ni wewe ulivyo na wewe ni fakiri na ushahidi wa hili Allah mwenyewe anasema “nyinyi ni mafakiri mbele ya Allah subhanahu wataalah”

Na yeyote ambaye analiona hili silo akatae kufa yeyote yule ambaye analiona hilo silo mimi sifi. Walikufa maimamu wa shia ambao wao walidai ya kuwa maimamu wao hawafi isipokuwa kwa kujipendea

Uliza wako wapi?
Wapo hai?
Allah ndiye mwenye nguvu
Allah ndiye mwenye kiburi
Allah ndiye mwenye kila kitu power zote kwa Allah
Mimi na wewe tunajiandaa kama nani kama maswahaba au tunajiandaa kama akina Abuu jahali

Wallahi tutafakari maneno mbele ya hili
Ni masikitiko makubwa kuona mzazi hana hamu, hana haja, hana hata kuhisi hasira vile ambavyo mtoto wake asomi madrasa, vile ambavyo mtoto wake haifadhi qur’an, vile ambavyo mtoto wake ajui namna ya kuswali. Yeye mwenyewe ajionei wivu wala ajionei hasira wala ajionei “kuna nini mimi katika nafsi yangu”

Na haya yana ushuhuda na nyinyi ni mashuhuda na mimi nimefikisha na mbele ya Allah sote tutaulizwa. Mimi na wewe lini ulikaa kuhangaikia kwamba nahikikisha kuwa milioni sita hii naipeleka katika shule iliyokuwa bora. Hii milioni sita nitahakikisha naboresha mazingira ya walimu wa madrasa, nitahakikisha nalipia wanafunzi vizuri wasome dini yao.

Vyuo mbalimbali vya kidini vina njaa nyinyi mpo,
Vyuo mbalimbali vya kidini watoto wanashindwa kusoma, hawana uwezo wa kipesa nyinyi mpo
Walimu wana shindwa chakula chao cha uhaba…

Hili mtaenda kuulizwa kwa Allah subhanahu wataalah, mali zako umetumia vipi?

Haya ni katika maswala ambayo lazima aulizwe! Mali yako ilivyo itumia sasa ni wewe utajibu vipi
Utajibu ulikuwa ukiwalipia wenzako simba na Yanga ukawalipia watu kumi kuingia kwenye mechi?
Umewalipia watu kumi kuingia kwenye muziki?
Umewalipia watu kumi kwa ajili ya mambo ya hanasa?

Waislamu wapi ni haya mazingira aliyokuwa akiishi mtume wetu
Lah!
Ni mazingira ambayo yako tofauti na sisi

Na je! Ni mazingira ambayo waliishi wema waliotangulia?
Lah!
Sivyo walivyo kuwa wakiishi

Waislamu!
Hawa watoto mnadhani kuwaandalia haya mazingira ya ya dunia ndio utakuwa umemjengea?
Ndio utakuwa umemuweka sawa!!
Lah!
Hatukatai watu kusoma, waosome sana na ndio tunawaitaji sana!?

Lakini hatuhitaji mtu ambaye amesoma tupande mmoja tu hataki kusoma dini yake, mbumbumbu hataki kusikiliza mawaidha, hataki kujisomea hata vitabu

Nini faida ya mtu huyu
Huyu atakuwa ni muislamu, atakuwa ni mwalimu, atakuwa ni trafiki
Atachukua rushwa atachukua kadhaa wa kadhaa
We ni mwalimu, wewe ni daktari, wewe ni trafiki wewe ni kadhaa wa kadhaa basi Uislamu unakutaka usimamie katika haki na wallahi ukisimamia katika haki watu wote wataiga

Na wallahi ukisimamia katika haki utang’ara na ukisimamia katika haki utaridhiwa mbele ya Allah subhanahu wataalah
Wape watoto elimu usiwafanyie hiyana, sio mwalimu usubiri kuchukua pesa tu watoto unawafanyia hiyana unawaburuza buruza tu
Wallahi utaulizwa mbele ya Allah hata kama unawaburuza katika somo pengine la hisabati utaulizwa siku ya kiama
Vile vile kwa fani nyingine mbalimbali toa huruma yako wasaidie wagonjwa katika hali ambayo unaona unao uwezo wa kuwasaidia.
Haya ndiyo mazingira ya kujiandaa na mwisho wako na pia kujiandaa na umauti

Waislamu!

Wallahi tukifikiri sana hatuto watesa wake zetu hauta subutu hata siku moja kama utafikiria umauti
Na haya mimi na wewe ni mashuhuda si tunaona wakati mwenzetu bado hatujamzika tunamuosha tunamvika sanda tunampeleka
Wewe nafsi yako inakuwa vipi mara nyingi nafsi inakuwa ah sitorudia tena katika maasi, kuanzia leo me nabadilika lakini angalia shetani alivyo kuwa na nguvu mtume anasema “shetani anatembea kwa mwanadamu katika mishipa ya damu”

Anaangaika usiku na mchana kuhakikisha namna gani atakupotosha
Ukisha toka tu makaburini mara anarudi katika matendo yake alisema kabisa mimi tena na pombe naacha mimi tena na bangi naacha mimi tena na kadhaa naacha
Mara kidogo anavuta alafu shetani anamwambia utatubia anaanza Allah nisamehe Allah naomba unifutie madhambi yangu
Siku ya kwanza siku ya pili siku ya tatu anarudi vile vile

Wallahi lau tukakaa kufikiria hasa namna gani namna gani ya umauti na namna gani utakavyoondoka utomkera na kumuudhi mke wako utomtesa na kumnyanyasa mke wako utomshidisha njaa utosubutu kwenda kumvalisha asiyekuwa mke wako na kumvalisha mke wako na lazima utampendezesha lazima utamuweka katika mazingira mazuri

Shetani siku zote anakutengenezea mazingira peleka huku huku acha huyu siku siku zote uko nae atapata tu kumbe unamtesa
Na wallahi kwa akina mama lau wakakaa kufikiria nini kifo
Kwa mume wake mwenye uwezo wa kuoa wawili watatu na wanne hatosubu kukataa katika dini ya Allah
Lazima atakaa na kutafakari mauti “mimi napinga hii ayat wakati mume wangu ana uwezo wa kuoa wake wawili watatu kuliko akaenda kuzini akaniletea magonjwa ndani ya nyumba”
Yeye ana pinga huyo ataingia katika mlango wa shetani
Lakini wallahi lau akina mama lau dada zetu wakakaa na kutafakari mwisho wa dunia dunia si lolote wala si chochote dunia ni jambo la kupita mtume alipigia mfano dunia kama vile kivuli mtu anakaa jua likija hivi kivuli kile kinaondoka ndivyo anavyoondoka.

Leo hii wewe utang’ang’ana na kupinga maamrisho ya Allah lakini mara Allah anakuondoa jioni unaondoka hali ya kuwa mpingaji wa maneno matukufu ya Allah subhanahu wataalah

Katika hatua nyingine Sheikh Ibrahim Twaha amewataka wazazi na walezi wa kiislam kuwalea vijana wao katika misingi imara ya dini sanjari na kuwapa elimu ya dini na ya akhera.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close