9. Khutbah

Kutopupia Riziki

MLINGANIAJI wa kimataifa kutoka nchini Burundi Sheikh Zuberi Bizimana amewataka waislamu nchini kuto pupia katika masuala ya utafutaji wa riziki na badala yake kuwa na subra ikiwa ni pamoja na kuzudisha uchamungu mbele ya ALLAH (ametakasika na ametukuka).

Sheikh Zuberi Bizimana ameyasema hayo wakati akitoa khutba ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa katika msikiti wa haqq uliopo mtaa wa Karume Manispaa ya Morogoro.

Aidha Sheikh Zuberi Bizimana ameongeza kuwa ni vyema wanadamu kumtegeme ALLAH (ametakasika na ametukuka) katika masuala ya utafutaji wa riziki zao na sio kwenda kinyume na maamrisho ya mwenyezimungu hali itakayompelekea kutenda madhambi.

Mbali na hayo Shekh Zuberi amewataka waislamu kutokuwa na tamaa ya mali kwani ALLAH (ametakasika na ametukuka) ndio muwezeshaji hivyo ni vyema Zaidi kumtegemea yeye na sio kitukingine chochote katika masuala ya riziki.

 

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close